Mwanasheria Mkuu: Wabunge wa CHADEMA wa Viti Maalumu waliapishwa kwa mujibu wa Sheria na Katiba, CHADEMA isiwaguse

Mwanasheria Mkuu: Wabunge wa CHADEMA wa Viti Maalumu waliapishwa kwa mujibu wa Sheria na Katiba, CHADEMA isiwaguse

Mwanasheria mkuu wa serikali amesema mchakato wa uteuzi na uapishwaji wa wabunge wa viti maalumu wa Chadema ulifuata taratibu zote za kisheria na kikatiba.

AG amewaonya Chadema kutowagusa wabunge hao kwani mkono wa sheria utawafuata popote walipo.

Source: Gazeti la Uhuru

Maendeleo hayana vyama!
Kumbe zile sheria kandamizi na zenye vioja zilizotungwa kabla ya Bunge lililopita kuvunjwa, zilikuwa na lengo la kuwapa viongozi dhalimu wawe na kinga za kutokushtakiwa kutokana na madudu ambayo wataelekezwa kuyatekeleza.

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
 
Pamoja na kuwepo kwa umoja wa wanawake ktk karibu kila chama lakini haujaweza kuondoa mfumo dume ktk hizi taasisi...

Hakuna umoja wa wanaume na wanaume ni wachache lakini ndio kama wenye maamuzi...

CHADEMA umaneni, mpeni mitano mingine Mbowe hata akikaa milele kama Prof. Lipumba, Mbatia, Mrema, Cheyo Momose ni Sawa si katiba itakuwa ina ruhusu na wanachama watakuwa wameamua iwe hivyo
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema mchakato wa uteuzi na uapishwaji wa wabunge wa viti maalumu wa CHADEMA ulifuata taratibu zote za kisheria na kikatiba.

AG amewaonya CHADEMA kutowagusa wabunge hao kwani mkono wa sheria utawafuata popote walipo.

Chanzo: Gazeti la Uhuru

Maendeleo hayana vyama!
AG amejuaje nini CHADEMA watawafanya hao watuhumiwa mpaka atoe tamko leo!? vipi je wasipowafanya lolote. Aiseee akili za kutumwa changanya zako..Hivi huyu ni Prof. Kweli?
 
Nawapongeza sana hawa wakina Mama,

Hongereni CHADEMA kwa kuwaruhusu kwenda kuapa,

Hongereni Watanzania kwa kuendelea kuenzi amani na umoja waliotuachia waasisi wa Taifa hili.

Mama TANZANIA ni wajibu wetu kumtunza kwa kuenzi AMANI NA UMOJA.
 
Wawafukuze tupate kujua undani wa sakata la "kura feki"! So far wanaongea wao tu, pengine kuanzia kesho tutawasikia na kina Mdee...
 
AG anahusika Vipi na maamuzi ya CDM?.
Kusifu Na Kuabudu
Maombi Na Maombezi

Wanamfurahisha Yule, Nikikumbusha Form Ya Kugombea Nafasi Ya Ubunge Jimbo La Ubungo
Ulijaa Ujanjaujanja Tu,DED Anakuwa Snitch Baadaye Kaumbuka
Acha Tuone Hili
 
Mwaka jana kulivuja sauti ya wabunge wa Chadema Said Kubenea na Anthony Komu wakipanga njama za kumuuwa Boniface Jacob ili hatimae wafanikishe adhima yao ya kumng'oa Freeman Mbowe kwenye uenyekiti wa chama.

Baada ya sauti hizo kuvuja mara moja chama kilitangaza kikao cha dharura cha kamati kuu kuwahoji ili waweze kuchukuliwa hatua kali sana ikiwa pamoja na kufukuzwa Chadema.
Matokeo yake baada ya kikao cha kamati kuu hao wabunge wauaji walisamehewa na kutakiwa kuomba radhi tu!!!

Kama hali ni hiyo, wabunge wa viti maalum Chadema si wauaji na wala hawajatishia kumuuwa mtu yoyote ila wanajaribu tu kutumia haki yao ya kikatiba iweje wafukuzwe Chadema?
Kweli kuwa mwanamke Chadema ni dhambi kubwa kuliko wapanga mauaji waliosamehewa??

Tusubiri na kuona kesho kikao cha kamati kuu chadema kitaamua nini ,bila shaka Mbowe is going to be tested again na maamuzi tofauti na kufukuza yatamwimalisha ,na maamuzi ya kufukuza hao wanawake itakuwa ni kiss of death kwa Mbowe na Chadema kwa ujumla.
Umeshasema mwaka juzi
 
DED3D669-4DB0-42F6-9768-CA7ECBF58B75.jpeg
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema mchakato wa uteuzi na uapishwaji wa wabunge wa viti maalumu wa CHADEMA ulifuata taratibu zote za kisheria na kikatiba.

AG amewaonya CHADEMA kutowagusa wabunge hao kwani mkono wa sheria utawafuata popote walipo.

Chanzo: Gazeti la Uhuru

Maendeleo hayana vyama!
Huyo siyo Mwanasheria mkuu ni mwanamatakwa ya CCM
 
Je, SOPHIA SIMBA hakuapishwa 2015 kwa mujibu wa katiba na sheria? AG tueleze.
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema mchakato wa uteuzi na uapishwaji wa wabunge wa viti maalumu wa CHADEMA ulifuata taratibu zote za kisheria na kikatiba.

AG amewaonya CHADEMA kutowagusa wabunge hao kwani mkono wa sheria utawafuata popote walipo.

Chanzo: Gazeti la Uhuru

Maendeleo hayana vyama!
Hii inaitwa "kutishiana nyau."

Mtu kufukuzwa chama kumeanza leo?

Ama kweli pori hili la sasa wameingia nyani wapya!

Kama hawa unaowaongelea ni wanachama wa CDM basi na mtege masikio. Kwani ni mbali basi:

Kesho Ijumaa mtanange unaanza saa mbili juu ya alama!
 
Hivi wa hayo yanayoendelea bado kuna mtu na akili zake timamu anashabikia siasa?
Kama wapo basi wakapimwe akili
 
Back
Top Bottom