Mwanamke wangu niliyezaa naye tumezinguana. Roho inaniuma naombeni ushauri wenu

Mwanamke wangu niliyezaa naye tumezinguana. Roho inaniuma naombeni ushauri wenu

Mfia nchi

Member
Joined
Jul 18, 2019
Posts
89
Reaction score
164
Member wote wa JF kwangu ni kama sehemu ya familia. Humu unaweza kupata ushauri mzuri sana ambao unaweza kubadirisha maisha yako ina a positive way.

Ndugu zangu kwa huo utangulizi naombeni ushauri wenu kuhusu haya mahusiano yangu.

Siku ya Xmass nilileta uzi humu kuhusu wife kunikamata red handed nikijiandaa kutoka kwenda kula Xmass na mama wa mwanangu japo wengine mlimuita mchepuko.

Siku ile nilienjoy vizuri tu na mama wa mwanangu na niliweza kurudi mapema nyumbani ili kumtuliza wife. Wife nilimkuta ana huzuni kubwa hata kula hakuweza.

Niliingia nikiwa nimevaa sura ya upole na kumkalisha wife chini na kuzungumza naye.

Nilimuomba wife ajaribu kunielewa. Utetezi wangu mkuu ulikuwa ni kwamba "yule mwanamke nimezaa naye, hivyo mtoto wake hana tofauti yoyote na hawa watoto wetu wa humu ndani, hivyo hata yeye na mtoto wake wanastahili better treatment as you and our children".

Wife kwa sababu ananipenda hakutaka kuongea sana ila aliendelea kununa japo baadae alikaa sawa na amani ndani ya nyuma ilirejea.

Ushauri ninaouomba kwenu ni kuhusu huyu mpenzi wangu niliyetoka naye siku ya Xmass. Jumapili ya 29 Dec nilimtaarifu huyu mama wa mwanangu ningekuja kwao kumchukua tuende zetu sehemu lakini alinikatalia kwa kisingizio eti kachoka anataka kumpumzika.

Nilimwambia hatutaenda mbali, nataka tutoke kidogo tu then tutarudi. In fact yeye alihisi nataka kwenda kula tunda hivyo alikuwa anadai yeye amechoka na mimi nilimsistizia lengo langu wala sio kula tunda.

Baadae alikubali akasema nimfuate. Basi muda umefika namcheki kwenye simu nakuta simu haipatikani, nikaendelea kumcheki now and then bado tu simu haikupatikana. Baadae baada ya kupita kama saa moja hivi akapatikana.

Swali la kwanza nilimuuliza kwa nini simu umezima, akasingizia eti network ndio shida ila hakuzima simu.

Nilihisi anaongea uongo hivyo nikampandishia, nikamkoromea akanikatia simu na kuizima kabisa. Baada ya kama nusu saa hivi simu ikaanza kupatikana tena. Nilichomwambia tusijuane.

Kusema ukweli huyu mwanamke nampenda na hapa nafsi inanisumbua sana. Najishauri sijui nimrudie, sijui nimpotezee mazima tu. Naombeni ushauri wenu.

Kama huna cha kushauri naomba upite kimyakimya tu badala ya kutoa kejeli.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.
 
Mtafute tu maana ni mzaz mwenzio
Afu kwa sasa tambua hauna mamlaka sana kama angekua mkeo wa ndani
Ko usimpeleke peleke unazidi kumuudhi.

Kwanza kwanini hukumuoa yeye?

Sent using Jamii Forums mobile app
Shukrani mkuu. ...Sikumuoa kwa sababu tayari nina mke ila nataka nimuoe hivyo hivyo hata kwa taratibu nje ya dini. ...By the way nikimtafuta si ataniona najipendekeza? Mimi mwenyewe ndio nilimwambia tusijuane halafu tena mimi ndio nianze kumtafuta huoni kama atachukua point zote tatu?
 
My brother, ni bahati nzuri ule uzi wako wa awali niliusoma vema.

There is a mistake you are doing. Tunapoowa au kuolewa (kwa wanawake) mara nyingi huwa tuanaacha mahusiano huko nyuma. Implication ni kwamba, kama hayo mahusiano umeyaacha na kuoa mwanamke mwingine, it means the former is irrelevant, not suitable, not material for your life etc.

Mi pia ni mtundu wa kuchepuka (na kwa kweli nina mtoto nje ya ndoa) ila namheshimu sana mke wa ndoa. I try every possibility and any possible janjafullness kuhakikisha communication ya mi na mchepuko haimfikii mke. Pia (with black and white) mchepuko anafahamu mi sio mmewe, on top nampa conditions za mawasiliano yoyote na mimi,

Usimhuzunishe mkeo, huyo ndio rafiki yako mzuri duniani. Anafahamu afya yako umelalaje leo, anaamua akupikieje nk. Wanawake ni wadhaifu, ila udhaifu mwingine tunawapa sisi waume zao. Hebu fikiria hili, kama alikamata mawasil;iano yako na mchepuko wako, ana uhakika wa mahusiano yenu. Waza tena, unaonaje leo au kesho akilipiza kisasi kwako kwa yeye kupata mchepuko ili iwe jino kwa jino, jicho kwa jicho?

The cicle goes like that. Wanaume tujifunze, huwezi kuonja kila mwanamke. Tufike mahali tuzame kujenga familia tu, mengine ya michepuko tuuite ujinga. Uhusiano wako na mzazi mwenzako usiathiri family base yako. Your family is your best status, the glory that God has given you. Amini hili hapa, Any family conflict, the most affected are children. Dont torcher your children please, dont torcher your wife. Itendee haki familia yako. Lea na hudumia mtoto wa yule dada, then dont think beyond that.

Sorry sijafanya proof reading maana sio thesis hii
 
Shukrani mkuu. ...Sikumuoa kwa sababu tayari nina mke ila nataka nimuoe hivyo hivyo hata kwa taratibu nje ya dini. ...By the way nikimtafuta si ataniona najipendekeza? Mimi mwenyewe ndio nilimwambia tusijuane halafu tena mimi ndio nianze kumtafuta huoni kama atachukua point zote tatu?
Nishakuambia Hujitambui.
Acha basi kutusumbua au!?
 
House of Commons,
Shukrani mkuu. Wife nampenda sana. Huwa akitishia kuondoka huwa naona dunia imefika ukingoni. Kiufupi wife means a world to me. Tatizo huyu mama wa mwanangu nampenda kinyama na nikiwa naye faragha huwa ananikuna kisawasawa. Ni wale mademu wenye utundu wa asili, pia she is very beautiful. Kumuacha aende zake sio rahisi as simple as people may think.
 
Yaan unaweka nguvu kwa mchepuko eti kisa mmezaa naye, mkeo ni mgumba? Mkeo anaweza pata mchepuko ukamvumilia? Jitahidi mchepuko apande chat uone kama watoto wako hao watakuwa na amani na malezi mazuri pumbavu kabisa! Mkeo toka umuoe mnatoka out mara ngapi kwa mwezi?
 
Shukrani mkuu. Wife nampenda sana. Huwa akitishia kuondoka huwa naona dunia imefika ukingoni. Kiufupi wife means a world to me. Tatizo huyu mama wa mwanangu nampenda kinyama na nikiwa naye faragha huwa ananikuna kisawasawa. Ni wale mademu wenye utundu wa asili, pia she is very beautiful. Kumuacha aende zake sio rahisi as simple as people may think.
Dah pole sana mkuu, kwa maelezo haya kwakweli bado upo nja panda!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom