Unaweza ukawa wa mwisho kwenye darasa lenye watanfunzi wenye akili sana au ukawa wa kwanza kwenye darasa la wajinga.
Nilichokuja kugundua baadae elimu ya high school na kuendelea inataka mtu wa kukariri sana, msuli mkubwa hadi unatoboa usiku. Hicho kitu kilinishinda.
Nashukuru kwamba C zangu nilikua nazifidia na vitu vingine nje ya shule ambavyo ndio vimenisaidia sana.
Mfumo wetu wa elimu ni wa hovyo sana, unatujenga kukariri tuuu na kufaulu mitihani badala ya kutupatia skills za kupambana na maisha.
Huku mtaani ama hata kazini As hazihitajiki kabisa, watu wanachotaka ni wewe kua na uwezo na skills za kufanya kazi inayohitajika kwa viwango vinavyohitajika.
Nakumbuka nimewahi kufanya kazi moja na watu waliosoma Malaysia, Uk, France, Netherlands na Kenya, nikafanya poa sana hadi wasimamizi wakaniuliza kama nimesoma nje ya nchi, nikawaambia hapana. Hawakuamini na wala hawakutegemea kama ningeweza kufanya vile. Sasa hizo skills na capabilities nimezijenga mwenyewe, sikuzipata chuoni wala high school.
Vijana wanamaliza vyuo vikuu reasoning hakuna, analytical skills hakuna ila wana As nyingi.
Tubadili mfumo wa Elimu.