TANZIA Mwanasiasa mkongwe, Mzee John Lifa Chipaka Afariki Dunia

Kweli marehemu alijitahidi sana kupambana kisiasa. Apumzike kwa amani.
 
Pumzika kwa Amani Babu yangu John Lifa Chipaka.

Mwanaharakati mpaka mauti yalipomfika.

Nilipata shiriki kwenye kikao cha moja ya Asasi za kiraia huyu mzee alikuwa hajifichi kujiita Mfungwa Huru
 
R.I.P

zaidi ya miaka 50 iliyopita Nyerere aliwakamata akina Lifa Chipaka kwa kuwa tu walikuwa washindani wake kisiasa,zaidi ya miaka 50 iliyopita Nyerere aliwafunga watu hawa bila hata kuwa na sheria!
Imagine unashinda kesi dhidi ya Nyerere halafu unaambiwa sasa hivi uraiani kuna kipindupindu na vita vya Kagera kwa hiyo huwezi kufunguliwa, unasota miaka mingine kadhaa unasubiri kipindupindu kiishe!

Tuliimbishwa mashuleni kwamba hawa ni maadui wa nchi. Kisa: John Chipaka kamuuliza Nyerere, mzee kwa nini umewapa ubunge na uwaziri Muingereza Bryceson na Mhindi-Mkanada Jamal? Nyerere akawa hana jibu, akaona kadhalilishwa na kijana mdogo.

Bryceson baadae alirudi kwao Uingereza, Jamal alienda kufia Canada. John Chipaka was right, hawa walikuwa foreign visitors, kwa nini uwape uwaziri?

Baba wa Taifa ametutoa mbali lakini udikteta wake ulikuwa ujahili mtupu. Nyerere ni sawa na mjomba aliyekusomesha lakini akaku molest.
 
Apumzike kwa amani.
Tulimwimba sana kwenye zile nyimbo za kumkashifu Kambona miaka hiyo tukiwa shule ya msingi, kama huu hapa (ubeti wa mwisho):
"Kwanza tunawahesabu
Waliokufa kwa tabu
Bila hata matibabu
Wengi hawana hesabu
Waliokufa kwa tabu
duniani.

Mwana Lumumba wa Kongo
Walimpiga vigongo
Wakavunja mgongo
Wakamtoa ubongo
na wala sio uongo
ni kweli.

Tom Mboya wa Kenya
Si kiongozi mbaya
kala risasi ya faya
Maharamia wabaya
wala hawaoni haya
kumuua.

Kambona aliagiza
Chipaka na Kamaliza
Pindueni mkiweza
Nitawapeni mapesa
Nikitoka safarini
Uingereza"

Ndiposa muelewe kuwa na mimi pia ni mhenga!
 
Kweli umenikumbusha mbali, naikumbuka sana hiyo idhaa ya kiswahili ya radio ya makaburu, ilikuwa inaitwa "Radio RSA". Mtangazaji maarufu alikuwa Duncan Mkandawire, sijui yuko wapi siku hizi.
 
Hii habari inanifanya niwe na shaka na ukweli wa habari yako nzima. Hili jambo sio kweli.
Unasema siyo kweli? Tuulize sisi wahenga. Baba yangu aliokota mojawapo ya vipeperushi hivyo akakificha kwenye koti maana polisi walizingira eneo zima wakavikusanya na kuvichoma. Watu wachache sana walifanikiwa kuokota. Baba akaja nacho nyumbani akakisoma halafu akakificha sana kwa miaka mingi. Mimi alikuja kunionyesha hicho kipeperushi mwaka 1985 Nyerere alipostaafu, na bado akaniasa nikifiche. Ninacho hadi leo kwenye nyumba yetu ya kijijini. Kipeperushi hicho kinatoa wito kwa jeshi kumpindua Nyerere, na wananchi wanahimizwa kuyakubali mapinduzi hayo kwani ni kwa faida yao. Pia kina picha ya Nyerere ameshika kichwa kwa mikono yote miwili, ikiwa na caption kwa herufi kubwa inayosema "Naomba msaada mambo yamenizidi kimo". Nikipata fursa nita-scan niwawekee hapa.
 
