Mwanangu wa darasa la pili hili swali kakosaje? Au mwalimu ndiye hajielewi?

Mwanangu wa darasa la pili hili swali kakosaje? Au mwalimu ndiye hajielewi?

Kwenye kamusi za kiswahili, mwamuzi na refa zote zina maana sawa
 
Kwa elimu yetu ya ukasuku ambayo siku ya mtihani mtoto anatakiwa kwenda kuyatapika yale aliyomezeshwa na mwalimu, na sio mawanda na mapana ya uelewa wake. Hapa mtoto wako anakuwa amekosea. Hakufundishwa hivyo.

Andika definition ya kitabuni kama unataka kufaulu mtihani- alisema professa wa Ranchodadas Chanchad!!
Virus.
 
Shule za msingi zinafungwa Leo, Niko hapa napitia mitihani na ripoti za wanangu!

Kuna swali hili; Mwamuzi wa mchezo wa mpira wa miguu anaitwa nani? Mwanangu kajibu MWAMUZI kakosa, eti mwalimu kawaambia jibu sahihi ni REFARII.

Je, jibu sahihi ni lipi hapo? Kosa ni la mtoto au mwalimu ndo hajielewi?

View attachment 1807716
View attachment 1807714
mkuu hiyoo ni swaga tu. ila jibu sahihi ni mwamuzi ni mwalimu mwenyewe kajichanganya kidogo kutokana na tafsiri yake kichwani kwa kingereza amejua kuwa kwa kiswahiili ndo hivyo hivyo
 
Mwanao yupo sahihi mwalimu ndio kajichanganya, mwalimu alipaswa kuuliza mchezeshaji wa mpira wa miguu anaitwa nani? Ili jibu liwe "mwamuzi"kwa kiswahili. Refarii ni lugha ya kiingereza tunayoitumi kimazoea, ni sawa na mtu anaposema naenda sheli kununua mafuta wakati kituo anachokwenda ni Total au Agip.
Barabara ya Ocean road[emoji41][emoji41][emoji41]
 
Jibu ni REFA

Neno mwamuzi limetumika kuuliza swali, kwahiyo huwez kulitumia kujibu swali. Mfundishe mwanao hii kitu isije kumuathiri huko mbele.
Mkuu
Mwamuzi wa mchezo Karate na Masumbwi anaitwaje?
 
Sio kila kitu lazima uki expose kwa mitandao ya kijamii acha utoto kama mwanao
 
Huu uzi tuupeleke Jukwaa la Lugha.
Hata huko mambo hayatakuwa rahisi mkuu, hili swali sio lakitoto hata kidogo sijui ilikuwaje tu hadi akaulizwa mtoto!? Angalia maveterani wa Jf wanavyosugua bongo bila muafaka kupatikana!!
 
Back
Top Bottom