Wakuu,
Akiwa anazungumza leo kwenye wa waandishi wa habari, Rugemaliza Nshala amekemea kauli ya Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhan Kailima kuhusu CHADEMA kukosa sifa za kushiriki Uchaguzi.
Ikumbukwe kuwa siku chache zilizopita Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Ramadhan Kailima alisema kuwa CHADEMA kwa kuwa hakikusaini kanuni za maadili basi kilipoteza sifa ya kushiriki kwenye uchaguzi.
Soma pia:
Mkurugenzi wa Uchaguzi INEC: CHADEMA hawakuwalisha maoni, hatuna taarifa rasmi ya kususia kwao
Leo, Nshala alisema kuwa kauli hiyo ni potoshi na propaganda chafu na kwamba Mkurugenzi huyo anatakiwa ajitokeze hadharani aombe radhi kwa kauli hiyo
"Alichokifanya Kailima kwa niaba ya ile inayojiita tume huru ya Uchaguzi ni upotoshaji wa hali ya juu wa kanuni zenyewe walizosema wamesaini na kwa mujibu wa wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sifa za vyama kugombea na kushiriki zimeainishwa na Katiba na kutosaini kanuni za maadili si sababu ya kupoka hazi za vyama kushiriki. Tuliona ni propaganda mbaya lakini bahati mbaya ilifanywa na tume"
"Kile ambacho kimefanywa na Kailima ilikuwa ni propaganda chafu na kama dhamira zao bado zi hai na kama akili zao zinafanya kazi, wafute hilo tamko. Kailima amekosea na kama alivyonukuliwa kwenye vyombo vya habari kwamba CHADEMA haina haki ya kushiriki, madhali amesema hayo, afute kauli hiyo"