Mwanamke usipoolewa ni aibu

Mwanamke usipoolewa ni aibu

Ukweli wa namna hii hauvumiliki. Maana hao instagram and Facebook ladies bdo wapo wapo sana hahaaaa
 
Tupa jiwe gizan, litakayempata poatuu

Sent from My GooglePixel using JamiiForums mobile app
 
Of course you have tried to put your point forward in a polite way. But nikuambie tu.

Not all women are cut for marriage. Even if we were created in equality a woman for one man.
Sijui kiinglishi
 
Huwa kuna kitu sielewi kwani miaka 30 ina nini? Maana mnapenda sana kuwasema wadada walio na hiyo miaka

Ukiwa na miaka 30 ujaolewa kuna tatizo gani yaan huwa nawaza sielewi, yaani kisa umefika miaka 30 ujaolewa uanze kuona aibu?



Sent using Jamii Forums mobile app
Point my dear..... hko uliko kunywa kinywaji chochote npo njian kuja kukulipia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maandiko hayajalazimisha kila mtu aoe au kuolewa. Upo mstari ambao unawatambua wasiotaka kuingia kwenye ndoa. Tuache kucomplicate maisha, tuishi kawaida
Upo mstari unaotahadharisha kuhusu kufuta aibu ya kutokuolewa.
 
Ameifuta aibu yake.
Kuna tangazo nilisikia redioni jana (sauti kama ya Mpoki hivi) mwanamme anamuomba mwanamke asiondoke na kumuacha huyo mwanamme kwani yeye mwanamme ana mimba ya huyo mwanamke.

Nikasema makubwa.

Hizi habari za kwamba mwanamke asipoolewa ni aibu ni tabia za jamii masikini.

Jamii masikini, typically zilizokosa elimu, zinamuona mwanamke kama si mtu kamili, mwanamke anakuwa defined kama mke wa fulani au mama fulani. Asipoolewa na kuwa na mtoto hana heshima. Hata akiolewa asipokuwa na mtoto hana heshima.

Ni matokeo ya kukosa elimu.

Mwanamke ambaye hataolewa kwa sababu ametumia muda mwingi sana wa maisha yake kusoma ili agundue dawa ya kansa mimi nitamuheshimu sana tu.

Kutoolewa si aibu. Sababu za kutoolewa zinaweza kuwa za aibu au za heshima kubwa sana.
 
Bado wanakula ujana kwanza, wakishatumika na kuzeeka wanajaa mitandaoni kutafuta watu japo wa kuzaa nao tu tena utawasikia mtoto ntalea mwenyeweeeh!
 
Na wao kutokuelewa kuwa wanapaswa kuolewa....
Gavana wa Arizona, State ya US, ni mwanamke anaitwa Janet Napolitano. Ana miaka 60 sasa. Hana mume, hana mtoto na hajawahi kuolewa.

Alikuwa Waziri katika serikali ya Obama. Watu wanamsifia sana kwamba anapiga kazi kichizi. Labda anapiga kazi kichizi kwa sababu hana distractions za mume wala mtoto na kazi anazofanya zinaweza kuwa zinaenda vizuri zaidi kama hana mume wala mtoto kwake yeye.

Kukosa kuolewa kwake hakujawahi kumfanya asiheshimike. Kwa sababu jamii yake inaelewa kwamba kukosa kuolewa si jambo la aibu na kunaweza kutokana na sababu tofauti.

Ni huko kwetu tu umasikini na ukosefu wa elimu unatusumbua.

Ni bora mwanamke kuishi bila mume kuliko kukubali kuolewa kwa pressure za jamii halafu akaishia kwenye ndoa isiyoisha migogoro.

Janet Napolitano - Wikipedia
 
Daah, wee mleta post sijajua kama unajua maana ya kuolewa. Siyo kuku wote wanaofugwa hutaga mayai na kutotoa vifaranga. Kuku wa kieyeji hujigawa majukumu wenyewe hasa wakiongezeka wakawa wengi.
Utakuta wengine ni kutaga tu. Wengine wanaatamia yaliyotagwa wao hawajui hata yanatagwaje. Wengine wanataga na kuatamia na kulea pia.
Usilazimishe watu waolewe maana swala hilo hata Mungu analijua wazi kwamba hakuna sare ya kufikiri.
Anayeolewa na aolewe na anayezaa bila harusi au kuwa na mme naye kaolewa hivyo hivyo usimdharau.
Unayejivunia ndoa yako sasa waweza kuwa mtoa machozi kwa ajili ya hicho hicho unachokiona bora sasa.
Kizuri zaidi ni kujikubali na kutoinyima nafsi yako daima.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki wanawake.
Sipendi manyanyaso, sipendi dharau. Kila mtu aliumbwa afurahie viungo vyake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I see watu waliolewa na 26yrs walipimaliza tu chuo mpaka mtu anafukisha 34kafungiwa kwa mume no kazi no business maisha gani hayo wadada tafuten maisha kwanza waume mtawapata hata wajane chaaaa

Hamna kitu kama hicho. Mpaka mtu anakua hvyo dunia hii ya sasa yenye smartphone na instagram huyo mwanamke ametaka mwenyewe tu.

Hakuna mwanaume anayependa kuwa na mke tegemezi all day everyday labda huyo mwanamke awe hajitambui au hana nidhamu kwa mme wake.
 
Back
Top Bottom