Wewe je? Umeweza
Hili si la leo. Enzi hizo kabla ya Uhuru, Mwanaume alikuwa akioa wake wengi ili apate watoto wengi. Alitegemea hao watoto na wanawake wawe ndiyo Wafanyakazi katika mashamba yake, watunze Mifugo yake etc. Maana halisi ya kuwa na wake wengi ilikuwa kupata watoto wengi ili apate cheap labour.
Hii ilisababisha ongezeko la watu. Njia ya kupunguza ongezeko la watu (population); serikali ikaanzisha pamoja na mikakati mingine, njia ya kupunguza vizazi ikiwa ni pamoja na ulazima wa kumpeleka mtoto shule. Hii si kwamba serikali ilitaka watu wasome! La hasha lengo la serikali lilikuwa ni kumfanya mzazi aone burden ya kuwa na watoto wengi ambao hawana faida kiuchumi. Kwani unazaa mtoto na anapokuwa anahitajika kwenda shule na si kuingia shambani akalima mashamba yako.
Hili Lilifanya wazazi kupunguza idadi ya watoto maana ukizaa wengi unakuwa mtumwa wao.
Kwa sasa wimbi la vijana wa JF waliobadili kibao kwa wazazi, ati wahakikishe wanamtunza mtoto hadi wazazi wafe, hii itasababisha kataa ndoa wawe washindi kwani ukioa, utazaa mtoto na huyo Mtoto atakuwa liability kwako hadi uingie kaburini. Sasa kwanini uingie katika mdomo wa mamba ukiwa na akili zako. Wakati machangu wa kuondoa uhanga wapo kibao mitaani. Na hapo utabakisha chenji ya kuweka akiba ya uzeeni.
Hivi vitu ni muhimu kwa nyie ma Azaboys kuyajua pia.