Mwanaume hakutakiwa kuteseka kisa mapenzi, kutokujitambua na upumbavu ndio kunawafanya kuwa hivyo

Mwanaume hakutakiwa kuteseka kisa mapenzi, kutokujitambua na upumbavu ndio kunawafanya kuwa hivyo

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Posts
35,812
Reaction score
107,628
By default wanadamu tulipoumbwa kila jinsia ilipewa majukumu yake, jukumu la viumbe wenye jinsia ya kiume (wanaume) wameumbwa kutawala jinisia ya kike (kike) katika kila Nyanja na jinsia ya kike imeumbwa kutawaliwa na jinisa me.

Sio maneno yangu bali ni maneno ya vitabu vyote vya dini Quran na bible pia science/psychology inakubaliana na hilo, mwanaume anajiona mkamilifu zaidi pale anapoweza kumtawala (sio kimabavu), kumuongoza na kumuhudumia mwanamke na mwanamke anajisikia amani na usalama zaidi anapopata mwanaume anayeweza kusimamia misingi ya uanaume wake yaani kutawala, kuongoza na kuhudumia .

Ikitokea jinsia moja imeenda kinyume na mfumo huo wa asili chaos must happen, labda mwanamke anapesa zake na maisha mazuri anataka afanye vile vitu anavyotakiwa kufanya mwanaume ajili ya kiburi cha pesa zake lazima mwanaume huyo kama anajitambua apinge (rebel) ajabu sasa mwanaume akiamua kuvumilia huyo mwanamke ajili ya pesa alizonazo mwanamke huyo atamdharau na kumuona fala sababu ameshindwa kusimama katika misingi ya kiume mahusiano hayo hayatadumu,that’s nature bwana.

Mwanaume umepewa dhamana kubwa duniani haijalishi mwanamke ana mapembe, mabawa, mkia, miiba au ana umri mkubwa na cheo zaidi yako bado atabaki kua mwanamke mtu na kanuni ni ileile atabaki kua chini yako daima, vijana wa sasa sijui mnafeli wapi aisee yaani mnadhalilisha jinisa na mamlaka yenu mbele ya wanawake.

Mwaume unayejielewa haiwezekani unalia, unashindwa kulia kisa mwanamke wako kakuzingua ni aibu mazee. Halafu wanawake wa sasa washajua wanaume wa sasa ni maboya tu hivyo wanakanyagia mafuta tu ya kuwaumiza maana washajua hamjui dhamana yenu duniani. Hivi unaanzaje kulia kisa mwanamke?

Wanaume tunapendwa sana na Mungu sijui hamjui au ni vipi hebu tembea mtaani, mitando ya kijamii uone wadada wazuri walivyojazana hao wote wameumbwa ajili ya mwaume awafaidi. Kwa hesabu za haraka duniani kuna watu zaidi ya bilioni 7 wanaume billion 3 na wanawake billion 4, yaani tukisema leo kila mwaume aoe mke mmoja mmoja kuna billion 1 ya wanawake itabaki haina kazi inapuyanga tu.

Logic
ya mungu kuumba wanawake wengi kuliko wanume ni kwamba kila mwaume apate uwanja mpana wa kuchagua mwanamke amtakae, pia kaumba wanawake wengi ili isije kutokea hata kwa bahati mbaya mwaume kuteseka kisa mapenzi/mwanamke.

Mungu anasikitika na kushangaa sana anapoona mwanaume analia na kuteseka kisa mwanamke mmoja wakati kashaumba wengi ni wewe kuchagua tu.

Mungu fundi sana yaani kaumba kikosi cha kwanza cha wanawake kisha akaumba Subs pia ili ikitokea uwanjani mmoja hakabi inavyopaswa basi anatolewa chap sub kutoka benchi anaingia kuendeleza kabumbu sasa wewe mwanaume unaona kabisa player uliyenaye analeta mazabe uwanjani badala ya kumuweka benchi uchukue sub wewe unabaki kulialia, walahi Mungu atawapa kipigo nyie maana mnashindwa kutumia raslimali zake ipasavyoo.

