Mwanangu wa darasa la pili hili swali kakosaje? Au mwalimu ndiye hajielewi?

Mwanangu wa darasa la pili hili swali kakosaje? Au mwalimu ndiye hajielewi?

Shule za msingi zinafungwa Leo, Niko hapa napitia mitihani na ripoti za wanangu!

Kuna swali hili; Mwamuzi wa mchezo wa mpira wa miguu anaitwa nani? Mwanangu kajibu MWAMUZI kakosa, eti mwalimu kawaambia jibu sahihi ni REFARII.

Je, jibu sahihi ni lipi hapo? Kosa ni la mtoto au mwalimu ndo hajielewi?

View attachment 1807716
View attachment 1807714
Such a good hand writing!! Ananikumbusha enzi zangu. So neat!!
 
Lakini mbona swali la tisa kama vile mwalimu kachemsha pia kwa hio ngoma droo
 
Sijui niandike vipi, ila nahisi swali lenyewe kama kakosea kulitengeneza hivi.

Any way, ni udhaifu mdogo tuu mkuu wala usijali, hayo ni mambo ya kawaida + kibinaadamu.usipaniki

Ila mtoto wako genious asee[emoji2], hadi hati ya mwandiko inaonyesha. Kongole sana
Ndo hivo nakomaa nao wapo KAYUMBA! Sina mpango wa private schools hata kidogo! Kila siku tunasoma
 
Huu muandiko mbona kama wa mtu wa sekondari?!!
Hapana: ni mtoto yupo kayumba, sema namzingatia kufuatilia madaftali kila siku, tunafundishana jioni! NAIMANI TUTATOBOA TU KIBISHI maana private sina huo mpango!
 
Niko form two tukagewa mtihani ambao ulikua na section ya Question Tags.

Sikumbuki swali ila lilikua la 'I am ...' so naassume..

I am a doctor, ... ?

Mi nikajibu ' ain't I?' nikakosa.

Nikaenda kwa mwalimu kulalamika akanijibu siyo kwamba haupo sahihi lakini sahihi zaidi ni 'aren't I?'

Nafikiri inaapply kwenye swala la hili swali. Mahakamani kuna watu wanafanya maamuzi, bungeni, mpaka kwenye maswala ya ndoa. Plus kutokana na kiswahili kukosa misamiati mingi tunakopa sana maneno hivyo mwalimu kuweka hiyo nyanjo siyo kwamba mtoto hayupo sahihi ila sahihi zaidi ingekua 'refarii'

Hili jibu la "aren't I?" kwenye question tags liliwahi kunipa shilingi 100 ya noti enzi hizo, mwalimu alijua wote tutakosea kumbe nimeshalipata mahali. Tulikuwa darasa la 7.
 
Unajua mfundishaji wa watoto shuleni ni mfundishaji ndio lakini jina specific analoitwa ni mwalimu. Sasa ukijibu mfundishaji haujakosea Sana ila sio sahihi kwa 100%.

Ni sawa na ukamuita mtu mlimaji badala ya mkulima, au muendeshaji badala ya dereva.
Case closed.
 
Refarii ndiyo jibu sahihi kwa mujibu wa kingozi cha mwalimu (marking scheme).

Mwamzi ni jina jumuishi sana mfano mwamzi mahakamani anaitwa Hakimu/Jaji.

Refarii ni (referee) ni neno la kiingereza, je kwenye kiswahili linatumika hivyo hivyo?
Kiplefti -Keep left
 
Nikiwa darasa la kwanza niliulizwa kwenye mtihani kuwa sare tunayovaa shuleni inaitwaje nikajibu ni sweta, shati na kaptura. Nilishindwa kabisa kujua kama yunifomu ni neno la kutumika katika Kiswahili, kati ya mitihani yangu pendwa ninayoitazama na kufurahia na ule upo.

Yunifomu? Duh
 
Unajua mfundishaji wa watoto shuleni ni mfundishaji ndio lakini jina specific analoitwa ni mwalimu. Sasa ukijibu mfundishaji haujakosea Sana ila sio sahihi kwa 100%.

Ni sawa na ukamuita mtu mlimaji badala ya mkulima, au muendeshaji badala ya dereva.
Referee ni kiingereza , kiswahili n mwamuzi, mwalimu kakosea
 
Refarii ni (referee) ni neno la kiingereza, je kwenye kiswahili linatumika hivyo hivyo?
Kiplefti -Keep left
Hadi hapa sijapata jibu sahihi inamaana huu mtihani na humu wote tungefeli au?
 
Jibu ni REFA

Neno mwamuzi limetumika kuuliza swali, kwahiyo huwez kulitumia kujibu swali. Mfundishe mwanao hii kitu isije kumuathiri huko mbele.

Mkuu hilo neno Referee sio ni kiingereza sema tumeozoea kulitumia tuu kwenye kiswahili kama vile Golikipa, Beki, Kamisaa na Fowadi?
 
Mkuu mwanao mjanja mjanja sana. Katelezea kwenye swali mule mule, mwamuzi wa mpira anaitwa, nae karudia mwamuzi!

Hivi mkuu nikikuuliza fundi wa ujenzi wa nyumba anaitwa nani utasema fundi au muashi

Tukiuliza askari wa usalama barabarani anaitwa nani utasema askari au trafiki

Tukiuliza muendesha ndege anaitwa nani utasema mwendesha ndege au rubani
Tanzania ina shida hii

Huon hapo unazunguka kwenye kizungu na kiswahili tu ?

Ndio wasomi lakn , mwalimu pamoja na wewe mmefeli
 
Imeishaje ? Hujui Referee n kiingereza na kiswahili ni Mwamuzi? Au wew ndio mwalimu nini?

Wengi tunatumia lugha kwa mazoea,Mkuu mimi ningesema mwalimu kamkosesha dogo, yaani ka set swali bila ufahamu wa kutosha neno referee halijatoholewa kuwepo kwenye kiswahili

Tuangalie huko huko kwenye mpira,hilo neno Referee (Refa) ni kiingereza ila tumeozoea kulitumia tuu kwenye kiswahili kama vile Golikipa, Beki, Kamisaa na Fowadi?

Siku huyo ticha akija na swali akisema

mshambuliaji wa mbele anaitwa nani-- atataka mwanafunzi aseme fowadi.
 
Tanzania ina shida hii

Huon hapo unazunguka kwenye kizungu na kiswahili tu ?

Ndio wasomi lakn , mwalimu pamoja na wewe mmefeli
Umeona nimeandika kizungu hapo?
 
Shule za msingi zinafungwa Leo, Niko hapa napitia mitihani na ripoti za wanangu!

Kuna swali hili; Mwamuzi wa mchezo wa mpira wa miguu anaitwa nani? Mwanangu kajibu MWAMUZI kakosa, eti mwalimu kawaambia jibu sahihi ni REFARII.

Je, jibu sahihi ni lipi hapo? Kosa ni la mtoto au mwalimu ndo hajielewi?

View attachment 1807716
View attachment 1807714
Mtoto yuko sahihi. Sidhani kama tuna neno la Kiswahili zaidi ya kumuita refa.
Nimependa mwandiko wa mtoto!
 
Traffic ni kimasai??

Referee ni neno la kiingereza, kiswahili ni mwamuzi
Kwahiyo katika kiswahili hakuna maneno yaliyoazimwa katika lugha zingine ikiwemo kingereza na yakawa rasmi?

Hospitali ni kiswahili au kizungu? Huwa hulitumii wewe?
 
Back
Top Bottom