YEHODAYA unaandika vitu vingi sana vya uongo. Kwanza ukisema kwamba wanyasa walikuwa waanglikana ndiyo maana Mwingereza aliwasomesha unaongopa. Unawezaje kutenganisha kuja kwa waingereza na uanglikana?
Kila siku huwa tunasema kuwa CCM inapalilia ubaguzi huwa mnabisha. Sasa unaposema kwamba kuna kabila linampinga Magufuli huoni kwamba unasema uongo. Leo kila mkoa kuna watu ambao wanampinga Magufuli, inakuwaje wewe uone kwamba kuna kabila mahsusi kazi yake ni kumpinga Magufuli?
Halafu kujenga picha ya uongo kwamba wanyasa walikuwa wengi Serikalini na walikuwa wasomi kuliko wachaga ama Wahaya ni jambo baya sana. Usiseme mambo ya ovyo kwa kuwa tu umejificha nyuma ya jina bandia. Unajua shule za kwanza kujengwa Kagera ama Kilimanjaro zilijengwa hata Nyerere hajawazia kuomba Uhuru wa Tanganyika. Hizo shule walikuwa wanasoma hao wanyasa wako?
Yaani unaongea maneno yenye maudhui yanayofanana kabisa na yale ya Interehamwe ambao walianza kuwaita wenzao "mende" mwisho wa siku wakaanza kuwaua. Kama wachaga na Wahaya ni wabaya kiasi hicho ni kwa nini CCM ina wanachama wake huko?
Kuwaita Lissu na Mbowe ni vibaraka wa wazungu unajifurhaisha tu. Serikali hii na nyingi za Afrika bila hao wazungu kuwepo zisingekuwa hivi zilivyo. Leo kama Afrika ingekuwa inajitawala bila ya hao wazungu sijui ingekuwaje. Fikiria pamoja na Makelele ya wazungu lakini watawala wa Afrika wanaua, wanakamata wapinzani wao, wanafuja mali za Umma, wanaupendeleo wa kidini, kikabila, hata kiukoo.