PreGE2025 Mwanasheria wa CHADEMA: Tume ilikosea kusema CHADEMA haina haki ya kushiriki kwenye Uchaguzi. Kailima ajitokeze hadharani kufuta kauli yake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu,

Akiwa anazungumza leo kwenye wa waandishi wa habari, Rugemaliza Nshala amekemea kauli ya Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhan Kailima kuhusu CHADEMA kukosa sifa za kushiriki Uchaguzi.

Ikumbukwe kuwa siku chache zilizopita Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Ramadhan Kailima alisema kuwa CHADEMA kwa kuwa hakikusaini kanuni za maadili basi kilipoteza sifa ya kushiriki kwenye uchaguzi.

Soma pia: Mkurugenzi wa Uchaguzi INEC: CHADEMA hawakuwalisha maoni, hatuna taarifa rasmi ya kususia kwao

Leo, Nshala alisema kuwa kauli hiyo ni potoshi na propaganda chafu na kwamba Mkurugenzi huyo anatakiwa ajitokeze hadharani aombe radhi kwa kauli hiyo

"Alichokifanya Kailima kwa niaba ya ile inayojiita tume huru ya Uchaguzi ni upotoshaji wa hali ya juu wa kanuni zenyewe walizosema wamesaini na kwa mujibu wa wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sifa za vyama kugombea na kushiriki zimeainishwa na Katiba na kutosaini kanuni za maadili si sababu ya kupoka hazi za vyama kushiriki. Tuliona ni propaganda mbaya lakini bahati mbaya ilifanywa na tume"

"Kile ambacho kimefanywa na Kailima ilikuwa ni propaganda chafu na kama dhamira zao bado zi hai na kama akili zao zinafanya kazi, wafute hilo tamko. Kailima amekosea na kama alivyonukuliwa kwenye vyombo vya habari kwamba CHADEMA haina haki ya kushiriki, madhali amesema hayo, afute kauli hiyo"

CHADEMA hamshiriki uchaguzi kelele za nini sasa? Wanaoshiriki wamekubali

CHADEMA kinawawasha nini?
 
Hi

Huyo lofa si aende mahakamani
 
Kichekesho hasa.CHADEMA wamesema hawagombei sasa chochote kinachohusu huo uchaguzi kiwe sawa kisiwe sawa kwa wanaoshiriki it is non of his business
Acha upotoshaji wa kijinga, cdm hawajasema hawagombei, wamesema hawashiriki bila mabadiko kwenye mfumo wa uchaguzi, na NRNE. Na mabadiliko sio kwa ajili ya cdm, bali mfumo wote wa uchaguzi.
 
Hiki chama kina watu wa ajabu sana!..

Yaani mkatae kushiriki uchaguzi wenyewe halafu wanaotaka mnataka kuzuia wasishiriki.

Hapo tume ina makosa gani si wamefanya mnachotaka.
 
CHADEMA hamshiriki uchaguzi kelele za nini sasa? Wanaoshiriki wamekubali

CHADEMA kinawawasha nini?
Kichwani upo sawasawa?

Kisheria na kikatiba, mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi hana mamlaka ya kukiondoa chama kwenye kushiriki uchaguzi. Chama cha siasa ndiyo chenye uwezo wa kutamka kutoshiriki, kama kinaona hakuna haja.

Huyu mkurugenzi yumkini ni bwege ambaye akili na elimu yake amevifanya kuwa watumwa wa tumbo lake.
 
Hiki chama kina watu wa ajabu sana!..

Yaani mkatae kushiriki uchaguzi wenyewe halafu wanaotaka mnataka kuzuia wasishiriki.

Hapo tume ina makosa gani si wamefanya mnachotaka.
Ubongo wako haufanyi kazi?? ni kama umepigwa shoti.

Unajua chadema wangesema wanataka reforms kwanza ndipo UCHAGUZI ufanyike kipi hujakielewa ? Ni either mama Samia akubali reforms muda still upo.

Ukiendelea kushupaza shingo ni sawa na kujipiga kidole / kujikuna sehemu za Siri na kunusa vidole vyako.
 
Kichwani upo sawasawa?

Kisheria na kikatiba, mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi hana mamlaka ya kukiondoa chama kwenye kushiriki uchaguzi. Chama cha siasa ndiyo chenye uwezo wa kutamka kutoshiriki, kama kinaona hakuna haja.
CHADEMA wametamka hawadhiriki wao wenyewe kwa taratibu zilizopo

Wenzao wamekubali

Sasa huyo mwabasheria anataka nini?
 
Aise! Kwahiyo tume inatakiwa kufata sheria tu ,chadema iwapo watashiriki
CHADEMA hawajateuliwa au kupigiwa kura na vyama vingine kuwa msemaji wao au mtetezi wao

Wao wamekubali

CHADEMA ipambane na hali yake
 
Kichekesho hasa.CHADEMA wamesema hawagombei sasa chochote kinachohusu huo uchaguzi kiwe sawa kisiwe sawa kwa wanaoshiriki it is non of his business
Hivi kumbe CHADEMA wamesema hawashiriki uchaguzi au mi ndio sielewi?? Bila kutumia jicho la CCM tujaribu kuelewa watanzania wengine wanasema nini, hawa wanasema bila mabadiliko ya sheria na taratibu za uchaguzi basi hakuna uchaguzi yaani ni Sawa na kazi bure, na wametoa ufafanuzi kuwa watashawishi watu wauzuie uchaguzi usifanyike. Yaani ukisema Kwa mfano, "sitaoa Hadi nijenge nyumba" je unamaanisha hutaoa??
 
watu wa upande ule wanataka kupambana na mtu wa Havard wakati Elimu yao ni ile ya hapa na pale pangu pakavu tia mchuzi, father dead mother dead now job- sijui watamuelewaje huyu mtu huyu wa Havard?
 
Back
Top Bottom