Mwanaume akikataa mimba au kukutelekezea mtoto, usitumie majina yake Kwa mtoto wako



Ndio maana nikasema, ikiwa itatokea hivyo Sisi wanaume tukubali lawama tuu
 
Yani mfano, Baba kipato kimepiga Chenga, basi mama mtoto abadili ubini wa mtoto?! Akili za wapi hizi?

Nchi hii na Taifa hili vinazidi kuwa vya hovyo kila sekunde!

Ee mwenyezi Mungu uturehemu.[emoji120]
Anezungumzia kuhusu kukwepa uja uzito
 
Upo sahihi ,kesho na kesho kutwa mtoto akifanikiwa pasiwe na usumbufu
 
Kwanza kwa nini ukatae au kutelekeza mtoto...
 
Tujue jinsia yako kwanza isije kua ni kaka unatumia mkorogo umeamua kuja kumsemea dada yako
 
Leo siungi mkono hoja, unapaswa kujua kuwa hata kama baba kakataa mtoto lakini haitaondoa ukweli kuwa huyo ni mtoto wake na anapaswa kufahamika kwa ubini wa baba yake.
 
Tatizo unakuta mtoto anapewa wababa watatu aisee kuna wanawake wabaya jamani ?!
 
usikute unayetoa mawazo hayo hata mke huna...!
 
Mtoto ni matokeo ya baba kuwa na mchango wa 50% na mama 50%.

Baba kutohusika na malezi haifuti na haibadirisha sifa ya kutokuwa mtoto wake. kubadilisha majina ya mtoto, ni njia ya mzazi kujidanganya na kujifariji.

JE KWA NINI BABA AKATAE/ATELEKEZE MTOTO?KWANINI ASHINDWE KUCHANGIA MATUNZO YA MTOTO WAKE?
 
Simple tumia jina la ukoo wa baba yake usitumie la baba yake
 
Kuna mmoja alijaribu kunifanyia sarakasi ya hivi.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Katika dhambi sitaki kuifanya ni kumbambikizia mwanaume mtoto asie wa kwake,, amtelekeze, awe kapuku ama mfu mtoto wangu sitamficha Nani Ni baba yake halali, na atatumia ubin wa baba yake no matter what!

Kuwa mama sio kubeba mimba na kunyonyesha tu Ni pamoja na kubeba aibu ya matukano kutoka kwa walimwengu km single maza, Malaya nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…