Mwananchi: Kwenye daftari la mazishi ya vifo vya COVID19 Jina la babangu lilikuwa namba 256 (Amana Hospital-Ilala)

Bora vyombo vya kimataifa sasa vitumike kueleza nini kinaendelea hapa nchini ili watu wajue hali halisi ikoje.
Tutaamini vp na hivyo vyombo vya nje au hapa tunachagua wa kumuamini na si kuangalia uhalisia wa kinachosemwa? Hebu vuta picha kama sie wenyewe tu ambao ndio tunaishi hapa Tz ila tunatofautiana kwenye vifo vya corona wengine wanasema watu wanakufa sana wengine hawaoni hao watu wanaokufa sana na wote tunaishi nchi mmoja,sasa hivyo vyombo vya nje nao tutawaamini kwa lipi?
 
Wewe jua taarifa za mwisho wagonjw walikuwa 480,vifo 20.

Ikitoka taarifa nyeingine ndio itakuwa ya kushika.
 
Bora mabeberu waseme. Maana sisi huku habari hatuzipati kabisa yani hakuna updates.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo lilivyo hata huku mitandaoni hakuna mashuhuda wa waliyofiwa na ndugu zao au hata majirani kwa vifo vinavyojulikana kabisa ni vya corona ili kuja kutoa ushuhuda ili tupate picha halisi kinachoendelea kuhusu corona.
 
Mkiandika kwa lugha hii hata beberu wa.chato hatakuja elewa mnazungumzia nini hata police hawawezi angaika na habari kama hii sababu watanzania wengi hawaelewi hii lugha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa 256 ndio wanatushadadia namna hii? Mbona USA kuna vifo zaidi ya 80,000?

Magu voice
Kwa kuwa uwezo wako wa kufikiri ndio umeishia hapo ndio maana umeandika ulichokiandika. Naomba ufanye hesabu ya Kutafuta CASE FATARITY RATE (CFR) kati ya Tanzania na huko USA halafu utagundua ni nchi gani tatizo lipo kubwa usiangalie idadi ya vifo pekee piga hesabu ndugu.
 
Wewe jua taarifa za mwisho wagonjw walikuwa 480,vifo 20.

Ikitoka taarifa nyeingine ndio itakuwa ya kushika.
Kwahiyo hadi sasa tujue ya kwamba hakuna maambukizi mapya hivyo kwa takribani wiki tatu sasa, watanzania tumejitahidi kupambana na hili janga la covid-19? Ama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaokufa ni binadamu na ni wapendwa wetu na ndugu na jamaa
Kutoa takwimu labda wanaona wananchi watakuwa na woga sijui
Lakini huku kwingine takwimu zinatolewa kila siku ingawa takwimu haziko sawa kwa sababu kadhaa lakini zinakaribiana

Nafikiri wakitaja takwimu za ukweli hata kwa wanaokufa hospitali tu

Ingawa ni vigumu kupata vipimo kila hospitali kugundua kuwa kafa kwa nini
Lakini waataje kama kawaida yao kafa kwa changamoto za upumuaji
Sisi tumetajiwa takwimu za vifo na hii imepelekea tujichunge zaidi ila huko mnachukulia kawaida Kwa sababu hamuambiwi ni wangapi wamepoteza maisha


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Hii habari haiwezi kuwa ya kweli!! Hakuna kitabu cha kurekodi watu waliokufa na corona tu!! Kinarekodi marehamu wote. Kwa hiyo huyo mzee alikuwa ni marehemu wa 256 katika orodha ya kitabu hicho. Ni vifo vya magonjwa mbali mbali mbali. Uongo uko hapo!!
 
Hizi media za nje ni mandumi ya kuwili, yamefanya propaganda kibao duniani zilizoleta machafuko. Hatuwaamini tena, mutuachie mambo yetu ya ndani tupambane nayo wenyewe sio kutupangia cha kufanya. Tunajikuna pale mkono unapofika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…