Mwanamke wa Miaka 76 ajifungua Mtoto wa Kiume, Ethiopia

Mwanamke wa Miaka 76 ajifungua Mtoto wa Kiume, Ethiopia

bro alex

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2025
Posts
1,889
Reaction score
2,294
Tukio la kushangaza limeripotiwa mjini Mekelle, makao makuu ya Jimbo la Tigray, Ethiopia, ambapo mwanamke mwenye umri wa miaka 76, Woizero Medhin, amejifungua mtoto wa kiume. Tukio hilo limetajwa na wengi kuwa la kimiujiza, likifananishwa na simulizi la kibiblia la Sara aliyejifungua akiwa na miaka 90

Akizungumza na kituo cha Dimtse Woyane News, Woizero Medhin alisema, “Sikuhisi nilipopata mimba… Ilikuwa ni mapenzi ya Mungu.” Ingawa tarehe halisi ya kujifungua haijatajwa, taarifa hiyo imetolewa leikiwa ni siku ya ubatizo wa mtoto, jambo linaloashiria kuwa mtoto huyo alizaliwa takriban siku 40 zilizopita, kwa mujibu wa mila za Kanisa la Orthodox Ethiopia

Ingawa ripoti rasmi ya kitabibu haijatolewa, taarifa kutoka mitandao ya kijamii zinaeleza kuwa mama huyo alijifungua kwa njia ya kawaida bila upasuaji. Katika video iliyosambazwa, familia na marafiki waliandaa sherehe kubwa ya ubatizo, huku kijana mmoja wa familia akitamka kwa imani, “Kwa Mwokozi Mtakatifu hakuna lisilowezekana.”




Borkena
Updated on February 7, 2025
 
Nimeweka screen short ya taarifa na tukio limetokea MWEZI WA pili hivo INGEKUA fake news wange batikisha
 

Attachments

  • Screenshot_20250726-100551.png
    Screenshot_20250726-100551.png
    453.9 KB · Views: 43
Huyo haitwi bibi bado hajajukuu maana hana mjukuu
Ahaaa mi nimemuita bibi SABABU UMRI wake MKUBWA SANA Miaka sabini na SITA Ina maana ni MKUBWA sanaa hata kwa mama yetu WA taifa. Basi nmeielewa mkuu🙏🙏🙏

Kwishaaaaaaaa
 
Weka link ya source ya taarifa hiyo.

Tupime habari kubwa kama hiyo, je imewekwa kwenye source zinazoaminika ama ni wahuni tu wamezusha
 
Ujiue kisa kukosa mtoto !?

Huo si-uchizi
Ndio wanajiua SANA TU SI unajua MANENO ya waja WA mwenyezi MUNGU ACHA TU mkuu.

ZILE kauli za mawifi, unajaza TU choo cha kaka yetu kuzaa HAMNA SI uwende KWEnu. DAH hua inauma SANA kama SI mcha MUNGU unajikuta ni chakula cha waganga kuliwa tunda kimasihara ILI azae maskini..


Kwishaaaaaa
 
Weka link ya source ya taarifa hiyo.

Tupime habari kubwa kama hiyo, je imewekwa kwenye source zinazoaminika ama ni wahuni tu wamezusha
NDUGU YANGU samahani Kuna screen shot nimeweka HAPO JUU Ina taarifa zaidi likiwemo jina la mlengwa hivo UNAWEZA search na ukjiridhisha SABABU MPAKA interview zake zipo kibao TU una ona mkuu. Sorry


Kwishaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom