Mwanangu wa darasa la pili hili swali kakosaje? Au mwalimu ndiye hajielewi?

Kakosa hilo.

Mwambie mwanao kuwa refa pia ni neno la kiswahili hutumika
 

Mwamuzi wa mpira anaitwa Nani?
 
Mtoto hafundishwi kama mtu mzima,mtoto anafundishwa kitotototo kuendana na mazingira yanayomzunguka huko mbele sasa ndo ataanza kujishepu mwenyewe kadri anavyopanda darsa..mfano,sisi tulipokuwa darsa la pili tulifundishwa (2-3=haiwezekani),na tukaamini hivyo hadi tulivyopanda darsa tukajua (2-3=-1) ..mtoto hufundishwa kwa staili ya kipekee sana
 
Waamuzi wa mpira wapo zaidi ya mmoja uwanjani,kwa ligi yetu wapo 4,,kwa ligi kubwa za ulaya baadhi ya mechi wapo 5.


Mwamuzi anayezungumziwa hapa ni mwamuzi wa kati,yaani REFARII. Hivyo swali lilipaswa kuwa:
Mwamuzi wa kati wa mpira wa miguu huitwa.............
Watoto wa sasa wanaweza wakasema VAR...maana nayo pia hutoa maamuzi[emoji848][emoji848]
 
Huu muandiko mbona kama wa mtu wa sekondari?!!
 
Unajua mfundishaji wa watoto shuleni ni mfundishaji ndio lakini jina specific analoitwa ni mwalimu. Sasa ukijibu mfundishaji haujakosea Sana ila sio sahihi kwa 100%.

Ni sawa na ukamuita mtu mlimaji badala ya mkulima, au muendeshaji badala ya dereva.

Huyu mtoto hajakosa hilo swali kapata 100% swali limeulizwa kwa kiswahili lijibiwe kwa kiswahili hakuna namna
 

Mtoto ana akili sana mzee swali la kiswahili lijibiwe kwa kiswahili, referee sio kiswahili sijui umeelewa angeandika referee angekosea pakubwa kwanini ajibu swali la kiswahili kwa kingereza ?
 
Nafikiria dogo kwelie janja mingi ila ili jibu liwe refarii, hapa watu wa kiswahili inabidi waconfirm kama hilo neno limetoholewa rasm kwenye lugha yetu, vinginevyo tafsiri ya referee ni mwamuzi, dogo kapatia.
 
Refarii ndiyo jibu sahihi kwa mujibu wa kingozi cha mwalimu (marking scheme).

Mwamzi ni jina jumuishi sana mfano mwamzi mahakamani anaitwa Hakimu/Jaji.
Refarii ni kiswahili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…