Mwanaume ambaye hana pesa asioe

Mwanaume ambaye hana pesa asioe

Kula tano chali 👊

Tunavolalamika kuwa wanawake mnapenda sana pesa, sio kwamba sisi wanaume hatutaki kuwapa wanawake wetu pesa, au tunataka kukimbia majukumu. Tunapenda sana kuwapa hela.

Ishu ni kwamba kibinadamu, mwanaume ukijua mwanamke uliye naye yuko na wewe kwenye mahusiano kwasababu una pesa, na sio kwasababu kakupenda/ kavutiwa na wewe, kiukweli roho inauma, mtu unahisi kama unatumika.

Na wanawake wengi sahivi hawampendi mwanaume, ila wanapenda hela za mwanaume, sasa hapo kutakuwa kuna mahusiano kweli, hapo wanaume tutaacha kulalamika kweli.

Mfano rahisi jiulize siku ukigundua kuwa mumeo aliekuoa hakuwahi kukupenda wala kuvutiwa na wewe, ila alikuoa sababu una pesa, imagine utajihisi vipi Lamomy Jadda
 
Hitimisho hapo muoe na mtimize majukumu yenu km wanaume na baba wa familia
Sasa wewe ndio umeongea point mamyy😘😘😘😘.
In short kutimiza majukumu ndio jambo la msingi.
Uishi kivyako ama kwa wazee ila mambo matatu ni muhimu;
1)Majukumu binafsi ya mwanamke kutimizwa ipasavyo.
2)Uhuru wa mwanamke kuwepo itakikanavyo.
3)Amani iwepo pale muishipo(hususan kwa sisi wakaa nyumbani).

Hata wewe mamy kwa mfano katokea shemela kwao wamezaliwa watatu wa kwanza yeye na mtoto wa kiume pekee ana kazi,anaishi na wazazi nyumba ambayo ina nafasi kiasi ukimka unaweza usikutane na mama/baba mkwe,wakwe wamekupenda.
Je wewe hutoridhia kuolewa naye!?
 
Ukomavu wa AKILI na HISIA ndo vigezo muhimu vya MTU kuoa au kuishi na mke pamoja na familia.

Kuna watu hasa kwenye ndoa walikuwa wanaishi vizuri Ila kipato kilipoongezeka mwanaume anabadilika anakuwa MTU wa wanawake kila kona na Amani inapotea.


Ikiwa umekomaa kiakili na kihisia waweza kuoa ,haijalishi mtapitia nini Ila mtaweza kuishi kwa Amani.
 
Back
Top Bottom