Mwananchi waomba radhi baada ya wananchi wengi kupiga kura ya kuridhishwa na Sera za Uchumi za Magufuli dhidi ya marais wengine

Mwananchi waomba radhi baada ya wananchi wengi kupiga kura ya kuridhishwa na Sera za Uchumi za Magufuli dhidi ya marais wengine

Nyerere alituunganisha kuwa kitu kimoja na kuondoa ubaguzi kati yetu,ila sera zake za uchumi zilirudisha nyuma nchi ndio maana aliondoka madarakani maana sera zake zilifeli.
Ungekua haujaunganishwa kuwa kitu kimoja huo uchumi ungeundelezaje? Kwanza labda kusingukuwepo na hii nchi.
 
Ungekua haujaunganishwa kuwa kitu kimoja huo uchumi ungeundelezaje? Kwanza labda kusingukuwepo na hii nchi.
Ukabilaa ni jambo bayaa sanaa ndo maana wakenya hadi leo kuja sintofahamu...!! Maendelo JPM tunamuhitaji zaidi kuliko rais yeyote..! Alikuwa na mipango mikubwa na utendaji wa watu ulijaaa nidhamu.
 
Weka ushahidi wa haya madai yako ili data ziendani na hoja bila ushahidi unadhihirisha jinsi gani hauna akili.
Ushahidi huu hapa, huyo JPM hamfikii Samia kwa ukusanyaji mapato ingawa hateki, hafungii biashara wala kufoka kwenye makamera.

Compare na data za JPM mwaka wake wa mwisho 2019/2020.
 
Attachments

Magufuli alikuwa Rais na pia alikuwa Amiri Jeshi Mkuu.
Wananchi kufuatilia habari za Tanzania kwenye media halikuwa jambo rahisi au eti kwa upendo tu, bali ilikuwa kwenda kupata tips za Hofu na Tumaini vyote kwa pamoja vinaendelea.
 
Mods rekebisheni kichwa cha habari kianze 'gazeti la mwananchi' na sio mwananchi'.
 
Ukabilaa ni jambo bayaa sanaa ndo maana wakenya hadi leo kuja sintofahamu...!! Maendelo JPM tunamuhitaji zaidi kuliko rais yeyote..! Alikuwa na mipango mikubwa na utendaji wa watu ulijaaa nidhamu.
Mipango ipi? Alikua anaua uchumi, huwezi tengeneza uchumi kwa kuikandamiza sekta binafsi!!
 
2025 Dunia itakuja kushuhudia Jambo zito kuwahi kutokea katika ardhi hii dalili ziko wazi ujumbe umetumwa mapemaa wenye kuelewa wamekwisha elewa.
Hamna lolote mnafanya, mbona mlisema hawezi kuwa mwenyekiti wa CCM ila akazoa kura zote. Huyo Mpina alikua mpiga kelele cha ajabu aliangushwa NEC mkoa na taifa na hakuna kitu mlifanya sukuma gang kumuokoa mwenzenu.
 
Gazeti la mwananchi lilianzisha kura za mtandaoni ama poll ya kuuliza wadau ni sera za kiongozi yupi wa Tanzania kati ya Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia wanazozikubali.

Matokeo ya kura yakaonesha Kikwete kupata 17% sawa na Samia, Mkapa kupata 7% na Magufuli kupata 57%.

Baada ya matokeo hayo kutoka, Mwananchi wameamua kuomba radhi kwamba uchaguzi ama vigezo vilivyotumika havikuwa sahihi wanaomba radhi😂.

View attachment 2973698View attachment 2973699
Mwananchi kumbe bogus.Yaani wameandaa poll,wameandaa vigezo,tena naamini walivipitisha kwa wadau wengine ili wapewe maoni as to their suitability,vikaonekana vinafaa,leo wanatuambia havikuwa sahihi,sikweli vilikuwa sahihi, ila wanaogopa serikali itawa-deal.Anyway kwa Mwenye akili na Samia message sent,viatu vya Magufuli havimtoshi,ajitathmini.

Mwisho niseme hivi,Mwananchi wala hawakuwa na haja ya kuomba radhi,huo ndio ukweli.Asanteni Mwananchi kwa poll,it has confirmed what we already new.
 
Ushahidi huu hapa, huyo JPM hamfikii Samia kwa ukusanyaji mapato ingawa hateki, hafungii biashara wala kufoka kwenye makamera.

Compare na data za JPM mwaka wake wa mwisho 2019/2020.
Makusanyo ya mapato sio kitu cha kulinganisha uongozi kwa sababu vitu kama wingi wa watu vinabadilisha kiwango cha mapato.

