Sikatai...hakuna mwanamke asiyependa kuolewa. Ni ndoto ya mwanamke yoyote yule.
Ninachoongelea mimi ni ile mwanamke umri umeenda hajapata mume kashfa zinaanza juu yake na ndio hapo anapoamua tu aolewe na yoyote ili kuepukana na aibu.
Kuolewa/kuoa kunahitaji utayari na pia upate mtu unayedhani ni sahihi kwako na si tu ujilazimishe kwasababu umri unaenda na jamii inakushangaa.
Kukashifu mwenyewe naungana na wewe sio jambo jema...lakini wapo kabisa ambao hizo kashfa watakuwa wanazistahili baadae hao nafikiri ambao bado hawajawa victims,ni bora wakajifunza kwa Uzi huu
Check and analysis
At 16-20 wasichana mnapata tamaa ya kuwa na mwanaume kwa vigezo vya maumbile yake... Vitu kama handsome,mweupe...mrefu nk
20-23 mnafundishwa kuwa mwanaume anatakiwa kuwa na fame ya uanaume wake,yaani awe na nguvu tuu au wa kwanza sehemu muhimu mfano mchezaji bora,msanii,mwanamitindo nk ...yote haya yanabebwa na namna ya kumudu changamoto zenu kimaisha,issue ya pesa au kuwa njema hapa ndio huwa ina nafasi...
Na hapa mewapoteza wengi ambao pontentially walikuwa hivyo subira kidogo tuu mngewapata...ndio wengi mnajutia kwa ma ex wenu,hatari ya hapa wengi wenu pia huwa mnafikiri mtakuwa kwenye mahusiano milele kwa hiyo mnatumia nafasi hii kuponda raha na kusahau ya muhimu kwa mwanamke
Wanaume wa hapa huwa wanachukuliwa na wenzenu wajanja wa 25-28...ambao wao huwa wanashtukia kuwa kuna cut off time kwa hiyo wanawinda yeyote anaekuwa average
Hapa 29 kuendelea...wengi wanaolewa na watu wasio wapenda kisa presha tuu...na sio nzuri
Wengi hapa kisingizio eti ilimradi awe Mchamungu..."God forbid mchamungu wakati mnazini au mnafanya uasherati kila Sikh???"...
Cha msingi Dada zangu hasa mlio chuo,usifikirie assignments tuu...anza kumtafuta baba wa watoto wako sasa hivi,sisemi uanze kutongoza nooo...
Anza kujibrand kama potential good wife,potential good husbands watakuja na Muombe Mungu atakuonesha your Mr Right