Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umemaliza mwendo babu Judge Mark Bomani RIP, Poleni familia ya mwendazake pamoja na marafiki zake wote wa karibu kama Judge Joseph S. Warioba, Amb. Juma V. Mwapachu & co.
Kweli maccm makatili sn..... Hata Mkapa akiwa hai walikaa kimya amekua wamepeleka maiti uwanjani ndo rais anatangaza utaitwa Mkapa......How,Kama alikuwa hai hawakujali,iwe leo!
bangi unayovuta inakuharibu mpaka unapotosha kwa makusudiPigo kubwa sana , nakumbuka kaka yake aliyeitwa Paulo alishirikiana na Mwl Nyerere kuanzisha BAKWATA
Mzanzibar ...! na Chief wa Wasukuma!?Kumbe Jaji Mark Bomani ni Mzanzibari! Sikuwahi kujua hili. RIP
nimevutiwa na background
Pumzika kwa Amani Mzee wetu
Habari zilizotufikia ni kwamba Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Jaji Mark Bomani amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Septemba 11, 2020, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mtoto wake amethibitisha kifo hiki. Shughuli za msiba zipo nyumbani kwa Marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.
View attachment 1565939WASIFU WAKE KWA UFUPI
Jaji Mstaafu Mark Bomani enzi za uhai wake akiwa na mkewe wakikata keki katika hafla ndogo ya kusherehekea miaka 50 ya ndoa yao mwaka 2017
Mzaliwa wa Pemba, Zanzibar. Mwanasheria Mkuu wa 2 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mzawa wa kwanza kushika wadhifa huo. Kwa miaka 11 alisimama kidete kuitetea serikali ya Mwl. Nyerere. Jana, Septemba 10, 2020 amemaliza kazi aliyotumwa duniani.
Alizaliwa mwaka 1943 huko wilayani Wete kisiwani Pemba, Zanzibar. Elimu ya msingi alipatia huko huko kabla ya kujiunga na shule ya sekondari ya wavulana ya Tabora, Tanganyika. Baadae alienda nchini Uganda na kujiunga na elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Makerere.
Aliporudi masomoni, Mark Boman alijiunga na chama cha TANU na mwaka 1965, Mwalimu Nyerere alimteua kuwa Mwanasheria mkuu wa Serikali ya Tanzania. Alikuwa Mtanzania mzawa wa kwanza kushika nafasi hiyo aliyohudumu mpaka mwaka 1976
Baada ya kazi ya Serikali, Mark aliteuliwa na kuwa mshauri mkuu wa maswala ya kisheria wa umoja wa mataifa nafasi aliyohudumu kwa takribani miaka 14 (1976 - 1990), akishiriki vyema katika michakato iliyopelekea kupatikana kwa uhuru wa nchi za Namibia na Afrika Kusini.
Moja kati ya huduma kubwa za kimataifa alizowahi kuzifanya ni kushiriki katika majadiliano ya amani baina ya pande mbili wakati wa vita ya kwanza ya wenyewe kwa wenyewe nchini Burundi. Mark, alikuwa Katibu mkuu wa Mwl. Nyerere na Mzee Mandela wakati wote wa zoezi hilo.
Baadhi ya mada kuhusu Jaji Bomani
> Jaji Mark Bomani: Serekali 2 au 3 zisijadiliwe kwenye Bunge la Katiba!
> Jaji mstaafu Mark Bomani naye atoa mpya..
> Jaji Mstaafu Mark Bomani akataa Tanzania kuitwa Tanzania Bara, ataka iitwe Tanganyika
> Jaji Mark Bomani: Ni vizuri kukawepo kura ya maoni kuhusu Muungano (Referendum)
> Jaji Mstaafu Mark Bomani aunga mkono Serekali 3 asema wasemao ni harama hawana mashiko
> Muungano lazima ujadiliwe kwa Ukweli na Uwazi! - Jaji Mark Bomani
> Jaji Bomani: Wageni wanaimaliza nchi kupitia sekta ya madini
> Jaji Bomani apigilia msumari Katiba Mpya
> Jaji Bomani: ZEC imejipunguzia imani
> Jaji Bomani awachafua wazanzibari
> Bomani: Gamba litapasua CCM
Ni ndugu. Mie nikijua huyu atakuwa na umri karibia miaka 90!Mark bomani na paul bomani wanaundugu au ni majina tuh kufanana??
Mwenyewe sikufikiria kabisa Kama ni kutoka visiwani. R.i.p jajiAlizaliwa Wete Pemba?Mzanzibari??
Born in Pemba, raised and grew up in his homeland Tanganyika.Mwenyewe sikufikiria kabisa Kama ni kutoka visiwani. R.i.p jaji
CCM IMECHOKWAHali si hali watu, watanzania baadhi kama siyo wote wamechoka, kufuatia kifo cha Jaji mstaafu Mark Bomani, hii ni tweet ya rais wa Tanzania;
"Nawapa pole familia na wote walioguswa na kifo cha Jaji Mstaafu Mark Bomani. Nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa Serikalini katika masuala ya sheria na katika chama akiwa Mjumbe wa Baraza la Wadhamini wa CCM. Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina."
Baada ya tweet hiyo hapa chini ni baadhi ya comments za wananchi wake wakimpa pole 😂...
View attachment 1566754
Kwani duniani wavuta bangi wanakosa?Mwenyewe nilizipitia hizo comments nikajiuliza Magu sijui kitu gani kinamfanya afikiri anapendwa, raia wamemsiliba haswa!
Na hao wanao andika ni washabiki wa chadema, baada ya kupigwa za uso kwenye kampeni hivyo wamenuna.Anapata anachostahili