Mwanasheria: Barua ya Job Ndugai kujiuzulu Uspika ni batili kwa mujibu wa Katiba

Mwanasheria: Barua ya Job Ndugai kujiuzulu Uspika ni batili kwa mujibu wa Katiba

katibu wa Bunge amesema Bunge limepokea nakala tu,
hivyo hawafanyii kazi nakala wanasubiri barua rasmi.

Katibu wa CCM anasema ameshapeleka barua rasmi kwa Katibu wa bunge.

Lakini bado haiondoi hoja kwamba alitakiwa spika alitaarifu bunge kupitia katibu wa bunge.

Sasa hapo ndio unaposhangaa chombo cha kutunga sheria kinaposhindwa kuelewa taratibu na mambo madogo kama haya.

Ndio maana wanapitisha mambo bila umakini baadae wanaongea tofauti utafikiria ni jambo geni kabisa.
 
Period! Nakala huwa haifanyiwi kazi. Ni taarifa tu anapewa aliyenakiliwa!
... naanza kupata picha kwamba hiyo barua Ndugai aliandikiwa na kazi yake ikawa moja tu - kusaini tena mbele ya "chuma". Kwa stress zile hakuwa na namna zaidi ya kusaini. Ni mtego aliwekewa ili wapate sababu ya kumfukuza akose haki zake zote.
 
procedure anatakiwa aandike barua kwa katibu wa bunge ampe nakala katibu wa ccm,yeye kafanya tofauti kaandika barua kwa katibu wa ccm na kumpa nakala katibu wa bunge!
... in short Katibu wa Bunge ambaye ndiye mamlaka ya kujiuzulu Spika Kikatiba hana taarifa rasmi kwamba Spika kajiuzulu zaidi ya kusikiasikia huko tu!
 
katibu wa Bunge amesema Bunge limepokea nakala tu,
hivyo hawafanyii kazi nakala wanasubiri barua rasmi.
Yaonekana Katibu wa Bunge bado hajitambui wala hajijui kuwa hana uwezo wa kuyazuia hata kama kuna makosa katika mtiririko wake.
Pia, maji haya yanamzidi kimo, kwani hata yale mamlaka fake aliyokuwa anavalishwa na Ndugai ili kukomoa wengine , nayo sio tu hayapo tena bali yatakuwa ndio sababu za kumnyoa nae.
 
procedure anatakiwa aandike barua kwa katibu wa bunge ampe nakala katibu wa ccm,yeye kafanya tofauti kaandika barua kwa katibu wa ccm na kumpa nakala katibu wa bunge!
Wewe hiyo ni minor,na kama amefanya kwa kupitiwa au kutojua ni kitu insignificant,afu barua inaweza badilishwa cha muhimu kaandika barua kujiuzuru.
 
Ndugai amekua bungeni kwa kipindi kirefu na anajua taratibu za kisheria za kujiuzulu, amepeleka barua kwenye chama chake ukiwa ni utaratibu wa awali ili chama kiwe na muda wa kuandaa spika mwingine.

Japokua nafasi ya spika sio lazima uwe mwanachama lakini ni dhahiri spika mwingine atatoka CCM.

Hivi hakuna kikao cha bunge kinachoendelea ninaamini atafuata tu taratibu za kisheria, ambazo anazijua.
 
Anaejiuzulu anaweza kupeleka barua popote anapota mradi tu pia apeleke barua hio hio kwa bosi wake wa kazi anayotaka kujiuzulu.
We hujui... unapeleka popote lakini mwenye mamlaka ya kukubali au kukataa kujiuzulu kwako ndiye anakuwa mlengwa mkuu, wengine wanapewa nakala kwa maana ya kutaarifiwa tu ya kinachoendelea
 
... in short Katibu wa Bunge ambaye ndiye mamlaka ya kujiuzulu Spika Kikatiba hana taarifa rasmi kwamba Spika kajiuzulu zaidi ya kusikiasikia huko tu!
Basi Sawa, kama hana taarifa rasimi, mimi ntamwambia badaye!
 
Kwani wakati wa kugombea Uspika nani alipeleka jina la Ndugai kwa Katibu wa Bunge,na wakati wa kutaka kugombea Uspika Ndugai aliomba kwa nani nafasi ya kugombea.
 
Leo nimesikiliza Mwanasheria mmoja kupitia UTV ameeleza kuwa kwa mujibu wa Katiba Spika akitaka kuachia madaraka anapaswa kulitaarifu Bunge na si Chama kama alivyofanya. Je Bunge litakuwa na uhalali wa kufanyia kazi barua yake kama asipoandika barua kwa Katibu wa bunge?
Imeisha hiyo mjomba,hakuna tena muujiza.
D673B8B3-332A-4EC2-A3B2-8C7172E634AC.jpeg
 
We hujui... unapeleka popote lakini mwenye mamlaka ya kukubali au kukataa kujiuzulu kwako ndiye anakuwa mlengwa mkuu, wengine wanapewa nakala kwa maana ya kutaarifiwa tu ya kinachoendelea
Mi kweli sijui, ila hapa hakuna ishu, kama barua imepelekwa palapa husika na imepokewa haijalishi kama kaipeleka mwanzo au mwisho,kinachohitajika ni barua ya kujiuzulu tu na sio kuwahi au Kuchelewa kuipeleka.
Pia akitaka kujiuzulu ubunge anaweza akawapelekea wapigakura wake wote barua mwanzo kisha asije kusahau kupeleka bungeni tu na anaweza akachelewa hata wiki nzima mradi tu na bungeni apeleke barua.
 
katibu wa Bunge amesema Bunge limepokea nakala tu,
hivyo hawafanyii kazi nakala wanasubiri barua rasmi.
Katibu wa Bunge kama anaipenda kazi yake atakanusha hii taarifa na kufanyia kazi mchakato wa speaker chap chap.
 
Mi kweli sijui, ila hapa hakuna ishu, kama barua imepelekwa palapa husika na imepokewa haijalishi kama kaipeleka mwanzo au mwisho,kinachohitajika ni barua ya kujiuzulu tu na sio kuwahi au Kuchelewa kuipeleka.
Pia akitaka kujiuzulu ubunge anaweza akawapelekea wapigakura wake wote barua mwanzo kisha asije kusahau kupeleka bungeni tu na anaweza akachelewa hata wiki nzima mradi tu na bungeni apeleke barua.
Maneno yako matatu ya mwanzo kwenye bandiko hili (nayanukuu... Mi kweli sijui... mwisho wa kunukuu) yanasababisha niache kuendelea kukueleza.. Maana hujui na unaelezea kuonyesha unajua
 
Mh. Raisi hebu fanya 'special order' ili Prof. Assad aende akafanye 'special auditing' ya ofc ya huyu mheshimiwa.

Nakuomba sana mama, huenda tukayajua mengi nyuma ya pazia.
 
Back
Top Bottom