Mwanamke wa kiislamu alivyorudisha mamilioni aliyookota

Zee la madawa

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2022
Posts
1,895
Reaction score
4,478
Kuna Taarifa kuhusu mwanamke Muislam kutoka Lapai, Jimbo la Niger, Nchini Nigeria anaeitwa Hajiya Aisha Isah Yelwa ambaye alirudisha Naira milioni 330 zilizo ingizwa kimakosa kwenye akaunti yake ya benki

Kwa Ufupi ni kwamba Aligundua kiasi hicho kilichopokelewa bila sababu ya dhahiri kwenye akaunti yake ya First Bank mnamo Desemba 29, 2025.

Badala ya kutumia fedha hizo, aliripoti suala hilo benki na mamlaka husika asubuhi iliyofuata.

Benki ilithibitisha kuwa ilikuwa ni makosa ya mfumo wa malipo na ilirejesha fedha hizo mara moja.

Utekelezaji wa kitendo chake umepokelewa kwa Namna Tofauti

Wengine wameshutumu na wengine wameona kama mfano wa uadilifu mkubwa, haswa ikizingatiwa hali ngumu kiuchumi ambayo inaweza kuwatesa wengi kutaka kutumia fedha zisizo zao.

Kitendo cha Hajiya Aisha kinatoa fursa nzuri ya kufikiri kwa undani kuhusu imani, uadilifu, na utamaduni sio tu kwa Waislamu bali kwa jamii kwa ujumla.

Katika dini ya Kiislamu, uadilifu ni mojawapo ya sifa muhimu sana.

Qur’ani na mafundisho ya Mtume Muhammad Swalallahu Aleyhi wasalam yanasisitiza sana kuheshimu mali ya wengine

Qur’ani inasema wazi kwamba mali ya mtu mwingine ni takatifu na haiwezi kuchukuliwa bila idhini ya Mmiliki.

Kama dini, Uislamu unafundisha kuwa dhulma ya mali si halali hata kama imekuja kimakosa, na msamaha au kurejesha mali ni tendo la thawabu katika maisha ya baadaye akhera.

Hivyo, kitendo cha Hajiya Aisha kinazingatia mafundisho haya kwa kuonyesha kwamba kuzuia matumizi ya mali isiyo yake ni sehemu ya imani ya kiroho na maadili ya Kiislamu.

Ingawa hadithi hii imejidhihirisha kwa mfano wa mwanamke Muislamu, uaminifu na uadilifu si sifa zinazokua tu kwa Waislamu, bali ni kanuni ya maisha bora kwa binadamu wote bila kujali dini au tamaduni.

Hata hivyo, katika jamii nyingi za Kiislamu, matendo ya ukubwa wa aina hii mara nyingi hupokelewa na pongezi zaidi hasa pale wanapoeleweka kuwa wamefanya hivyo kwa sababu ya imani yao.

Hadithi kama hii mara nyingi hufanya watu wa jamii kujiuliza

Kwa nini baadhi ya watu wanamuona kama “jazba ya kusalia na fedha” badala ya sifa nzuri?

Kuna shinikizo la kiuchumi ambalo linaweza kuwafanya wengi “kujaribu bahati” kuliko kurejesha fedha?

Maadili ya mtu binafsi mara nyingi yanaweza kupimwa zaidi wakati wa majaribu kuliko wakati wa furaha.

Kitendo cha Aisha kinakumbusha jamii kuwa maadili na uadilifu bado yanathaminiwa, ingawa wanaweza kukosolewa au kulindwa kwa misimamo tofauti.

Kwa mujibu wa ripoti zingine kutoka Nigeria, kumekuwa na mfano mwingine wa mwanamke aliye rudisha N4. milioni‎ 8 zilizo wekwa kimakosa kwenye akaunti yake na alipata shukrani na zawadi kwa kitendo chake hicho.

Hii inaonesha kuwa sifa za uaminifu na uadilifu huchochewa na dini, kijamii na mara nyingi pia huenda zikatambulika na jamii kwa njia chanya.

Swala la Uwaminifu kwa Waislam Linaendelea kupamba moto, Waislam wengi wamejizolea Sifa kubwa ya Kurejesha amana ya watu Pindi wanapo Gundua si Halali yao.
 
Amerudisha Hela mtu binafsi, unasifiwa uoslamu wote, na waislam sifa hizo wanazipokea.
angelawiti musilamu sifa ya ulawiti waislam wangeikataa.
Uaminifu na Uadilifu hauchagui dini ya mtu au kabila la mtu.
Tuacheni mihemuko
 
Amerudisha au hakurudisha, Bank wangepata pesa yao tuu, na inaonekana nia ya uzi ni udini tuu, acha ujinga
 
HIi habari ukiangalia kwa jicho la kawida ni kuupa uislam promo. Pili hata kama asingetoa taarifa au kurudisha hizo pesa ingejulikana na asingeweza kuzitoa achilia mbali kuzitumia. Tatu hata angetoa na kutumia angelazimika kuzirudisha maana si zake na zimewekwa kwenye acc yake kimakosa. Hamna jambo la ajabu hapo.
Ni kuupa uislam sifa za kijinga
 
Bank ya NMB huwa wana hiyo tabia ya kujikosesha wanawekea watu pesa hasa watumishi ambao akaunti zao wanapitishia mishahara!

Wewe jifanye hamnazo uzikwapue,unakuwa umekopeshwa wanakuita urudishe au waanze kukufyeka!!
 
Uaminifu hauhusiani na dini. Huyu msouth Africa wiki iliyopita alirudisha $400,000(zaidi ya bilioni 2 za kitanzania)
Hivi visa vya watu kupata au kuokota mamilioni na kurudisha kwa wenyewe vipo vingi Sana, havuhusiani na dini.
 
Attachments

  • Screenshot_20260102-200611_1.jpg
    Screenshot_20260102-200611_1.jpg
    295.8 KB · Views: 31
Tunampongeza huyo dada ila sio uislamu wake

Japo angechukua hata 10% na benki wasingejali
 
Amerudisha Hela mtu binafsi, unasifiwa uoslamu wote, na waislam sifa hizo wanazipokea.
angelawiti musilamu sifa ya ulawiti waislam wangeikataa.
Uaminifu na Uadilifu hauchagui dini ya mtu au kabila la mtu.
Tuacheni mihemuko

Pamoja na kwamba siwapigii debe ILA ukiwa na biashara ambayo huna nafasi ya kuisimamia kwa karibu tafuta Muislam anayesali, umuweke hapo akusaidie kusimamia; Utanishukuru baadae!
 
Hujui kitu wewe,niulize mimi!!!

Nilienda kuchomokea fidia ya Tsh 10,000,000/= mahakama ya rufaa Ilala baada ya kunibunia kesi na kunishinda mahakama ya mwanzo Kariakoo baada ya kuahidiana pesa na wafanyakazi wa mahakama,mpaka leo nikimtizama huwa siamini na toka siku hiyo mtu anayejifanya ana Mungu sana sitaki hata kumsikia.
 
Back
Top Bottom