Mwanasheria Mkuu: Wabunge wa CHADEMA wa Viti Maalumu waliapishwa kwa mujibu wa Sheria na Katiba, CHADEMA isiwaguse

Kumbe zile sheria kandamizi na zenye vioja zilizotungwa kabla ya Bunge lililopita kuvunjwa, zilikuwa na lengo la kuwapa viongozi dhalimu wawe na kinga za kutokushtakiwa kutokana na madudu ambayo wataelekezwa kuyatekeleza.

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
 
Pamoja na kuwepo kwa umoja wa wanawake ktk karibu kila chama lakini haujaweza kuondoa mfumo dume ktk hizi taasisi...

Hakuna umoja wa wanaume na wanaume ni wachache lakini ndio kama wenye maamuzi...

CHADEMA umaneni, mpeni mitano mingine Mbowe hata akikaa milele kama Prof. Lipumba, Mbatia, Mrema, Cheyo Momose ni Sawa si katiba itakuwa ina ruhusu na wanachama watakuwa wameamua iwe hivyo
 
AG amejuaje nini CHADEMA watawafanya hao watuhumiwa mpaka atoe tamko leo!? vipi je wasipowafanya lolote. Aiseee akili za kutumwa changanya zako..Hivi huyu ni Prof. Kweli?
 
Nawapongeza sana hawa wakina Mama,

Hongereni CHADEMA kwa kuwaruhusu kwenda kuapa,

Hongereni Watanzania kwa kuendelea kuenzi amani na umoja waliotuachia waasisi wa Taifa hili.

Mama TANZANIA ni wajibu wetu kumtunza kwa kuenzi AMANI NA UMOJA.
 
Wawafukuze tupate kujua undani wa sakata la "kura feki"! So far wanaongea wao tu, pengine kuanzia kesho tutawasikia na kina Mdee...
 
AG anahusika Vipi na maamuzi ya CDM?.
Kusifu Na Kuabudu
Maombi Na Maombezi

Wanamfurahisha Yule, Nikikumbusha Form Ya Kugombea Nafasi Ya Ubunge Jimbo La Ubungo
Ulijaa Ujanjaujanja Tu,DED Anakuwa Snitch Baadaye Kaumbuka
Acha Tuone Hili
 
Umeshasema mwaka juzi
 
Huyo siyo Mwanasheria mkuu ni mwanamatakwa ya CCM
 
Je, SOPHIA SIMBA hakuapishwa 2015 kwa mujibu wa katiba na sheria? AG tueleze.
 
Hii inaitwa "kutishiana nyau."

Mtu kufukuzwa chama kumeanza leo?

Ama kweli pori hili la sasa wameingia nyani wapya!

Kama hawa unaowaongelea ni wanachama wa CDM basi na mtege masikio. Kwani ni mbali basi:

Kesho Ijumaa mtanange unaanza saa mbili juu ya alama!
 
Hivi wa hayo yanayoendelea bado kuna mtu na akili zake timamu anashabikia siasa?
Kama wapo basi wakapimwe akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…