Super Sub Steve
JF-Expert Member
- Jul 9, 2011
- 17,404
- 10,900
La kumi na moja dogo chenga kabugi.Mwalimu yupo sahihi.Tangu lini udongo wa kichanga ukatumika kufinyanga?Kwangu naona swali la 11 na swali la 15 yamekatwa kimakosa!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
La kumi na moja dogo chenga kabugi.Mwalimu yupo sahihi.Tangu lini udongo wa kichanga ukatumika kufinyanga?Kwangu naona swali la 11 na swali la 15 yamekatwa kimakosa!
Mwalimu Kaneli aliniandikia vile. Unajua matatizo sio ya walimu ni ya hizi taasisi za Kiswahili zinarahisisha mambo na kuzembea kwenye kukuza lugha. Zinapotosha, unakuta kamusi za siku hizi neno helicopter wanaita "helikopta" eti ndio wametafsiri. Ukichukua TUKI za miaka ya sabini kuna maneno ya ndani kabisa.Yunifomu? Duh
Jibu kwanza mkuu kisha nawewe ndio uulize.Umeshawasiliana na mwalimu?
OohhMwalimu Kaneli aliniandikia vile. Unajua matatizo sio ya walimu ni ya hizi taasisi za Kiswahili zinarahisisha mambo na kuzembea kwenye kukuza lugha. Zinapotosha, unakuta kamusi za siku hizi neno helicopter wanaita "helikopta" eti ndio wametafsiri. Ukichukua TUKI za miaka ya sabini kuna maneno ya ndani kabisa.
Tunatakiwa kuwa na maneno mapya kama chakachua, piga tafu, tarakirishi, sharubati. Sio maneno kama internet ~ intaneti.
Mwanao yupo sahihi mwalimu ndio kajichanganya, mwalimu alipaswa kuuliza mchezeshaji wa mpira wa miguu anaitwa nani? Ili jibu liwe "mwamuzi"kwa kiswahili. Refarii ni lugha ya kiingereza tunayoitumi kimazoea, ni sawa na mtu anaposema naenda sheli kununua mafuta wakati kituo anachokwenda ni Total au Agip.Shule za msingi zinafungwa Leo, Niko hapa napitia mitihani na ripoti za wanangu!
Kuna swali hili; Mwamuzi wa mchezo wa mpira wa miguu anaitwa nani? Mwanangu kajibu MWAMUZI kakosa, eti mwalimu kawaambia jibu sahihi ni REFARII.
Je, jibu sahihi ni lipi hapo? Kosa ni la mtoto au mwalimu ndo hajielewi?
View attachment 1807716
View attachment 1807714
refarii si kiswahili mkuu!!Thread imeishia hapa....safi sana mkuu shakir.
tatizo jibu la mwalimu halipo kwenye lugha aliyoitumia kuulizia swali. Tukubaliane tu kwamba Mwalimu alijichanganya kwenye kuunda swali.Jibu ni REFA
Neno mwamuzi limetumika kuuliza swali, kwahiyo huwez kulitumia kujibu swali. Mfundishe mwanao hii kitu isije kumuathiri huko mbele.
Maswali ya chemsha bongo ndivyo yalivyo.La pili! Basi kijana wako yupo vizuri, lakini jibu hilo ni kweli kakosea.
Haiwezekani 'structure' ya swali ikatumika kuwa ndiyo jibu la swali hilo hilo....'Mwamuzi' wa michezo halafu jibu liwe 'mwamuzi' hiyo hiyo.
Alama ya kosa anaweka kidogooooo....hata hakaonekani vizuri...sijui ndo kubania wino!!!
Huu nao ni ubinfsi chalii, akaulize wapi sasa Facebook? Akili za Facebook na za humu zipo tofautiJamani Jf ishakuwa dampo kila kitu hapa !!!
Kabisaatatizo jibu la mwalimu halipo kwenye lugha aliyoitumia kuulizia swali. Tukubaliane tu kwamba Mwalimu alijichanganya kwenye kuunda swali.
Jibu ni REFA
Neno mwamuzi limetumika kuuliza swali, kwahiyo huwez kulitumia kujibu swali. Mfundishe mwanao hii kitu isije kumuathiri huko mbele.
Kww hiyo mtoto alikuwa sahihi kabisa. Maana kama mwalimu akisema jibu ni Refarii, hicho siyo kiswahili.
VAR ni aid kwenye maamuzi haitoi maamuziWaamuzi wa mpira wapo zaidi ya mmoja uwanjani,kwa ligi yetu wapo 4,,kwa ligi kubwa za ulaya baadhi ya mechi wapo 5.
Mwamuzi anayezungumziwa hapa ni mwamuzi wa kati,yaani REFARII. Hivyo swali lilipaswa kuwa:
Mwamuzi wa kati wa mpira wa miguu huitwa.............
Watoto wa sasa wanaweza wakasema VAR...maana nayo pia hutoa maamuzi[emoji848][emoji848]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Sio mwalimu hajielwi bali mwanao ndio hajielewi na mpumbavu
Mtoto wako yupo na good handwriting.
Mpe pongezi kutoka kwangu.