TANZIA Mwanamuziki Maunda Zorro afariki dunia kwa ajali ya gari, mazishi Jumamosi Aprili 16, 2022

TANZIA Mwanamuziki Maunda Zorro afariki dunia kwa ajali ya gari, mazishi Jumamosi Aprili 16, 2022

Kuna jingine lilikuwa linaitwa GEMA LAO sjui bado yapo yalikuwa yanakimbia sana
Yes, GEMA LAO nalikumbuka, yakifika pale mjimwema shule yanalala na speed kubwa kiasi tairi zinaserereka kabisa. Wakitoka njia ya kibada kuja mjimwema waende huko mwongozo, ni 100 tu, hapo zinagongwa horn tu, poh, pooh. Wameshasababisha ajali mara kadhaa.
 
Mwanamuziki Maunda Zorro, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo (Alhamis ya April 14) baada ya gari alilokuwa amepanda aina ya VITZ kugongana uso kwa uso na lori la mchanga huko Kigamboni, Dar es Salaam.

Maunda Zorro ni mtoto wa muimbaji nguli wa muziki Zahir Ally Zorro pia ni mdogo wa mwanamuziki Banana Zorro.

Maunda Zorro aliwahi kutamba na vibao kama vile 'NATAKA NIWE WAKO' na 'MAPENZI NI YA WAWILI' ambavyo mpaka sasa vinapendwa na wapenzi wa muziki kwani ni aina ya muziki usiochuja.

Apumzike kwa Amani

=============================
Kaka wa marehemu ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Banana Zorro amesema:

"Nimezipata hizo taarifa ndio naelekea Hospitali ya Kigamboni, taarifa ni za kweli tulikuwepo kwenye msiba jioni ya leo wa rafiki yetu mwingine wa karibu, nilikuwa nae Maunda hadi jioni saa 11 hadi 12 nikarudi nyumbani kulala maana msiba ulikuwa Kigamboni na yeye anakaa Tuangoma.

"Chanzo cha kifo ni ajali ya gari, niliachana na Maunda saa 12 jioni ajali amepata mida ya saa 4 usiku, ila sina uhakika sana (wa muda aliopata ajali) hadi nikifika Hospitali maana nilirudi nyumbani nikiwa nimechoka sana."

View attachment 2186717
View attachment 2186720

Rest easy dada. Nakuombea Mizimu yetu waipokee roho yako!
 
Back
Top Bottom