DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Dah pole sana ila kwanini tangu mwanzo hukwenda polisi? hata kama polisi hawana msaada ila ni muhimu kutoa taarifa, pia wakati mwanao amelazwa ungepaswa kufanya kama hivi ulivyofanya sasa, Pole sana naamini utapata haki yako na hiyo shule watachukuliwa hatua,. HUU NI UPUUZI WA HALI YA JUU, Kila siku tunakemea mambo ya kuchapana hovyo, wafukuzwe wote kuanzia mwalimu mkuu na ulipwe.
watu mmeweka akili kwenye viboko tu , je report ya dakari mmeipuuzia kbs ? tusiishi kama viumbe mwituni
TUPENDE KUPIMA AFYA ZETU MPO WENGI HUMU MNATEMBEA NA MAGONJWA SUGU NA HAMJUI , SIKU UNASUKUMWA UNAMUACHIA KESI MTU

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
 
na report ya daktar inasemaje ? jaman mtu anaeza kufa popote , angalia report ya daktari inasemaj , ni kwel walimu wamezidisha adhabu lkn kwa attitide hii tunawapa nguvu watoto dhidi ya walimu wetu , kikubwa UTARATIBU WA VIPIMO VYA AFYA KILA MARA VIWE VINAFANYIKA , NAKUMBUKA NLIWAI OUTREACH ZA AFYA CHECK UP , NLIFIKA SHULE MOJA NKAKUTA WATOTO 5 WENYE MATATIZO YA MOYO NA WAZAZI WAO HAWAJUI

TUPENDE KUPIMA AFYA ZETU SIO MPK TUSUBIR MAGONJWA

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
Kwani lazima uwapige? Mbona private hakuna huu ushenzi wa kuwapiga watoto na bado shule zao zinaongoza kufanya vizuri...??

Yaani unapishana asubuhi na makundi ya watoto wa shule za serikali wamebeba fimbo tatu tatu za mianzi wakielekea shuleni. Je ni haki?
 
Naitwa Janeth Shayo, mkazi wa Uru, Moshi. Naomba unisaidie kupaza sauti mwanangu Jonathan Makanyaga (07) mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mrupanga, ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inataka kupindishwa.

Tar.28/02/2024 mwanangu alienda shuleni akiwa mzima. Alipofika aliadhibiwa kwa kuchelewa "namba". Alipoingia darasani alianza kutokwa damu puani na mdomoni. Akarudishwa nyumbani. Nilipomkagua nikamkuta na majeraha yaliyovilia damu mgongoni, kwenye mbavu na mguuni.

Kesho yake nikaenda nae shuleni kutaka kuoneshwa mwalimu aliyemfanyia ukatili mwanangu. Lakini Mwalimu mkuu akaomba nibaki nje. Akaingia na mwanangu ofisi ya walimu na kumtaka amtambue Mwalimu aliyemuadhibu. Mwanangu akamtanbua. Mwalimu Mkuu akaniambia wameshamfahamu ni mwalimu wa "Field" hivyo atazungumza nae.

Wakanipa 20,000/= za matibabu. Nikampeleka mwanangu zahanati. Kesho yake akazidi kutoka damu, na kulalamikia maumivu sehemu za mbavu. Nikampeleka hospitali ya masista. Daktari akaniambia bandama imejeruhika ndio sababu ya kutoka damu mdomoni. Mtoto alidai pamoja na viboko alivyochapwa, Mwalimu pia alimpiga ngumi tumboni. Huenda ndiyo iliyopasua bandama.

Hali yake ilizidi kuwa mbaya tukapewa rufaa kwenda KCMC. Akatakiwa kufanyiwa upasuaji. Gharama 350,000/= lakini sikuwa nayo. Nikapiga simu shuleni wakasema tuombe afanyiwe halafu watalipa baadae. Hata hivyo kabla hajafanyiwa hali yake ikazidi kuzorota, akashindwa kupumua, akawekwa kwenye Oxygen. Akashindwa kula, akawekewa mpira wa chakula. Baada ya siku chache akafariki 😭.

Lakini ripoti ya hospitali inasema mwanangu amekufa kwa kansa ya damu. Kansa gani ya damu inayomuua mtoto kwa wiki mbili? Na kwanini hiyo kansa itokee baada ya kuadhibiwa shuleni? Kwanini Mwalimu aliyemuadhibu mwanangu anafichwa, na sipewi haki ya kumfahamu?

