DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Nikimkabidhi Mwanangu shule yoyote ile huwa nakaa kikao na waalimu cha dk 2-5 hivi.. sio kama nawatisha huwa nawaambia mapema kuwa nimeleta MTOTO na sio PUNDA.. mwenye sikio asikie..

Huyoooo naondoka mikono nyuma napiga mruzi....!
 
Hakuna mwalimu anayeweza kumpiga mtoto ngumi tena mtoto wa darasa la kwanza, huyo mtoto labda alipigana na wenzake au alipata ajali, uchunguzi wa kina ufanyike. Kuchelewa namba hakuwezi kumfanya mwalim ampigie mtoto ngumi ya tumboni.

Nimulize kitu hapa.

Siku hiyo adhabu ilipotekelezwa na huyo mwalimu kwa marehemu je ni wanafunzi wangapi walikuwa wamechelewa namba?

Hiyo ngumi alipigwa huyo marehem tu au walipigwa wanafunzi zaid ya huyo marehemu?

Hiyo adhabu ilitolewa katika mazingira gani? ili ushahidi uwe wa kina zaidi

Zaidi ya yote niseme kwamba, poleni sana wazaz, ndugu, jamaa na wote tulioguswa na msiba huu. Mungu amrehemu marehemu! Amina.
 
Shida ya MADAKTARI MAKANJANJA, unaona kabisa mtoto ameshambiliwa mwili mpaka amedhurika, lakini unaandika CANCER kwenye ripoti! 🤓

Is cancer the cause or a co-existing condition? (which is not a causation).

Mtu akiwa na malaria mwilini, kisha akakakatwa panga akafa, utasema amekufa kwa malaria?

Hizi shule zinazofundisha hawa MAKANJANJA zimesajiliwa kweli kihalali au zinafundishaje?

Hawa ndio wanaotushindilia MACHANJO YENYE MERCURY kutoka Marekani.

Cc Lamomy & DR Mambo Jambo
 
Daaah pole sana ndugu.
 
Naona Waziri kaamua kuuchuna....lingekuwa suala la uchawa ungemuona kaja mbio mbio..ndio naana huwa nawadharau sana watu wa namna hii..
Kulingana na hii taarifa kwa nini Waziri kamrudisha muhusika twice?...kosa kubwa sana...very irresponsible...
Mungu anisaidie sana jambo kama hili lisijetokea maishani mwangu kwani consequences zitakuwa mbaya sana kwa pande zote zinazohusika..
 
Kama ripoti ya Daktari inaonesha mwanao alikuwa na Kansa ya Damu ( dalili zote unazoelezea zinaendana) kwanini unalazimisha ionekane Mwalimu ndio kamuua mwanao?

Kuchapwa viboko kungekuwa kunaua tungeshakufa wengi sana tuliosoma zamani. Mnataka kutengeneza kizazi gani cha watoto wasiochapwa?

Kwanini mnataka kuleta malezi ya Kizungu watoto wa Kitanzania wenye mazingira na tamaduni tofauti katika malezi na makuzi?

All in all may His Soul Rest in Eternal Peace. Amen. Kuendeleza hii kesi ni kumkosea Marehemu kwa kulazimisha kitu kisichokuwepo.
 
Kumpiga tu mtoto wa darasa la Kwanza bila ruhusa rasmi ya Mwalimu Mkuu ni kosa kitaratibu za ufundishaji.

Mwalimu Mkuu pekee ndiye anayeruhusu Mwanafunzi achapwe viboko na ni lazima aandike aina ya kosa na idadi ya viboko isiyopungua viboko vitatu na sehemu ya mwili ya kuchapwa katika daftari la adhabu na kusaini.

Kisaikolojia ya ufundishaji, mtoto wa darasa la Kwanza hastahili kuchapwa viboko.
Anastahili kukaribishwa shuleni na kushawishiwa kuipenda shule na masomo husika, na kusikilizwa kama amekosea ili kumfundisha taratibu za shule.

Kama ilithibitika mtoto alichapwa na haikundikwa kwenye daftari la adhabu la Mwalimu Mkuu na saini yake ya ruhusa.

Utawala wa shule na Mwalimu mtoa adhabu wanapaswa kuwajibika.
Kwakuwa ulikuwa ni ugomvi binafsi wa Mwalimu dhidi mtoto na sio adhabu ya kikanuni.
 
Ni rahisi kusema hivi kwa kuwa lililotokea si lako.
 
Ukimpiga mgonjwa na akafa, wewe ndio muuaji.
Umesababisha afe kabla ya muda wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…