Kweli umenikumbusha mbali, naikumbuka sana hiyo idhaa ya kiswahili ya radio ya makaburu, ilikuwa inaitwa "Radio RSA". Mtangazaji maarufu alikuwa Dunstan Mkandawire, sijui yuko wapi siku hizi.
Kwanza nashukuru kwa kutuletea ule wimbo ambao wengine wetu tuliuimba sana kwa msisimko.

Kwetu Tanzania kulikuwa na ilie idhaa ya nje maarufu kama "External Services" ambayo kazi yake hasa ilikuwa ni kupiga Propaganda dhidi ya Makaburu wa Afrika ya Kusini. Na ni kwenye Idhaa hiyo ndiko mtu uliweza kupata bahati ya kuzisikia nyimbo za Ulaya na Amerika.

Na minara yake ya kurushia Matangazo ilikuwa pale mabibo palipojengwa "EPZ" na ndiyo maana eneo lile linaitwa "External" mpaka sasa. Kuna ule msemo maarufu sana usemao "Mafahali wawili wakigombana ziumiazo nyasi." ugomvi wa Mwalimu na Kamuzu Banda ulileta sintofahamu kubwa sana kwenye maeneo ya mikoa ya huko.
 
RIP Chipaka
 
acha uchochezi,wachaga wamekufanya nini mkuu
 
Hakika kabisa
 
Hawa wanasiasa wakongwe wameisaidia nn nchi katika kuleta usawa!?
Maana wanaona yanayotendeka wanakaa kimya af wakifa mnataka tuomboleze[emoji16][emoji16]
 
Exactly mkuu .Hayo makaratasi ilikuwa ukiokota ukakutwa nayo ungeozea jela. Sasa hivi miaka imepita weka tu ukipata nafasi Hakuna tatizo. Hongera kwa Mzee wako na wewe kwa kutunza kumbukumbu ya historia.
 
Kwa heri Mzee Chipaka

Siasa zenu zilimtisha Nyerere mpaka akakimbilia kufuta Vyama vya Upinzani 1965
 
Kwa heri Mzee Chipaka

Siasa zenu zilimtisha Nyerere mpaka akakimbilia kufuta Vyama vya Upinzani 1965
Hakufuta Nyerere bunge ndio lilifuta yeye alisaini kilichoindhinishwa na bunge
 
Kweli umenikumbusha mbali, naikumbuka sana hiyo idhaa ya kiswahili ya radio ya makaburu, ilikuwa inaitwa "Radio RSA". Mtangazaji maarufu alikuwa Dunstan Mkandawire, sijui yuko wapi siku hizi.
Kabla Ya vipindi vya Radio RSA idhaa Ya kiswahili kuanza unakumbuka kuna mlio wa ngoma ulikuwa unaanza ukipiga ndu ndu ndu ndu ndu halafu unafuatiliwa na milio ya ndege walio imba churuu churuuu churuuu. Kile kilikuwa kiapo cha siri cha makaburu chenye maana ya kusema kuwa sikieni makaburu tulipofika afrika kusini tulikuta ndege tu sio watu hivyo pale Afrika kusini ni kwetu na ndege tu
 
Hakufuta Nyerere bunge ndio lilifuta yeye alisaini kilichoindhinishwa na bunge

Mswada wa Kufuta haukuletwa na Bunge ukiletwa na Serikali ya Nyerere kazi ya Bunge ikawa kupitisha Pendekezo la Serikal

Tanzania haijawahi ma haitawahi kutawaliwa na Dikteta Kama Nyerere!

Unamkamata Mtu 1968 inafika 1970 unagundua huna Sheria ya kumfungia unatunga Sheria then una back date isomeke ilianza kutumika 1968 unamfunga Mtu Maisha Halafu unajiandaa kutunga Sheria kuzuia Watu wasikate Rufaa kwny Mahakama ya EA lakin Watuhumiwa wanawahi kukata Rufaa na wanashinda rufaa lakin unatekeleza Rufaa hiyo kwa kuwaachia huru Gerezani baada ya Miaka 10 baadae!

JPM ni cha Mtoto kwa Nyerere
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…