Mwanangu anashindwa kutumia common sense?? Hii ni shida gani?

Okay, sikufundishi kazi au malezi ila ebu jaribu kumuachia mama iyo kazi kwa miezi kadhaa.

Wewe uwe unapata info kupitia kwa mama yaan mama ndio afanye the rest. Wanasema mama na mtoto wa kiume na baba na mtoto wa kike.
 
Kabla ya kusema hayupo smart tuanzie hapa kwanza.

Yupo logically - ana uwezo wa Ku-reason mambo , mfano unaweza mwambie aende sehemu Ila yeye akakataa kwa kukupa sababu zenye mashiko na ukamkubalia?

Angalia kuhusu temperament (silika) mtoto wako ni introvert au extrovert

Kuna utofauti wa kuwa mkimya na kupendelea kukaa kimya hivyo angalia haiba yake .

MTU mkimya huwa Ana monology na MTU ambaye upendelea kukaa kimya hana monology.

Ikiwa mtoto wako ni intovert MTU mkimya basi smartest yake haiwezi kusomeka haraka kupitia kuongea bali kupitia matendo na kuandika.


Tufanye nini ili kijana awe smart.

Ikiwa temperament (silika) yake ni introvert basi muwekee mazingira ya kumjenga .

Anza na kumpa wisdoms words -maneno ya hekima.

Mjenge kakili na kihisia

Mtafutie vitabu vyenye personal growth

Anza kutambua strength zone yake. Ikiwa anapenda jambo Fulani mfano labda anapenda udaktari anza kumuwekea mazingira ya yeye kuwa daktari.

Msikilize na ukiona anazubaa jaribu kumuwekea mazingira ambayo yatamfanya kuwa comfortable , Quit place.

Nb kuwa smart huwa nimatokeo ya kuwa tabia ya kujifunza kila siku.

Na wewe Kama mzazi usimuhukumu mtoto kuwa sio smart Ila anza na kumjenga kupitia hayo mambo.

NB TV Kama Unayo haifai Sana waweza kumpuguzia muda wa kutazama TV na asome vitabu huku ukimpa motivation .
 
Kazi ni mvuvu sasa sijuagi ana talent gan??
uvivu inaweza kua talent

Majibu yako yote yanaegemea kumuhukumu na kuwa negative kwake.

Hapo tu umeshajijengea picha yako kichwani na huo ndio ukuta unakutenganisha wewe na mwanao

Huwezi kujiuliza mtu anapenda nini au yupo vizuri kwenye nini kama wewe hujawahi muuliza au kukaa nae kwa karibu kujua

Kama kila muda unamuhukumu kiasi cha kujikariri kama mjinga, vipi kama anapenda ubunifu, je atakuwa na ujasiri wa kukuambia anachokipenda bila kusubiria judgement yako

Vipi kama kutokana na kuonekana failure, tayari ana low self esteem kiasi cha kujichukulia kama failure, hiki ni kitu kibaya sasa umejiandaaje kama mzazi kumsaidia

Utamuacha mtoto wako ateketeee au utasimama kiume kumjua na kumpambania maana 17 sio mkubwa sana na hata exposure ya maisha hana. Hivyo, wewe una nafasi ya kucheza hapo

Nilivyokusoma unaonekana ni mzazi flani traditional na unaamini sana katika shule kutokana na historia yako.


Ila itabidi ukubali umuone mwanao kama alivyo na sio lazma awe reflection ya enzi zako.. That's the only way utaweza kumuelewa, kumthamini, kumpambania na kumjengea ujasiri...

Mfano akirudi likizo, tafuta course ambazo zipo skilled based, iwe computer, graphics, videography etc then mpe option ya kuchagua anachokitaka..

Ukifanya hivyo taratibu utaona sehemu nyingine ya uwezo wake mkuu, usimuhukumu, muelewe na umkubali alivyo maana ni wako
 
mkuu naona uko well Educated kwene mambo za temperament
nieleweshe monology??

huyu kwa ninavomsoma ni introvert lakin sasa ndo nashangaa introvert huwa na akili nyingi tofauti ni kwake.
 
slow learners wapo, ni kwenda nae taratibu tu na kujaribu kumshughulisha na shughuli nyingi za kufanya, then make sure you demand and ask feedback on each task umempatia ata changamka tu 🐒
 
Mamaake vipi? Umeme kichwani ni mkubwa au mdogo?

Mtoto si wa kwako pekeyako.

Ukiachana na kurithi akili, kuna sababu kedekede za binadamu kuwa slow au average, sinazochagizwa na experience wakati wa makuzi hasa katika umri wa miaka 0-3, 3-12.
 
Muulize mama yake kipindi anazaliwa huyo mtoto alilia baada ya muda gani?

Alizaliwa kwa njia ya kawaida ?



DR Mambo Jambo
 
mkuu nimekuelewa!
yes ana low self esteem
Ni mwoga wa maumivu fimbo nk si kwangu generally tu.

Nimekua nikijaribu kumpa councelling
hasa ya kujiamini,,,kutokua muoga nk.

Shida ni moja mi likija swala la shule siwezi kabisa kua mvumilivu hasa mtu akirudi hamna alichoelewa. au msahaulifu wa simple concepts ambazo mwanzo alikua anaweza.

Nadhan labda mm kwasababu shule haijawai kunisumbua ndo maana siwezi muelewa mtu anaeshindwa vitu vidogo vidogo
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…