Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 5,628
- 6,411
- Thread starter
- #41
NaamUkishinda ndo furaha yenyewe sasa
NaamUkishinda ndo furaha yenyewe sasa
SahihiUpo sahihi sana Brethren,
Msisitizo wa hoja yangu ni "akili ya kupambana na kushunda bila kujali unajisikia furaha au huzuni, vizuri au vibaya....
Usipopambana hutashinda na usiposhinda hutofurahi. Chaguo la mwanaume kufurahi ni "kupambana na kushinda".Furaha= Health+ Wealth+ Good relationship
Kwamba Mwanaume hatakiwi kuwa na afya njema, utajiri na mahusiano Bora/mazuri.
Kama kuna kiumbe kinapaswa kiwe na furaha basi ni Mwanaume.
Changamoto ninayopitia naona yangu ni mdogo sana Kuna watu wanapitia mazitoSuala la kufurahi ni kwa ajili ya wanawake na watoto ila siyo kwa wanaume (akina Baba). Maisha katika zama tunazoishi yamejawa na misongo na matatizo hayahitaji kujionea huruma.
Ikumbukwe unachokitaka wewe na mwingine anakitaka hivyo njia ya pekee hapo ni kupambana na kushinda na siyo kusubiria huruma.
Karibu kila kitu leo kinapatikana kwa kushindana na siyo kuoneana huruma au kujionea huruma "just fight and win".
Akili ya mwanaume inapaswa ikubali kupita katika ugumu kwa saababu ndani ya ugumu huo ndipo yalipo mafanikio. Mafanikio yapo katika kutatua matatizo ya watu na kutatua matatizo ya watu siyo suala la kujionea huruma na kutafuta furaha kama kipaumbele cha maisha kumbuka kupambana na kushinda ndiyo mkao wa akili ya kiume "stress and win".
Watu wana matatizo lukuki yanayohitaji suluhu kutoka kwa watu wengine ambao kwa hakika wanapaswa kuwa katika mtazamo wa kiakili ulio tofauti na wao "stress and win mindset".
Furaha haipaswi kuwa lengo kuu la mwisho la maisha ya mwanaume.
Usipopambana hutashinda na usiposhinda hutofurahi. Chaguo la mwanaume kufurahi ni "kupambana na kushinda".
Ndivyo ilivyo kadiri ya ugumu ulivyo ndivyo na ushindi ulivyo. Nguvu inayotumika kupita pagumu ndiyo nguvu ya ushindi...Changamoto ninayopitia naona yangu ni mdogo sana Kuna watu wanapitia mazito
Sawa sawaUsipopambana hutashinda na usiposhinda hutofurahi. Chaguo la mwanaume kufurahi ni "kupambana na kushinda".
Kupambana siyo kuteseka Mkuu, tafakari taratibu.Sio kila mafanikio lazima yatokee kwenye mchakato mgumu, wapo watu wengi wanapitia michakato migumu na hawajafanikiwa na hawatafanikiwa vilevile.
-Lengo la kutafuta mafanikio ni nini kama hakutakuwa na furaha ndani yake??
-Unataka ufanikiwe ili iweje??
-Ukishatatua hayo matatizo lukuki ya watu what next??
-Unataka mafanikio yanini kama furaha sio kipaumbele cha maisha yako?
Ukiamua kujitesa uwe na uhakika na matokeo ya mateso yako sio kila jambo linalokuja mbele yako unawaza kujitesa, utajitesa na kaulimbiu zako za kizamani mwanaume mateso na haufanikishi chochote.😂😂😂
Kwani wewe kipato changu unakijua? Au unajua kinavyo patikana? kama una magumu yanayofanya usipate furaha hiyo ni shida yako mzee usitafsiri maisha ya wengine kwa kutazama ya kwako, tulia kabisafuraha ipi wewe una kipato Gani Cha kuwa na furaha utafutaji upo ulio nao wewe maisha ya mwanaume yamejaa steres 99;9 na kama ni furaha ni asilimia Moja na inakuja mara Moja na kuondoka?