Mwananchi waomba radhi baada ya wananchi wengi kupiga kura ya kuridhishwa na Sera za Uchumi za Magufuli dhidi ya marais wengine

Huwezi kumnyima 'credit' zake juu ya hao wachimbaji wadogo wadogo wa madini na soko la madini. Huwezi kuuficha ukweli huo kwa yeyote.
Katika ukichaa wako, kuna mambo mazuri aliyafanya pia.
Ukweli upi Sasa? 🀣🀣 Mbona mnalazimisha mliyoshindwa? 😁😁😁😁

Nimekueleza Samia kawapelekea umeme,kawanunulia mtambo wa Utafiti,kawajengea soko la Madini na kawapelekea Huduma za ugani wa Madini za GST kule Chunya.

On top of that kawapa eneo na amewarihusu wachimbe Hadi kwenye vitalu ambavyo Watu wa mazingira walizuia.

Samia anajua kutafuta hela ndio maana anafaulu usilinganishe na wajamaa unaowatetea ni waharibifu na watumiaji wa vya wengine
 
Bandari, na mbuga za wanyama na watu kuhamishwa makazi kupisha wawekezaji.
Yeye kuamini kwamba waTanzania hawawezi kuleta maendeleo ya nchi yao; bali tuwategemee watu kutoka nje waje kutuletea maendeleo hapa. 'Philosophy' ya kijinga sana hii kuwa nayo kiongozi wa nchi.
 
Wapiga makofi wa samia kama kawaida yenu, tafiti inewaumbua endeleeni kupiga tu makofi lakini ukweli uko wazi
 
Katika yote uliyoyaeleza kuhusu Wilaya ya Chunya na wachimbaji wadogo, karibu yote ni yale aliyoyasimamia Magufuli. Samia hajaongeza chochote cha maana hapo.
 
#noma sana
 
Nchi hii wizi wa kura uko kwenye vinasaba, kama haikutokea kama wasimamizi wa uchaguzi wanavyotaka, wanafuta matokeo kama ilivyowahi kutokea Zanzibar.
 
Semeni tu mumetishwa na wale chawa. watanzania wengi wanajua mipango ya uchumi ya magufuli ilika mizuri kwa namna alivyoleta matokeo haraka kutokana na usimamizi wa mapato ya serikali kwa jinsi alivyodhibiti rushwa uzembe na ufisadi serikalini. Hebu fikiri kiongozi wa nchi unawaambia watumishi wa serikali wale kwa urefu wa kamba zao za malisho unategemea nini hapo.
 
Wamejitekenya afu wakacheka wenyewe, hili jambo la uchawa kwa mama kuna watu kitawapata kitu kujipendekeza. Sssa imagine unashindanishwa na marehemu na anakushinda sijui unajisikiaje kama mtu alie hai.
 
Rais aliyerithi kiti anatakiwa afanye maridhiano na hayati JPM pamoja na wananchi wengi wa kawaida vinginevyo huko anakoelekea itabidi alazimike kuongea lugha yao kwa vyovyote ili akubalike.

JPM policies regarding the country's economic growth were better than the rest of the past and the sitting chair.

Someone sitting on the majesty chair has been mercilessly crucified amid the chanting rogues.

Waandishi wa gazeti hili la mwananchi na citizen si ndio wale walienda hadi Chato kukejeli na kuandika kitabu kumshushia hadhi hayati JPM? This is just a tip of the worst to come before the general elections come 2025.

Wakianzisha poll nyingine ndio watapigwa vibaya zaidi ili aibu iwaangukie na hawatainuka tena
 
Uzuri ni kwamba sisi tumeshika ya awali tu , Awali ni awali na wala hakuna awali mbaya
Hatimaye mwanachadema nae ameamua kusema ukweli wa moyo wake bila kujali chama alichopo πŸ˜‚ safi sana mkuu, ni vyema kutofautisha mambo yako binafsi na za chama ulichopo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…