Mwanao anaongoza darasani au alikua anaongoza, nini ulifanya kufanikisha hilo?

Kama ni kilaza focus na kipaji chake usimpotezee mtoto muda maana elimu yetu haina maana sana sikuhizi! Kazi hamna mtoto unamkalisha darasani miaka 17 ni upuuzi tu
Excellent! Japo hajasema ni level ipi ya elimu.. Kama ni primary hawezi kwepa.. Pia O-level hawezi kwepa pia. Lazima apate basics hata kama atakuwa wa mwisho.
La kuzingatia ni wakati anahakikisha anapata hizo basics, awe anahakikisha anatambua matakwa (comfort zone) ya mwanae ili aanze kumuwashia torch
 
Mie hata simfatilii na sinaga huo muda kabisa ila ndo hivo wa kwanza au wapili akishika watatu atarudi nyumban na kilio halaf m namshangaa sa unalia nini?
Kula cartoon na mwanao mzee..
Baadhi ya ambazo sisi tumeshakula;
1. Chicken run
2. Madagascar...
3. Puss in boots
4. Coco
5. Shrek
6. Ice age
7. Khumba
8. Frozen/Elsa
9. Ralph breaks the internet
10. Zootropia
11. Hotel translvania
12. Ballerina (Ballery dance...)
13. Barbie
14. Etc.

Sisi tunasubiri tufike P5 tuanze shule rasmi.. Kwasasa tunaelezana concept ndogo ndogo tu..
 
Mimi mwanangu hana tution Wala Nini ,nahisi kilichomsaidia ni ugomvi uliokuwawako Kati yangu na mama yake,maana dogo shule ndo ilikuwa home kwake,kaanza kwenda shule akiwa na miaka 2,nilikataa kumuweka mfanyakazi nyumbani wa kumlea ,nikasema atashinda shule,Sasa Yuko darasa la 4 anakuwaga wa kwanza au wa pili,
 
Hello bosses,

Kama mwanao anaongoza darazani angalau nafasi 10 za juu.

Je, nini ulikifanya kufanikisha hilo?,

Mtoto anapata shule nzuri, tuition za kutosha, muda wa kupumzika, homework n.k lakini bado maendeleo yake ya shule sio ya kuridhisha.
Kwani kuongoza ndo nini? Diamond unazani alikuwa anaongoza Darasani?
 
Huwa nawakagua kazi zao kila wiki, hapo ni kuanzia upangaji wa kazi zao mpaka mwandiko, nawasisitiza kufanya kazi zao za nyumbni wenyewe ila nawapangia muda...siangalii amekuwa wa ngapi ila naangalia alama zake ni zipi...! Maendeleo yao yanaridhisha! Kijana yuko 5 kadada kapo 2..[emoji4]
 
Nashukuru hata mimi mwanangu yupo kwenye topu teni, alikuwa wa 8 kati wa wanafunzi 11. Ninachofanya ili asitoke kwenye topu teni ni kumsisitiza asome. Asandi sana
Top 10 then? Je huyo mtoto Maisha halisi anaweza pambana? Ukiacha huo u top 10?
 
Muvi za kitoto ni zipi? Zile katuni zs wazungu? Zs ku fanya watoto kuwa wajinga?
 
Sometimes kushika nafasi ya juu inategemeana na wanafunzi wengine wakoje.

Unaweza kuwa unakuwa wa kwanza shule fulani lakini ukihamishwa shule, huko kwingine hata top 10 unaitafuta kwa tochi.
 
Duh, kuna watu bado wana imani na elimu ya Tz
Wana imanai na matokeo hawana imani na elimu? Yaani nacheka humu, yaani mtoto anakuwa wa kwanza kwenye mfumo upi wa elimu? Hahaa aiseee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…