Habari zilizotufikia ni kwamba Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Jaji Mark Bomani amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Septemba 11, 2020, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mtoto wake amethibitisha kifo hiki. Shughuli za msiba zipo nyumbani kwa Marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.
View attachment 1565939
Jaji Mstaafu Mark Bomani enzi za uhai wake akiwa na mkewe wakikata keki katika hafla ndogo ya kusherehekea miaka 50 ya ndoa yao mwaka 2017
WASIFU WAKE KWA UFUPI
Mzaliwa wa Pemba, Zanzibar. Mwanasheria Mkuu wa 2 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mzawa wa kwanza kushika wadhifa huo. Kwa miaka 11 alisimama kidete kuitetea serikali ya Mwl. Nyerere. Jana, Septemba 10, 2020 amemaliza kazi aliyotumwa duniani.
Alizaliwa mwaka 1943 huko wilayani Wete kisiwani Pemba, Zanzibar. Elimu ya msingi alipatia huko huko kabla ya kujiunga na shule ya sekondari ya wavulana ya Tabora, Tanganyika. Baadae alienda nchini Uganda na kujiunga na elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Makerere.
Aliporudi masomoni, Mark Boman alijiunga na chama cha TANU na mwaka 1965, Mwalimu Nyerere alimteua kuwa Mwanasheria mkuu wa Serikali ya Tanzania. Alikuwa Mtanzania mzawa wa kwanza kushika nafasi hiyo aliyohudumu mpaka mwaka 1976
Baada ya kazi ya Serikali, Mark aliteuliwa na kuwa mshauri mkuu wa maswala ya kisheria wa umoja wa mataifa nafasi aliyohudumu kwa takribani miaka 14 (1976 - 1990), akishiriki vyema katika michakato iliyopelekea kupatikana kwa uhuru wa nchi za Namibia na Afrika Kusini.
Moja kati ya huduma kubwa za kimataifa alizowahi kuzifanya ni kushiriki katika majadiliano ya amani baina ya pande mbili wakati wa vita ya kwanza ya wenyewe kwa wenyewe nchini Burundi. Mark, alikuwa Katibu mkuu wa Mwl. Nyerere na Mzee Mandela wakati wote wa zoezi hilo.
Baadhi ya mada kuhusu Jaji Bomani
>
Jaji Mark Bomani: Serekali 2 au 3 zisijadiliwe kwenye Bunge la Katiba!
>
Jaji mstaafu Mark Bomani naye atoa mpya..
>
Jaji Mstaafu Mark Bomani akataa Tanzania kuitwa Tanzania Bara, ataka iitwe Tanganyika
>
Jaji Mark Bomani: Ni vizuri kukawepo kura ya maoni kuhusu Muungano (Referendum)
>
Jaji Mstaafu Mark Bomani aunga mkono Serekali 3 asema wasemao ni harama hawana mashiko
>
Muungano lazima ujadiliwe kwa Ukweli na Uwazi! - Jaji Mark Bomani
>
Jaji Bomani: Wageni wanaimaliza nchi kupitia sekta ya madini
>
Jaji Bomani apigilia msumari Katiba Mpya
>
Jaji Bomani: ZEC imejipunguzia imani
>
Jaji Bomani awachafua wazanzibari
>
Bomani: Gamba litapasua CCM