Tukio la kushangaza limeripotiwa mjini Mekelle, makao makuu ya Jimbo la Tigray, Ethiopia, ambapo mwanamke mwenye umri wa miaka 76, Woizero Medhin, amejifungua mtoto wa kiume. Tukio hilo limetajwa na wengi kuwa la kimiujiza, likifananishwa na simulizi la kibiblia la Sara aliyejifungua akiwa na miaka 90
Akizungumza na kituo cha Dimtse Woyane News, Woizero Medhin alisema,
“Sikuhisi nilipopata mimba… Ilikuwa ni mapenzi ya Mungu.” Ingawa tarehe halisi ya kujifungua haijatajwa, taarifa hiyo imetolewa leikiwa ni siku ya ubatizo wa mtoto, jambo linaloashiria kuwa mtoto huyo alizaliwa takriban siku 40 zilizopita, kwa mujibu wa mila za Kanisa la Orthodox Ethiopia
Ingawa ripoti rasmi ya kitabibu haijatolewa, taarifa kutoka mitandao ya kijamii zinaeleza kuwa mama huyo alijifungua kwa njia ya kawaida bila upasuaji. Katika video iliyosambazwa, familia na marafiki waliandaa sherehe kubwa ya ubatizo, huku kijana mmoja wa familia akitamka kwa imani,
“Kwa Mwokozi Mtakatifu hakuna lisilowezekana.”
Borkena
Updated on February 7, 2025