Mwanasheria Mkuu: Wabunge wa CHADEMA wa Viti Maalumu waliapishwa kwa mujibu wa Sheria na Katiba, CHADEMA isiwaguse

Mwanasheria Mkuu: Wabunge wa CHADEMA wa Viti Maalumu waliapishwa kwa mujibu wa Sheria na Katiba, CHADEMA isiwaguse

Maajabu ya mwaka haya. Kwa iyo amesema kifungu gani cha sheria kinakataza vyama kuwashughulikia wanachama wake??? Na amesema yeye Kama nani??? Tangu lini mwanasheria mkuu wa serikali akavisemea vyama??? Kweli Fatma Karume alikuwa sawa juu ya huyu jamaa
Hawa jamaa wako desperate na hela za mabeberu mpaka wanafanya upuuzi uliopitiliza!
 
AG ajibu hoja za Katibu Mkuu Mnyika kama alivyoweka wazi kwenye press conference. Nyaraka zile zilizopo NEC zenye majina, sahihi na mihuri nani kagushi? Kamati kuu ya chama imekaa lini kuteua majina?
Siyo anatoa jibu la jumla kama anawajibu watu sokoni.
 
Hahahahaha mbn unasikitika Sana? au umeanza kuona dalili kuwa CDM iko thabiti
Mwaka jana kulivuja sauti ya wabunge wa Chadema Said Kubenea na Anthony Komu wakipanga njama za kumuuwa Boniface Jacob ili hatimae wafanikishe adhima yao ya kumng'oa Freeman Mbowe kwenye uenyekiti wa chama.....
 
Inavyoelekea chama tawala kinafanya kila namna ili CHADEMA iwafukuze wakina Halima. Wanafanya hivi kwa sababu wakishafukuzwa, watabaki bungeni kwa ridhaa ya chama tawala na hivyo hawatakuwa na uhuru wa kusema au kufanya wanachotaka maana chama tawala kikiamua kuwa hawana tija hawatakuwa na pa kukimbilia.

Kama CHADEMA hakitawafukuza, Chama tawala kitakuwa hakina leverage juu yao na hivyo wataweza kuendelea kujinasibu kama wapinzani. Lakini kwa namna ambavyo wameonekana kukubali kukumbatiwa na Chama Tawala baada ya kuapishwa, kama watakataa kuachia ubunge wao, hata kama Mbowe atakuwa anawaonea huruma , chama chao kitakuwa hakina jinsi ila kuwafukuza.

Watafukuzwa lakini watabaki bungeni kwa ridhaa ya Tume na Spika ila kila mtu atajua wao ni sehemu ya Chama Tawala na hivyo watakosa legitimacy hata wakijitahidi kuisimamia na kuikosoa serikali maana itajulikana kuwa ni maigizo tu maana mwisho wa siku kura zao hazina uzito.

Aidha, itawabidi wakubali kutumiwa kukichafua chama chao cha awali, kitu ambacho kitazidi kuwaharibia. Wakati huo huo wafia chama wa CCM hawatakuwa na imani nao maana watajua kuwa mwaka 2025 watawanyang'anya nafasi zao. Hii miaka mitano watavuna, wote watakuwa mawaziri vivuli, kiongozi wao atakuwa KUB lakini baada ya hapo watakuwa na wakati mgumu sana.

Ukweli mwingine ni kuwa kuna wanawake wengi wenye uwezo walikuwa wanatamani nafasi zao ndani ya chama chao lakini walishindwa kutoboa kwa jinsi walivyokuwa wamejijenga kwa jamii na uongozi wa chama. Hii ndio nafasi yao ya kuchukua nafasi hizo na hawata jivunga.

Amandla...
 
AG anazidi kuwachoresha CCM.
Wataguswa kwa barua ya kutimukiwa ili akae nao hapo bungeni kama wabunge wa mataga.
 
Maajabu ya mwaka haya. Kwa iyo amesema kifungu gani cha sheria kinakataza vyama kuwashughulikia wanachama wake??? Na amesema yeye Kama nani??? Tangu lini mwanasheria mkuu wa serikali akavisemea vyama??? Kweli Fatma Karume alikuwa sawa juu ya huyu jamaa
Hao ni wabunge halali lazima AG awalinde
 
The thing is katika taasi ya CHADEMA kuna watu wakubwa kuliko taasisi yenyewe , hiki kitu siyo rahisi kukikuta katika taasisi zinazo jielewa

Hapo kifuatacho ni kalipio kali basi (msitegemee kusikia akina halima wamefukuzwa , )

[emoji1787][emoji1787]
 
The thing is katika taasi ya CHADEMA kuna watu wakubwa kuliko taasisi yenyewe , hiki kitu siyo rahisi kukikuta katika taasisi zinazo jielewa

Hapo kifuatacho ni kalipio kali basi (msitegemee kusikia akina halima wamefukuzwa , )

[emoji1787][emoji1787]
Hakuna MTU mkubwa kuliko taasisi...
 
