TANZIA Mwanamuziki Hussein Jumbe afariki dunia

TANZIA Mwanamuziki Hussein Jumbe afariki dunia

Mimi sio mzee ila nyimbo za hawa wazee huwa zinanipa burudani sana.
R.I.P Mzee nasi tupo njia hiyohiyo kasoro tu umetutangulia.
 
Hakika dunia ni mapito tu na itabakia milima tu.

Namkumbuka sana mzee wa KUCHECHEMEA ...HUSEIN JUMBE pale kisuma mbagala na Mwembe Yanga hakika nalia kwa uchungu sana ingawa ndiyo kazi ya Mungu haina makosa.

Jamaa ametutoka ameitwa na maanani ili neno litimie.
 
yaani maisha yako yote mpaka mauti yanakukuta mishe zako ni kazi miongoni mwa kazi za Shetani(muziki) dah !

eeh Mwenyezi Mungu tujaalie mwisho mwema 🙏
 
Hii ndio Taarifa iliyotufikia hivi punde , na kwamba Mzee Hussein Jumbe amefikwa na umauti katika Hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam leo 10/4/2023

Enzi za Uhai wake aliwahi kutumikia bendi za DDC MLIMANI PARK na MSONDO NGOMA

Aliwahi kutamba na Kibao chake cha "Nachechemea"

Apumzike kwa Amani .

---

Tasnia ya Muziki wa Dansi imekumbwa na majonzi makubwa baada ya aliyekuwa Nguli wa Muziki huo, Mzee Hussein Jumbe, kufariki leo Aprili 10, 2023 katika Hospitali ya Amana, alipokuwa akipatiwa Matibabu

Mzee Jumbe maarufu 'Mzee wa Dodo' alitamba kwa nyimbo kali alizowahi kuandika ikiwemo 'Nachechemea' na amewahi kuwa katika bendi za Tabora Jazz, Mara Jazz, Urafiki Jazz, DDC Mliman Park ‘Sikinde’ na TOT Band, Juwata Jazz na Mikumi Sound

View attachment 2583799
Siri ya nini,wimbo bora kwangu Mungu amlaze mahali anapostahili
 
Back
Top Bottom