Mwanamke usivunje ndoa kisa michepuko ya mumeo

Mwanamke usivunje ndoa kisa michepuko ya mumeo

Cosovo

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2018
Posts
667
Reaction score
1,810
Mwanamke elewa kuwa asili ya mwanaume ni udume ambao anahitaji atawale dunia kwa kila kitu. Wanyama na ndege pia viumbe vya kiume hutawala species zao.

Kwa hiyo basi fanya ufanyalo mwanaume lazima achepuke, hata umlambe makunyanga yake lazima achepuke, hii siyo tabia ni nature ya viumbe vya kiume. Kuna mdada alimuacha mume wake akimtuhumu kuwa anachepuka, baada ya miaka miwili akaolewa na mwanaume mwingine ambaye sasa alikuwa anachepuka mpaka anahama mji.

Akaachika na kuolewa kwa mwanaume mwingine ambaye kila mwezi lazima amlete barmaid nyumbani na kumuamrisha mke wake awapikie. Baada ya kupitia mitanange miwili amerudi kwa mume wa kwanza anamsihi warudiane lakini jamaa anakataa na harusi inakaribia.

Mwanamke baada ya kuona jamaa hamuelewi anaanza kumtishia kumroga na binti bibi harus mtarajiwa. Enyi wanawake tulieni kwenye ndoa zenu, kuchepuka ni nature ya wanaume.

1643695042481.png
 
Kuchepuka hawatukatazi wanachotaka heshima ifate mkondo
Right is right even though no one is doing & wrong is wrong even though all people are doing, usitake kuaminisha watu phalsapha yako ya zinaa, kuchepuka itabaki kuwa uovu tu hata kama wanaume wote chini ya jua watachepuka ila hawezi kubadili dhambi kuwa haki, never.
 
Hivi huu ufahamu wa kishetani aliwapaga nani ???

Nani alikuambia kila mwanaume lazima achepuke kama wewe rafiki zako ndugu zako na watu wanaokuzunguka wanachepuka ni hao usije na conclusion zako kutokana na circle yako na stori unazisikia

Msimamo wangu ni huu mwanaume ambaye hana hofu ya MUNGU (mahusiano na Mungu binafsi) huyo kuchepuka ni lazima wala sio hiari ,mwanaume mwenye hofu na MUNGU kamwe hawezi chepuka haijalishi nini

Note:Sijasema wanaoenda kanisani au walokole au wasabato ni wenye hofu ya MUNGU maana unaweza kulala garage usiamke gari.
Period
 
Hivi huu ufahamu wa kishetani aliwapaga nani?
Though nakubaliana nawe kwa 100%, mwanaume mwenye hofu ya Mungu hatochepuka, ila je wako wangapi? Nadhani kwenye 1000 utabahatika sana ukiwapata wawili. Kuna kitabu kinasema, kwa nukuu isiyo rasmi, kuwa UAMINIFU WA MWANAUME HUTEGEMEA HIS OPTIONS.
 
Right is right even though no one is doing & wrong is wrong even though all people are doing, usitake kuaminisha watu phalsapha yako ya zinaa, kuchepuka itabaki kuwa uovu tu hata kama wanaume wote chini ya jua watachepuka ila hawezi kubadili dhambi kuwa haki, never.
Hata kama ni dhambi mkuu pia acheni nature ifanye kazi
 
Wala wanawake hawana presha na kuchepuka kwenu siku hizi....

Wao wenyewe wanachepuka.

Nani hataki raha ya penzi jipya?

Nani hataki mashamsham ya mcheps?

Kuna vijana wanasimamia kucha aisee na kunyonga viuno kama feni mbovu!!!!

Kwa hiyo mnywe maji mengi tu na muendelee kuchepuka.....

Mume akichepuka kushoto...mke anachepuka kulia ...mnarudi nyumbani wepesiiiiii

Afterall haiachi alama!!!

Wala haiishi!!!
 
Baba Mtakatifu (Papa) juzi ndo alitupiga Wakatoliki kwa kitu chenye ncha kali kichwani eti kuzini ukiwa ndani ya ndoa siyo dhambi kubwa.
Kwel kabsaa kuzin sio dhambi kubwa (japo kwa Mungu hakuna dhambi kubwa na ndogo) maana kuzini ni matokeo ya dhambi ya tamaa na kukosa heshima. Kama leo hii ukiweza kuzishinda dhambi za tamaa na kiburi bas hauto angukia kwenye uzinzi tena
 
Kuliko kubaki kwenye ndoa kwa maisha ya sononi na kukosa furaha sababu ya Mwanaume malaya ni bora kuchagua kuondoka kwenda kutafuta Furaha na amani yako ewe mwanamke.

Ndio maana ni muhimu Mwanamke kuwa na kipato huru bila kutegemea K ili uishi mjini.
 
Hivi kwanini hii mada isitangazwe kwenye magazeti ili wanawake wote waione

Mleta mada taja namba ya akaunti fasta nkutumie 20,000
 
Mwanaume mpaka unaamua kwenda kuchepuka na Mwanamke mwingine maana yake kuna kitu umekikosa kwa mkeo ukaenda kukipata kwa mchepuko, sasa mwanamke wa ndoa akiamua kuondoka ndoa ikavunjika ili akupe nafasi uendelee na mchepuko wako kuna ubaya gani?

Maana wengine huwa hawaishii kuchepuka tu lakini na kuzaa na mchepuko, imagine?!

Mke wa hivyo naona ni muungwana sana na asiependa shari anayeamua kuachana kwenye ndoa.

Mshika mawili Moja humponyoka.
 
Back
Top Bottom