Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 5,628
- 6,411
Suala la kufurahi ni kwa ajili ya wanawake na watoto ila siyo kwa wanaume (akina Baba). Maisha katika zama tunazoishi yamejawa na misongo na matatizo hayahitaji kujionea huruma.
Ikumbukwe unachokitaka wewe na mwingine anakitaka hivyo njia ya pekee hapo ni kupambana na kushinda na siyo kusubiria huruma.
Karibu kila kitu leo kinapatikana kwa kushindana na siyo kuoneana huruma au kujionea huruma "just fight and win".
Akili ya mwanaume inapaswa ikubali kupita katika ugumu kwa saababu ndani ya ugumu huo ndipo yalipo mafanikio. Mafanikio yapo katika kutatua matatizo ya watu na kutatua matatizo ya watu siyo suala la kujionea huruma na kutafuta furaha kama kipaumbele cha maisha kumbuka kupambana na kushinda ndiyo mkao wa akili ya kiume "stress and win".
Watu wana matatizo lukuki yanayohitaji suluhu kutoka kwa watu wengine ambao kwa hakika wanapaswa kuwa katika mtazamo wa kiakili ulio tofauti na wao "stress and win mindset".
Furaha haipaswi kuwa lengo kuu la mwisho la maisha ya mwanaume.