Mwanaume andaa future nzuri kwa wanao, ila usitegemee lolote kwa wanao

Huyu anatafuta karo ya mtoto wake
Halafu litoto la JF ati likifanikiwa mbeleni linadai kwanini hakujiwekea akiba ya uzeeni
View attachment 2880074

Mingi ya mitoto inayosupport huu Upuuzi ni ya single mother
Una uwezo mdogo sana wa kuchanganua mambo

Ukiona mtu wa umri wa kama huyo umeweka picha yake bado anatafuta ada ya mtoto ujue alipokuwa kijana alikuwa mjinga kabisa
 
Mwanaume tafuta pesa kwa bidii, wape watoto elimu bora, wape mahitaji yao muhimu, jenga nyumba nzuri waishi vizuri, lakini ukizeeka usitegemee lolote kutoka kwa wanao.

Enjoy maisha ya uzee kwa pesa zako mwenyewe ulizochuma ujanani.
Kwann tunawaogopa sana wake zetu siku hizi bro ?
 
Akili za kitoto! We are all investors. Tunapanda ili baadaye tuvune. Kama huwezi kuvuna, yanini kupoteza fedha? Hizo pesa ambazo ulitakiwa kuenjoy uzeeni ndizo unatumia kuinvest kwa mtoto. Acheni akili za kijinga
Waliyaona haya wenzio.
Usije TU toa laana kwa watoto
 
Kwa vile watu weusi wanaacha kutumia akili baada ya kustaafu...Ndio maana wanazaa mapema eti wasomeshe mpaka miaka 60 wawe wamemaliza kila kitu ,kifuatacho kuanza kutegemea Watoto...

Tunajilimit eti miaka 60 mtu akuwa hopeless na maisha anakuwa tegemezi kutupia lawama watoto,kuna mzee hapa naona anastaafu mwaka huu ila mpaka hivi sasa ana mikopo ana watoto kama 6 ...Kujenga naona anangojea kustaafu huyu lazima alete tabu halafu kachoka sana..

Mbona nje wazee kibao wapo 80's wapo fresh !? Huku mtu miaka 60 basi kama mzee wa miaka 100...Tatizo ni pesa ukiwa na pesa fresh wakina mzee kikwte wapo 70 hata mpira wanacheza.
 
Ulaya waliandaa mifumo ya kupita tangu unazaliwa Hadi kifo upite wapi thus wao miaka 18 tayari unajitegemea.
Sisi hadi 40 upo home
 
Kutegemea watoto wakusaidie sio uwekezaji mzuri ni bahati nasibu.
Kizazi Cha Sasa angalau uwe na apartment,mashamba au viwanja utaheshimika uzeeni.
 
Mwanaume tafuta pesa kwa bidii, wape watoto elimu bora, wape mahitaji yao muhimu, jenga nyumba nzuri waishi vizuri, lakini ukizeeka usitegemee lolote kutoka kwa wanao.

Enjoy maisha ya uzee kwa pesa zako mwenyewe ulizochuma ujanani.
Mnavyoongea utasema jambo raisi lkn frsh
 
Akili za kitoto! We are all investors. Tunapanda ili baadaye tuvune. Kama huwezi kuvuna, yanini kupoteza fedha? Hizo pesa ambazo ulitakiwa kuenjoy uzeeni ndizo unatumia kuinvest kwa mtoto. Acheni akili za kijinga
Mjinga apa ni wewe
 
Mtoa uzi upewe maua ila hali inakuwa mbaya zaidi kwa hawa watoto wa kiume
 
Kwanini watu wanataka wakizeeka watoto wawasaidie? Kama unataka hela si ungefanya biashara hiyo miaka yote unalea?

Hamna sababu za msingi zaidi za kutaka watoto?
Sifahamu una umri gani, lakini naamini una wazazi.

Mzazi wako akiwa na shida si jukumu lako kumsaidia hata kabla hajakuomba?!

Fadhila zako kwa wazazi kukulea na kusomesha; (pengine kukutafutia ajira) hadi hapo ulipofikia ni zipi?
 
Fadhila zako kwa wazazi kukulea na kusomesha; (pengine kukutafutia ajira) hadi hapo ulipofikia ni zipi?
Shukrani

Kuwasaidia kifedha ni mpaka iwe lazima, haifai mzazi kumtegemea mtoto, hapo ukute mtoto ana familia yake na yeye
 
Una maana gani kumsaidia kifedha ni mpaka iwe lazima?
Ni msaada gani mwingine utakuwa unampa?
Namaanisha yeye tayari anatakiwa anajitegemea, mimi kumsaidia iwe ni pale anapokwama basi

Misaada mingine itatolewa tu, hii mada inazungumzia pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…