Mwaka jana kulivuja sauti ya wabunge wa Chadema Said Kubenea na Anthony Komu wakipanga njama za kumuuwa Boniface Jacob ili hatimae wafanikishe adhima yao ya kumng'oa Freeman Mbowe kwenye uenyekiti wa chama....
Hushangai kwamba serikali haijakanusha tuhuma nzito za CHADEMA ? Hiyo ndiyo habari kuu
 
Kwani Chadema iko juu ya sheria?

Kwani AG anawashwa washwa nini si taratibu zote za kisheria zilifuatwa namely:

1. Kamati kuu ya CDM iliwapitisha.
2. Forms zao zina baraka zote za CDM.
3. Katibu mkuu CDM aliwasilisha majina yao kwa mkurugenzi wa tume Dr. Mahera.
4. Supika akapata majina tokea tume.
5. Supika akawaapisha.
6. Nao wakaishukuru CDM na Mbowe.

Wanaitwa kuhojiwa kuhusu hayo yeye AG anawashwa washwa?

Asubirie sindano imwingie.

Itapendeza zaidi Lissu akihudhuria kikao cha kesho hata kwa voice link achilia mbali video.

Aluta continua!
 
Anayebidi aongelee hili suala kwa sasa ilibidi awe NEC lakini nao simu hawapokei wakipgiwa. Wanaona aibu hata kutoa matamko. Sasa huyu mwanasheria mkuu huo mchakato wa ndani ya CHADEMA alikuwepo mpaka apingane na Katibu wa chama!

Kweli Tanzania ina ajabu sana.
Wacha uongo mbona walitoa tamko tangu juzi tenalimo humu JF.
 
Mwaka jana kulivuja sauti ya wabunge wa Chadema Said Kubenea na Anthony Komu wakipanga njama za kumuuwa Boniface Jacob ili hatimae wafanikishe adhima yao ya kumng'oa Freeman Mbowe kwenye uenyekiti wa chama.

Baada ya sauti hizo kuvuja mara moja chama kilitangaza kikao cha dharura cha kamati kuu kuwahoji ili waweze kuchukuliwa hatua kali sana ikiwa pamoja na kufukuzwa Chadema.

Matokeo yake baada ya kikao cha kamati kuu hao wabunge wauaji walisamehewa na kutakiwa kuomba radhi tu!

Kama hali ni hiyo, wabunge wa viti maalum Chadema si wauaji na wala hawajatishia kumuuwa mtu yoyote ila wanajaribu tu kutumia haki yao ya kikatiba iweje wafukuzwe Chadema?
Kweli kuwa mwanamke Chadema ni dhambi kubwa kuliko wapanga mauaji waliosamehewa??

Tusubiri na kuona kesho kikao cha kamati kuu chadema kitaamua nini ,bila shaka Mbowe is going to be tested again na maamuzi tofauti na kufukuza yatamwimalisha ,na maamuzi ya kufukuza hao wanawake itakuwa ni kiss of death kwa Mbowe na Chadema kwa ujumla.

Wale walikubali makosa na kuomba msamaha kuwa hawatarudia tena na hao kama wanakunali makosa na kujibua ubunge watasamehewa maana chama kitakuwa hakijawa sehemu ya wizi wa kura
 
Napata shida sana kuona CCM wenzangu tuna angaika na maswala ya chadema, waacheni waumane...

AG, chadema wakifanya kikao chao na kuazimia kuwa futa uanachama ni hatua gani utachukua? Ni itakuwa dhidi ya taasisi au utachukua kwa mmoja mmoja na kuiacha taasisi salama?

Kwa CCM wenzangu kushabikia hili ina tuingiza moja kwa moja ktk swala lenyewe, hivyo ni bora waumane wao kwa wao...

Maswala yao ya Ndani tuwaachie wenyewe, ili mradi wafate sheria za nchi.

Nawasihi tuwaache wapambane na mambo yao... Mfumo dume hauta kuja kuisha kuanzia ktk familia, ktk taasisi za kiimani mpka ktk serikali

Sasa wanao pinga mfumo Dume ktk siasa wana ajenda zao

Mh. Rais wa Zanzibar Dr. Mwinyi alieleza vizuri sana ktk hotuba yake na ktk maswali na majibu

Kidumu chama cha mapinduzi...

Mfumo dume Kwani hao akina Mdee walikuwa wanaume walipo kuwa CHADEMA na sasa ndo wamekuwa wanawake. Kama kuna mfumo dume mbona wote walipewa majimbo ya kugombea. Wanaacha kuhangaika na adui wa nchi hii sasa wanahwanyika wao. Fukuza wote kesho hakuna kitu kitatokea na huyo AG hili halimuhusu anayetakiwa kusemea ni Mahela siyo yeye
 
Back
Top Bottom