Mwanangu anaogopa sana wafu

Mwanangu anaogopa sana wafu

Nikiwa mdogo nilikuwa nikisikia msiba mahali hasa kijijini usiku mzima silali yaani,mawazo kibao na kuogopa ilifika kipindi ikaisha
 
Inaonesha mwanao amekuzidi imani na upeo wa akili.

1) Amekuzidi imani kwasababu hakuna kiumbe kisichoogopa kifo na wafu. Hata mitume iliogopa kifo sambamba na kuogopa wafu na madhambi yao walioyatanguliza mbele kwa muumba wao.

Na mtu akifa, kitabu chake cha hesabu cha maombi yake binafsi hufungwa rasmi, kwamba hawezi kujiombea hata msamaha kwa muumba wake (Isipokua sadaka/maombi ya kuendelea alizoacha au anazofanyiwa, na dhambi za kuendelea alizoacha - mfano Kama aliacha danguro basi kila dhambi zinazotendeka humo ana asilimia zake huko anakoenda n.k).

2) Amekuzidi upeo wa akili kwasababu mtu mwenye akili ya kawaida wafu ni kitu kisicho ogopeka na kisichokua na madhara. Ila hakika, kwa mtu mwenye upeo mkubwa wa akili mfu ni kitu cha kuogopwa sana kwasababu huwa kinaambatana na mambo mengi tusioyaona kwa macho ya kawaida. Na pia watu wabaya hutumia wafu au vitu vilivyotumika kumuandaa mfu kufanyia mambo mabaya sana, kama vile uchawi na ulozi.

Huyo mtoto ni mwema, mpende na mlinde sana.
Dead body knows nothing
 
Back
Top Bottom