Nalazimishwa nichukue maiti nikazike lakini nimekataa. Nataka uchunguzi huru. Nimeenda dawati la jinsia kulalamika nikapuuzwa. Nimepiga simu kwa Waziri Dkt. Gwajima D akanipa namba ya mtu wa kunisaidia. Nilipopiga kumbe ni yuleyule Mkuu wa dawati la jinsia aliyenipuuza. Nikamrudia Gwajima akasema niwasiliane nae huyohuyo. Nimekosa pa kulilia haki ya mwanangu Jonathan
Dkt. Gwajima D
Unaitwa huku utoe neno
 
na report ya daktar inasemaje ? jaman mtu anaeza kufa popote , angalia report ya daktari inasemaj , ni kwel walimu wamezidisha adhabu lkn kwa attitide hii tunawapa nguvu watoto dhidi ya walimu wetu , kikubwa UTARATIBU WA VIPIMO VYA AFYA KILA MARA VIWE VINAFANYIKA , NAKUMBUKA NLIWAI OUTREACH ZA AFYA CHECK UP , NLIFIKA SHULE MOJA NKAKUTA WATOTO 5 WENYE MATATIZO YA MOYO NA WAZAZI WAO HAWAJUI

TUPENDE KUPIMA AFYA ZETU SIO MPK TUSUBIR MAGONJWA

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
Ripoti ya daktari inahusiana nini na mwalimu kujieleza kilichotokea? Unajua mnaweza saidia kumlinda mtu anayefanya ukatili kwa watoto?

Kwanini afichwe bila kuhojiwa?

Si mwalimu anajieleza, ni kweli alimchapa ila si kwa kiwango hatarishi, hakumpiga ngumi. Hayo majeraha kama yapo hayatokani na kipigo chake. Maelezo yanayojitosheleza kwa huyo mzazi. Unadhani angepewa hayo maelezo na dr akamueleza kuwa kuna kansa angefika huku kote?

Amefika huku kwa sababu kuna jambo linafichwa fichwa, hata huyo mwalimu anayedaiwa kumpiga hajulikani. Wewe angekuwa mwanao ungeona sawa?
 
pole sana asee , lkn usiwekeze akili kwa mwl tu , watz hatupend kupima afya zetu , mwl hata awe mkorofi vp haez mpiga ngumi mtoto wa drs la 1 , kwa maelezo yako umeelezea rufaa tatu hapo , ni ngumu kwa rufaa hizi tatu mwl mkuu wa shule ya msingi kujitoa kumlinda huyo mwl wa field , Ziamini report za madaktari , mtoto anauma ila mwisho wa siku kubali tu lkn hii iwe fundisho kwa walimu pia EPUKA KUPIGA MTOTO WA MTOTO ANAEZA KUWA MAREHEMU ANAYETEMBEA HLF MZIGO UKAKUANGUKIA , MIMI NI DAKTARI NA NMEONA WATU WENGI WANAOAMINI WAZIMA KUMBE WANATEMBEA NA MAGONJWA SUGU

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
Jaribu kuvaa kiatu cha mhusika, mambo haya yanafikirisha:;

1: Mhusika wa hilo tukio kufichwa asijulikane na mama wa mtoto, inaonyesha dhahiri hawana utu kuanzia uongozi wa shule

2: Anayetakiwa kumwadhibu mtoto ni mkuu wa shule kulingana na sheria walizowekewa, hapa mkuu wa shule ni namba 2 kwenye hii ishu baada ya aliyetenda hili tukio

3: Ripoti ya daktari nayo ina namna ya rushwa, ufanyike uchunguzi mwingine na madaktari wenye utu

Likimshinda waziri mkuu wa nchi anapitapita huku pia atasaidia familia hii haki kupatikana
 
Mama yangu Mhe Dkt Mwijuma
Ninapenda kukushauri uliangalie hili jambo kwa jicho pevu.

Kilio cha mama kimetugusa wengi. Inaamsha hisia
report ya daktari umeiona ?huyu mama anabishana na report ya madaktari , km mtoto bado hajazikw basi wampeleke hospitali yoyote wathibitishe kama kwel ni kansa ya damu au bandama iliharibiwa , TUSIPENDE KUWAJAJI WALIMU WOTE SAWA , SIO KWEL , MUDA MWINGINE TUNAWAPELEKEA WALIMU WATOTO AMBAO AFYA ZAO NI TIA MAJI TIA MAJI , MWL HAWEZ MWAZIBU MTOTO WA DRS LA 1 KWA KUMPIGA NGUMI , WAZAZI WENGI WAONGO SANA