Halafu sasa wanawake hua wanapenda mwanaume mwenye wanawake wengi aua mwenyekuweza kupata mwanamke yoyote wakati wowote usipokua hivyo mwanamke anadharau anajiona keki anajua huna pengine pa kwenda. Hapo ndio utaona mwanaume anaomba msamaha kwa kosa alofanya mwanamke kisa asiachwe. Ngedere wewe

Wanaume achene upuuzi wa kulialia kisa wanawake, simamieni misingi ya uanaume wenu.

-C. Cole
 
By default wanadamu tulipoumbwa kila jinsia ilipewa majukumu yake, jukumu la viumbe wenye jinsia ya kiume (wanaume) wameumbwa kutawala jinisia ya kike (kike) katika kila Nyanja na jinsia ya kike imeumbwa kutawaliwa na jinisa me.
Umesema yote, sahihi kabisa, Mwanamke Anapaswa Kuwa Chini ya Mwanaume, Ila Hii ina gharama yake nayo ni Mwanaume Awajibike ipasavyo na Sio aache kutekeleza majukumu yake

Sent from my SM-C9000 using JamiiForums mobile app
 
Hao wanawake wengi unao wasema
Wengi ni wajane!
Wengi ni single mother
Wengi ni wabibi
Wengi ni wanafunzi

Sasa mkuu unasemaje😂😂😂
Tulia mkuu, takwimu zinaonyesha wanaume ndio wanakufa mapema zaidi kuliko ke. Hivyo bado Reserve bank ya wanawake bado ina stock ya kutosha tu.
Katika hao wanaume Bill3 kuna
  • Mahanithi
  • Wazee
  • Wafungwa
  • Mashoga
  • Watoto
  • Machizi.
Yaani always ratio ya wanawake ni kubwa kuliko me
 
Tulia mkuu, takwimu zinaonyesha wanaume ndio wanakufa mapema zaidi kuliko ke. Hivyo bado Reserve bank ya wanawake bado ina stock ya kutosha tu.
Katika hao wanaume Bill3 kuna
  • Mahanithi
  • Wazee
  • Wafungwa
  • Mashoga
  • Watoto
  • Machizi.
Yaani always ratio ya wanawake ni kubwa kuliko me
Mi nafikiri iliyobaki tukuunge mkono kwa kuongeza list mi naongeza makundi mawili...
.Vibamia
.Madomo zege

Wenye nafasi waongezee
 
Shaurini mtakavyoshauriana
Ila wamiliki wa *tamu ndo sie....

Msisahau alikuwepo Samson ila pia alikuwepo Delilahh..
Tulia wewe huo utamu nyie ni stock tu ila ni mali yetu sie. Ndio maana kitendo cha kunipa huo utamu wako kinaitwa kufanywa yaani ww mwenye utamu ndio umetendewa sio wewe kunitendea mimi Me😅

Samson alikua mwaminifu tu kwa demu na hakua fala kama wanaume wengine.
Kilichomponza ni kumuamini tu demu wake hii inaothibitisha kua wqnaume sisi ni watu waaminifu na wakweli sana
 
Ss mbona mnahangaika😅🤣

Dawa yenu tunaijua tangu zama za Adamu hehe
Tulia ww hakuna anayehangaika hapa nawaweka sawa tu machalii wanaoshindwa kusimamia misingi yao.
Tukio la adamu pia linathibitisha kua wanaume sisi tuna mapenzi ya kweli na tupo waaminifu sana. Ila nyie vivuruge tu, ila sema adamu hakua na option nyingi Mungu alimbania
 
Sio kweli kuwa wanaume wote wanapenda kuongoza,acha kuwa na msimamo potofu,, Kuna wanaume wanapenda wanawake watakao wa challenge na wengine wanapenda kuwa submissive kwa wake zao,...tembea uone
 
Back
Top Bottom