Mwanangu ana Sickle Cell, tiba yake nini?

Mwanangu ana Sickle Cell, tiba yake nini?

Asante mkuu, umetaja dalili zote vyema kinachonishangaza mama yake na mimi hatuna historia ya kiukoo kuwako kwa ugonjwa huu. Kwa sababu yeye ndiye aliyempeleka hospitali nikamuuliza mbona wote kwetu haupo akasema eti sisi ni carrier.

Mbaya zaidi sijaviona vipimo kwa macho, hata nikimdai document za majibu anadai hakupewa.

Mpaka napata mashaka. Ila dalili ni hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
Muulize vizuri mke wako, pengine anakuficha au mtoto sio wako. No in between
 
Kama kwao na kwenu hakuna huo ugonjwa, umepigwa
 
Wakuu Salaam,

Niende moja kwa moja kwenye mada, nina binti yangu wa miaka minne. Hivi majuzi amebainika kuwa na sickle cell kusema kweli nimechanganyikiwa sababu nasikia ni ugonjwa usio na tiba.

Naomba kujua yafuatayo;
1. Ni kweli ugonjwa huu hauna tiba?
2. Kama si kweli, tiba yake ni ipi?
3. Kama hauna tiba nini hatima yake?

Nimenyongea kwa kweli[emoji27]

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu Panzi Mbishi kwanza tambua kuwa jina lako linaashiria nguvu,fuata ushauri wa kitabibu,usikubali kupotezwa na wanaoamini njia zisizo za tiba ya kisayansi,wapo baadhi wanakuwa na hali hiyo katika umri mdogo,ila wanapovuka umri huo wanakuwa sawa,japo wakati mwingine kuna gharama za kupata huduma za tiba hadi kuvuka umri wa utoto.
 
Asante mkuu, umetaja dalili zote vyema kinachonishangaza mama yake na mimi hatuna historia ya kiukoo kuwako kwa ugonjwa huu. Kwa sababu yeye ndiye aliyempeleka hospitali nikamuuliza mbona wote kwetu haupo akasema eti sisi ni carrier.

Mbaya zaidi sijaviona vipimo kwa macho, hata nikimdai document za majibu anadai hakupewa.

Mpaka napata mashaka. Ila dalili ni hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini usimpeleke kumpima wewe ujiridhishe kama anao?
Pole sana kwa mitihani mkuu
Mungu ampe afya na nyie muwe na subra
 
Relax

magonjwa mengi sana yaliyokuwa tishio miaka ya nyuma sasa hivi si tishio tena kwny Ulimwengu wetu kutokana na maendeleo kwny Technolojia na maendeleo ya tiba

Hata sisi wa zamani kidogo tuliopita shule shule na kupata ofisi za kuzugia miaka ya 1980s kendra 1990s tunepoteza marafiki na wafanyakazi wenzetu wengi kutokana na maradhi mengi ambayo leo yana ama Tiba au njia nyingine mfano Ukimwi

fuata maelekezo ya Wataalam na kujua namna ya kuishi na hilo tatizo,

Leonel Messi kama kumbukumbu zangu zipo sawa niliwahi kusikia alikuwa na tatizo hilo utotoni
Ndio nasikia hata naibu waziri yule wa rubudani Nae walewale
 
Pole kuna ndugu ana ugonjwa huo ni ugonjwa wa kurithi wazazi huwa ni carrier wa vinassba vya ugonjwa,cha kuzingatia hakikisheni anahudhuria clinik za wagonjwa wa sikocell,matibabu yameboresha atakua na atatimiza ndoto cha msingi muwe karibu naye muepusheni na baridi kali ama joto kali pia wanashauriwa wanywe maji mengi ili damu iwe nyepesi kuepusha maumivu yatokanayo na damu kukwama kwenye vishipa vidogo.

All the best.
 
Pima DNA huyo mtoto
mtoto siyo wako, mbane mke atoe majibu
Umenena jambo

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakazia [emoji3578]
Muulize vizuri mke wako, pengine anakuficha au mtoto sio wako. No in between
Kukua ni pamoja na kumuambia mtu ukweli
Pimeni DNA
Kwao na kwenu hakuna historia ya huo ugonjwa lakini mwanao anao!!!

Mkuu pole, sitaki kuwaza nje ya hii maada muhimu fuata ushauri/maelekezo ya wataalamu wa afya.

Mungu yupo atamsaidia.
Hili ni jambo sahihi kwa wakati usio sahihi!! Mama na mtoto obviously watahisi uko na unyanyapaaa!! Tumia hekima na busara katika wakati huu!!
 
Back
Top Bottom