Mwanaume ambaye hana pesa asioe

Mwanaume ambaye hana pesa asioe

Nimeona wanaume wengi kwenye mitandao ya kijamii wakilalamika jinsi wanawake wa siku hizi wanavyopenda pesa, ukiwachunguza hao walalamikaji utagundua hawana hela Ila wanatamani kuoa. Hivi umewahi kuchunguza - ni katika tamaduni gani mwanaume asiye na kitu alipewa mke?

Kwa maoni yangu binafsi, haijalishi una mali kiasi gani. Ikiwa mwanaume unamudu kulipia nyumba hata ya chumba kimoja - na unaweza kujilisha - basi unaweza kumtunza mke...... na mtakuwa pamoja, oa.

Lakini ikiwa unaishi kwa kula chakula kutoka katika sifuria ya mama yako na unalala ndani ya chumba chako cha tangu utotoni nyumbani kwa mama yako, ni dhahiri haupo tayari kwa ndoa usithubutu kuoa.

Bili hazilipwi kwa busu - bili hulipwa kwa pesa tasilimu. Hama kwa mama yako uende ukatafute hela kwa jasho lako ukisha pata hela oa na uishi na mkeo kwako na sio kwa mama yako.

Pesa hujibu mambo yote (Mhubiri 10:19)

Ubarikiwe.
Yaani wewe akili zako unazijua mwenyewe. Pesa ni kama maua kuna wakati yanachanua na kuna wakati yananyauka so unataka kuniambia siku pesa zikikuishia ukafilisika itabidi umwache mkeo?
 
kuna siku hapa nilikuwa napitia uzi fulani, naona mlikuwa manongelea mijengo ya akina samia, 😂😂😂 huko mbweni, na wewe ulikua mbele kutoa coments, nikaona doh basi unapajua, sasa unipe ka experience viwanja bei zinaanziaje😂😂, wapi pakishua zaidi
Haha kwanini Umeniuliza hilo swali mkuu 😀😀
 
kuna siku hapa nilikuwa napitia uzi fulani, naona mlikuwa manongelea mijengo ya akina samia, 😂😂😂 huko mbweni, na wewe ulikua mbele kutoa coments, nikaona doh basi unapajua, sasa unipe ka experience viwanja bei zinaanziaje😂😂, wapi pakishua zaidi
Hahaha kote kuzuri tu ila Mbweni kuzuri zaidi kuliko Goba si unajua tena baharini ni baharini tu, bei inategemea na ukubwa wa eneo ila kwa nilivyosikia Uswahilini vinaanzia 30M na kuendelea, mitaa ya Ushuani ndio kuna hadi vya 500M na kuendelea huko
 
M500🫢, sas huko jumba c inabid liwe la bilioni sasa dah, mfnykz serkalin hela hizo anatoa wapi, nahisi hapo kuna watu wanamilk viwanda na malampuni mkuu, anyway ngj tujipige pige pesa.
 
Hiyo mitaa ukinunua huruhusiwi kujenga nyumba ya chini ni ghorofa tu kama huwezi uza, wanaoishi hiyo mitaa wengi ni viongozi wa serikali na wafanyabiashara wakubwa, hii nchi usiulize eti mfanyakazi wa serikali anatoa wapi hizo pesa watu wanapiga mkuu
 
Pesa hujibu mambo yote lakini tukumbuke unaweza kuoa ukiwa na pesa lakinj pesa ikaja kuisha ukiwa na mke ndo ukaanza upya kuitafuta , hapa point yako ni hii OA ukiwa umeshajipanga kimaisha.
 
Ukiweza na uwezo wa kulipia pango hata chumba kimoja na uwezo wa kujilisha kila siku unao, OA, pesa ikiisha huku unaishi pamoja na mkeo mtapambana kuirudisha maadam mliapa kuishi pamoja katika shida na raha.
 
Nimeona wanaume wengi kwenye mitandao ya kijamii wakilalamika jinsi wanawake wa siku hizi wanavyopenda pesa, ukiwachunguza hao walalamikaji utagundua hawana hela Ila wanatamani kuoa. Hivi umewahi kuchunguza - ni katika tamaduni gani mwanaume asiye na kitu alipewa mke?

Kwa maoni yangu binafsi, haijalishi una mali kiasi gani. Ikiwa mwanaume unamudu kulipia nyumba hata ya chumba kimoja - na unaweza kujilisha - basi unaweza kumtunza mke...... na mtakuwa pamoja, oa.

Lakini ikiwa unaishi kwa kula chakula kutoka katika sifuria ya mama yako na unalala ndani ya chumba chako cha tangu utotoni nyumbani kwa mama yako, ni dhahiri haupo tayari kwa ndoa usithubutu kuoa.

Bili hazilipwi kwa busu - bili hulipwa kwa pesa tasilimu. Hama kwa mama yako uende ukatafute hela kwa jasho lako ukisha pata hela oa na uishi na mkeo kwako na sio kwa mama yako.

Pesa hujibu mambo yote (Mhubiri 10:19)

Ubarikiwe.
Wamekusikia mkuu
 
Kauli sahihi ni kuoana,maanake muunganiko hivyo kwa kauli nyingine mwanaume anamuoa binti na binti anamuoa kijana....kutengeneza neno kuoana,,,,,wazungu wanasema marry,....
Kuoa/Kuolewa =kuoana

Mwanaume anaoa.

Mwanamke anaolewa.

Bado kiswahili ni kigumu kwako?
 
Back
Top Bottom