MWAKA kadhaa nyuma nlikuwa mwl nlimchapa mtoto kisha mtoto aliondoka shule vzr tu na hakwenda nyumban kisha akaenda kuchuma maembe yeye na ndugu zake wa karibu akaanguka kutoka juu hadi chini kisha akaenda kwao akatunga uongo kuwa alichapigwa teke na mwl ambae ni mimi , ila uzuri siku anaanguka alikwepo mzazi tunajuana na siku mtoto anakuja na mzaz wake kuniamshia moto , hii siku ilikuwa siku ya kikao cha wazaz , basi kesi ilikuwa ofisi ya mwl mkuu sikuongea lolote maana nlijuwa kuna namna yule mtoto anafeki taarifa , katikati ya maongez yule mzaz alifuata kiti ofisin akakuta mabishano ya mwl mkuu na mzazi basi akahoji, alipohadithiwa akasema alimwona kaanguka kutoka mtini na alisema atamsingizi mwl ambae ni mimi

TUSIPENDE KUWAAMINI WATOTO MUDA MWINGINE WANADANGANYA KUOGOPA KUFOKEWA NA WAZAZ

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
 
Ripoti ya daktari inahusiana nini na mwalimu kujieleza kilichotokea? Unajua mnaweza saidia kumlinda mtu anayefanya ukatili kwa watoto?

Kwanini afichwe bila kuhojiwa?

Si mwalimu anajieleza, ni kweli alimchapa ila si kwa kiwango hatarishi, hakumpiga ngumi. Hayo majeraha kama yapo hayatokani na kipigo chake. Maelezo yanayojitosheleza kwa huyo mzazi. Unadhani angepewa hayo maelezo na dr akamueleza kuwa kuna kansa angefika huku kote?

Amefika huku kwa sababu kuna jambo linafichwa fichwa, hata huyo mwalimu anayedaiwa kumpiga hajulikani. Wewe angekuwa mwanao ungeona sawa?
Mkuu umeeleza kila jambo hawa wanadhani sisi wajinga! Halafu wakamdanganya na elfu ishirini hahahaha
 
Kuna haja ya kusikiliza upande wa pili sidhani kama alio ya andika yote yako accurate, ila pole sana kifo cha mtoto wako kisikie kwa mgine tu kinauma sanaa, .......ila hi stori is not adding up, post mortem report ndo final official report inao pelekwa hata mahakamani kuja kui-challange sio jambo raisi.
 
report ya daktari umeiona ?huyu mama anabishana na report ya madaktari , km mtoto bado hajazikw basi wampeleke hospitali yoyote wathibitishe kama kwel ni kansa ya damu au bandama iliharibiwa , TUSIPENDE KUWAJAJI WALIMU WOTE SAWA , SIO KWEL , MUDA MWINGINE TUNAWAPELEKEA WALIMU WATOTO AMBAO AFYA ZAO NI TIA MAJI TIA MAJI , MWL HAWEZ MWAZIBU MTOTO WA DRS LA 1 KWA KUMPIGA NGUMI , WAZAZI WENGI WAONGO SANA

MWAKA kadhaa nyuma nlikuwa mwl nlimchapa mtoto kisha mtoto aliondoka shule vzr tu na hakwenda nyumban kisha akaenda kuchuma maembe yeye na ndugu zake wa karibu akaanguka kutoka juu hadi chini kisha akaenda kwao akatunga uongo kuwa alichapigwa teke na mwl ambae ni mimi , ila uzuri siku anaanguka alikwepo mzazi tunajuana na siku mtoto anakuja na mzaz wake kuniamshia moto , hii siku ilikuwa siku ya kikao cha wazaz , basi kesi ilikuwa ofisi ya mwl mkuu sikuongea lolote maana nlijuwa kuna namna yule mtoto anafeki taarifa , katikati ya maongez yule mzaz alifuata kiti ofisin akakuta mabishano ya mwl mkuu na mzazi basi akahoji, alipohadithiwa akasema alimwona kaanguka kutoka mtini na alisema atamsingizi mwl ambae ni mimi

TUSIPENDE KUWAAMINI WATOTO MUDA MWINGINE WANADANGANYA KUOGOPA KUFOKEWA NA WAZAZ

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
Mbona wewe hukufichwa? Hoja hapa ni mtuhumiwa ni nani? Kwanini mwalimu mkuu kamficha kabla hata mtoto hajafa maana alimpa na pesa ya matibabu akamtibu mtoto na kumuomba kuwa ataongea na mhusika.
 
Mbona wewe hukufichwa? Hoja hapa ni mtuhumiwa ni nani? Kwanini mwalimu mkuu kamficha kabla hata mtoto hajafa maana alimpa na pesa ya matibabu akamtibu mtoto na kumuomba kuwa ataongea na mhusika.
Unajua kosa ni kwamba watoto wengi huletwa mashuleni bila kufanyiwa thorough medical check up kwa chronical disease, sidhani kama mualimu anaweza kupiga ngumi ya tumboni mtototo wa miaka 7.
 
Back
Top Bottom