Mwanangu wa darasa la pili hili swali kakosaje? Au mwalimu ndiye hajielewi?

Mwanangu wa darasa la pili hili swali kakosaje? Au mwalimu ndiye hajielewi?

Refarii ndiyo jibu sahihi kwa mujibu wa kingozi cha mwalimu (marking scheme).

Mwamzi ni jina jumuishi sana mfano mwamzi mahakamani anaitwa Hakimu/Jaji.
Kiongozi cha mwalimu (teachers guide)
 
Aisee darasa la kwanza mpaka la nne nilikuwa nacheza namba 1-3,nilipofika la tano nikaanza kuona mapichapicha mara wa 10 mara wa 50. Secondary ndio usiseme bora nikae kimya
Nalog off
 
Mwalimu alishindwa kutunga swali. Alipaswa kuuliza hivi msimamizi wa mchezo uwanjani huitwa...... Ili jibu liwe mwamuzi.

Alichouliza ni mwamuzi kwa lugha nyingine huitwa......
 
Mwalimu alishindwa kutunga swali. Alipaswa kuuliza hivi msimamizi wa mchezo uwanjani huitwa...... Ili jibu liwe mwamuzi.

Alichouliza ni mwamuzi kwa lugha nyingine huitwa......
Upo sawa kabisa
 
Shule za msingi zinafungwa Leo, Niko hapa napitia mitihani na ripoti za wanangu!

Kuna swali hili; Mwamuzi wa mchezo wa mpira wa miguu anaitwa nani? Mwanangu kajibu MWAMUZI kakosa, eti mwalimu kawaambia jibu sahihi ni REFARII.

Je, jibu sahihi ni lipi hapo? Kosa ni la mtoto au mwalimu ndo hajielewi?

View attachment 1807716
View attachment 1807714
Mwanao anaonekana anatumia akili sana katika kutatua matatizo. Yeye amejikita katika kutafsiri neno badala ya kujibu swali. Amekosa kwa kuwa mwamuzi wa mchezo katika mazingira yetu ni refarii na ndio jibu la swali aliloulizwa.
 
Huyo mtoto anaakili sana ndo maana ameshidwa kujibu hilo swali sio kwamba halijui analijua vzr
 
Mwanao ana mwandiko mzuri (kwa darasa la pili, ni jambo kubwa). Hongera zake.
 
Yaani nawe umekaa na mtoto ukamwambia ni kweli mwalimu kakukosesha? we bogus kweli
 
Waamuzi wa mpira wapo zaidi ya mmoja uwanjani,kwa ligi yetu wapo 4,,kwa ligi kubwa za ulaya baadhi ya mechi wapo 5.


Mwamuzi anayezungumziwa hapa ni mwamuzi wa kati,yaani REFARII. Hivyo swali lilipaswa kuwa:
Mwamuzi wa kati wa mpira wa miguu huitwa.............
Watoto wa sasa wanaweza wakasema VAR...maana nayo pia hutoa maamuzi[emoji848][emoji848]
Na pia hizo kategory hufundishwa kwa level mtoto wa darasa la pili atafundishwa in general kwamba mwamuzi wa mpira ni refa akienda level za juu ndo anaweza kuta mgawanyiko wa hao waamuzi
 
Rejea kwenye kamusi ya Kiswahili sanifu uone. Huenda tamko "Referee" limetoholewa na likawa "Refa" kwa Kisawahili.

Ila huko google uliporejea jibu lao lina ukakasi sababu hatujui huyo aliyeweka maana ya hiyo kwa Kiswahili amerejea wapi.

Almuhimu kama rejea inasema ni Muamuzi,basi mwalimu amekosea a atakiwa kusahihishwa na aambiwe.

Ni hayo tu.
Ye amerejea kamusi ya wapi
IMG_20210604_150936.jpg
 
Wengi tunatumia lugha kwa mazoea,Mkuu mimi ningesema mwalimu kamkosesha dogo, yaani ka set swali bila ufahamu wa kutosha neno referee halijatoholewa kuwepo kwenye kiswahili

Tuangalie huko huko kwenye mpira,hilo neno Referee (Refa) ni kiingereza ila tumeozoea kulitumia tuu kwenye kiswahili kama vile Golikipa, Beki, Kamisaa na Fowadi?

Siku huyo ticha akija na swali akisema

mshambuliaji wa mbele anaitwa nani-- atataka mwanafunzi aseme fowadi.
Emu we baba mtoto ulitakaje
IMG_20210604_150936.jpg
 
Sio mbaya akishafundishwa kuhusu kutohoa mambo kama hata hayatamshinda
 
Shule za msingi zinafungwa Leo, Niko hapa napitia mitihani na ripoti za wanangu!

Kuna swali hili; Mwamuzi wa mchezo wa mpira wa miguu anaitwa nani? Mwanangu kajibu MWAMUZI kakosa, eti mwalimu kawaambia jibu sahihi ni REFARII.

Je, jibu sahihi ni lipi hapo? Kosa ni la mtoto au mwalimu ndo hajielewi?

View attachment 1807716
View attachment 1807714

Mfumo wa ufundishaji usio rafiki kwa fikra-tunduizi.
 
Back
Top Bottom