Huwezi kusema kwa kua Nyerere alikua anakusanya Milioni 10 kwa mwezi kwa mfano huku ana watu milioni 6 alikua anafanya vibaya kulinganisha na Samia anaekusanya Trilioni 2 kwa mwezi ana watu Milioni 65.

Unalinganisha makusanyo ya mapato kama tu vitu kama population, economic development or activities, nk viko sawa kwenye tawala zote.

Linganisha vitu visivyobadilika mfano miundombinu, huduma za kijamii nk.
 
Hamna lolote mnafanya, mbona mlisema hawezi kuwa mwenyekiti wa CCM ila akazoa kura zote. Huyo Mpina alikua mpiga kelele cha ajabu aliangushwa NEC mkoa na taifa na hakuna kitu mlifanya sukuma gang kumuokoa mwenzenu.
Tafadhali tujikite kwenye hoja kwa bahati mbaya mi sipo katika makundi uyawazayo sababu ndio yametufikisha hapa Kama Taifa hapa tunajadili polls za the citizen newspaper
 
Gazeti la mwananchi lilianzisha kura za mtandaoni ama poll ya kuuliza wadau ni sera za kiongozi yupi wa Tanzania kati ya Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia wanazozikubali.

Matokeo ya kura yakaonesha Kikwete kupata 17% sawa na Samia, Mkapa kupata 7% na Magufuli kupata 57%.

Baada ya matokeo hayo kutoka, Mwananchi wameamua kuomba radhi kwamba uchaguzi ama vigezo vilivyotumika havikuwa sahihi wanaomba radhi😂.

View attachment 2973698View attachment 2973699
Sera za Uchumi za MaRais? Yaani kila Rais wa Tanzania ana sera zake za uchumi?

Mwananchi waliuliza swali ambalo halina maana kabisa. Tanzania imetawaliwa na chama kimoja tu cha siasa tangu tupate uhuru: TANU/CCM. Tangu 1995 tuna mfumo wa vyama vingi vya siasa. Sera za Uchumi huandaliwa na serikali ya chama tawala na kupitishwa na bunge ambalo siku zote limekuwa na wabunge wengi wa hicho chama tawala: CCM.

Sasa kama Mwananchi wanaona kuwa kila Rais wa Tanzania ana sera zake za uchumi na Watanzania wanaamini hivyo basi kiwango cha ujinga nchini (literacy level) kimeshakuwa kikubwa sana. Itakuwa inamaanisha kwamba hatujui kabisa maana ya sera za uchumi (economic policies). LABDA kama kinachotafutwa ni UTENDAJI wa Rais lakini sio "sera zake".

Kubwa zaidi, kwanza hilo ni swali gumu sana kwa watanzania wengi ambao huelewa "itikadi" ni chama cha siasa, "sera" ni miradi ya ujenzi wa miundombinu na ununuzi wa mitambo, vifaa na vitendea kazi mbalimbali! Pili, hawana uwezo wa kuelewa serikali inavyoweza kucheza na "microeconomic tools" kupunguza mfumuko wa bei, kuongeza ajira, uwekezaji, kuboresha upatikanaji wa huduma za jamii, kuboresha utendaji wa sekta ya umma kwa ujumla, kuimarisha thamani ya sarafu, na mambo kama hayo. Hata mambo muhimu kama "value for money" kwenye miradi/manunuzi hawayajui wala kuyajali. Mbaya zaidi wametawaliwa na ushabiki uliokithiri wa viongozi na vyama vya siasa. Kila kitu wanaona kiko katika rangi "nyeusi" au "nyeupe" tu. Hawana uwezo wa kuelewa "kijivu" zenye mikolezo mbalimbali.

Hii poll haikuwa na maana yoyote kwa umma wa Watanzania labda kama Mwananchi walikuwa wanataka kujua Rais wa Tanzania mwenye washabiki wengi hivi sasa - jambo ambalo halina afya njema kwao. Labda ndio maana wamelazimika kuiondoa na kuomba radhi.
 
My opinion ,
  • Tariff ambazo January Makamba aliziongeza kwenye uunganishaji umeme zirudishwe kama awali.
  • Halmashauri za Miji zirudishe vitambulisho vya machinga lakini wawe stricted kwenye maeneo yao, na umachinga wao uwe na mipaka, mfano, wanauza only used items.
  • importer wa bidhaa mbali mbali wawe wanafuatiliwa kwa ukaribu ili kuhakikisha bidhaa hizo, aidha zinauzwa in wholesale only, aidha muhusika anakuwa na duka kwa ajili ya bidhaa zake, na si kuzimwaga directly kwenye meza za kariakoo!
Angalau umetoa wazo. Issue ya opinion ingefaa iwasaidie kuboresha sera na si kuukana utafiti
 
Back
Top Bottom