Mwananchi waomba radhi baada ya wananchi wengi kupiga kura ya kuridhishwa na Sera za Uchumi za Magufuli dhidi ya marais wengine

Mwananchi waomba radhi baada ya wananchi wengi kupiga kura ya kuridhishwa na Sera za Uchumi za Magufuli dhidi ya marais wengine

Huwezi kujisifia unakuza uchumi wakati unashindwa kupigania wananchi wako. Ona eti mchina anafungua supermarket na hiyo unaweka kwenye data kama FDI. Raia wa kigeni wanakuja kufanya kazi ambazo waTZ tunaweza kufanya. Magufuli nakumbuka alitoa limit ya raia wa kigeni kwenye kila kampuni kwa sababu alijua lazima Watanzania tujengewe uwezo na hii linatuwezesha kupata maslahi zaidi na kupunguza uondoshwaji wa pesa za kigeni. Ona sasa dollar inavozidi kupaa.
JPM ameongoza nchi kwa miaka 6, kwahy uzoefu wenu kazini mlitaka kuupata kwenye awamu ya JPM ila awamu za nyuma hamkutaka uzoefu.?
 
Nilijua mapema na nilisema walio hai kushindanishwa na wafu haya mmemvua nguo mtu, waendelee kucheza na jina Mwendazake kwenye ajenda zao watadhalilika sana!
Km una akili, hizo ni chokochoko sasa mama aamue kucheka nao au? Ukishaanza kupigiwa kura na mfu ni zaidi ya udhalilishaji. Hao waliompigia kura wamfuate kuzimu huyo mzimu wao. Ila Rais ajue hakuna uhuru usio na mipaka. Kuna kundi limejipanga piga ua garagaza 2025 wamwaibishe Rais wetu lina watu wakubwa. Nchi yetu siyo ya kufanyia mazoezi, hao wananchi si ni wakenya? Salalee kwanini wasifungashe?
 
Unajua hawa jamaa wanajifanya loyal kwa mamlaka ila ujumbe umeshafika!
Kama ni ngumi basi Msoga gang wamepigwa ngumi ya kisogo maana hata kuiona ilikotokea ni ngumu kwa hiyo ni ngumi isiyo na maandalizi ya kuipokea!
Ndoige
 
Ila tukubali tu ukweli Rais aliyeko madarakani kwa sasa nchi imemshinda. Yaani kwa ufupi tu wahuni wamemzidi kila upande.

Hali ya maisha mtaani imekuwa ni ngumu kupitiliza. Hela haishikiki! Na hata ikitokea ukaishika, inapukutika kirahisi tu ndani ya muda mfupi! Dah!! Halafu kuna watu wanataka atawale mpaka 2030! Sasa si tutapoteana kwa hali hii!

Maana mafisadi wanafurahia tu maisha! Huku wale wananchi wanaopambana kwa njia halali, wakiendelea kutaabika!
Fanya kazi bibie
 
Wao walitegemea majibu ambayo walioulizwa hawakuyaunga mkono, badala ya kukubali matokeo wanakana vitendea kazi vyao kuwa ndiyo vibovu!
Hii ni sawa sawa mtu aulize tende na muwa kipi ni kitamu zaidi halafu ategemee mtu amjibu muwa halafu majibu yanakuja kinyume.
 
Back
Top Bottom