Mwanaume hakuumbwa kufurahi: Aliumbwa kupambana na kushinda

ni sawa, lakini jambo ambalo unatakiwa kujua ni kuwa FURAHA ni tunda la Roho Mtakatifu. Mtu mwenye Roho wa Mungu regardless ana hali gani ya kiuchumi huwa na furaha, kwa sababu furaha ni zao la Roho Mtakatifu ndani ya moyo wa mtu.

Gal 5:22
Sio rahisi kuwa na furaha kama uchumi umekugonga ugoko, haya nadharia zinatumika kujifariji tu!
 
Unaposema "hakuumbwa kufurahi" unamaanisha nini kwanza?

Hakuumbwa na nani/nini?
 
Kitu unachopaswa kujua ni kwamba maisha hayalingani kama kwako maisha hayakupi kipande cha furaha huyo ni wewe na shida zako, lakini wengine maisha yetu yana sehemu kubwa ya furaha na tunatafuta kwa nguvu zetu wenyewe, acha kukariri unatakiwa kuelewa
 

Unakuta dume Zima lina miaka 30 na kuendelea linasumbua watu kwa kupost na kuwapigia simu eti ni birthday yake linataka uli wish na linafanya na sherehe
 
Mkuu sijaandika kuwa sitaki furaha hapo ila hoja ipo hivi "furaha siyo lengo kuu la maisha ya mwanaume" ...
Ifanye hiyo kua namna yako ya kuishi, lakini usituzungumzie wanaume kana kwamba umekua msemaji wetu, kila mmoja na namna ya kuishi maisha yake
 
Kufurahi kwangu mara nyingi naona inakuja na matokeo chanya ama tarajio fulani linapotimia unafurahi,


Wengi kutokana na ugumu wa maisha, kuumizwa kihisia, kisaikolojia, matarajio kuenda tofauti na tulivyo panga..... Tunakuwa na ile furaha ya kulazimisha tuu, uonekane upo sawa!!!

Furaha ndani ya moyo, akili na utulivu ni Bora zaidi
 
Siyo lazima hoja hii ieleweke kwa namna ambayo kila mtu anataka ila nilichokiandika kimetokana na uzoefu wangu tu wa kawaida na sikatai kukosolewa kwa sababu kila mmoja ana namna ya kuuona ulimwengu wake. Hatuono kwa namna ileile...
Ambacho sijipingi ni uhakika kuwa akili ya kupambana na kushinda ndiyo furaha ya kiume "fight and win mindset"
 
Sometimes furaha kwa mwanaume ni kwa ajili ya kuishi afya ya akili na kufanya maamuzi sahihi.
Maamuzi sahihi ya kiume katika zama hizi ni kupambana na kushinda "fight and win"
Happiness is not the ultimate goal
 
Maamuzi sahihi ya kiume katika zama hizi ni kupambana na kushinda "fight and win"
Happiness is not the ultimate goal
Kama furaha si lengo kuu la mwanaume, unadhani mwanaume anaishi kwa ajili ya mafanikio tu au kuna thamani ya kiroho, kihisia na kijamii ambayo haiwezi kupatikana kwa "kupambana na kushinda" pekee?
 
Hiyo ni kwa wananaume waliotoka familia masikini tu
 
 
Furaha ni kitu natural haijalishi una achievement kiasi gani
Upo sahihi sana Brethren,
Msisitizo wa hoja yangu ni "akili ya kupambana na kushunda bila kujali unajisikia furaha au huzuni, vizuri au vibaya....
 
Sio rahisi kuwa na furaha kama uchumi umekugonga ugoko, haya nadharia zinatumika kujifariji tu!
Hiyo ni kwako. Furaha ya Roho Mtakatifu hailetwi na pesa.

kuna mtu ana mamilioni kama sio mabilioni benki lakini hana furaha kumlinganisha na mtu mmoja pale kijijini aliyekula ugali wake na mboga yake pendwa, na hata hajui kesho atakula nini.

these things are deep!
 
Kitu unachopaswa kujua ni kwamba maisha hayalingani kama kwako maisha hayakupi kipande cha furaha huyo ni wewe na shida zako, lakini wengine maisha yetu yana sehemu kubwa ya furaha na tunatafuta kwa nguvu zetu wenyewe, acha kukariri unatakiwa kuelewa
furaha ipi wewe una kipato Gani Cha kuwa na furaha utafutaji upo ulio nao wewe maisha ya mwanaume yamejaa steres 99;9 na kama ni furaha ni asilimia Moja na inakuja mara Moja na kuondoka?
 
Mkuu umeijenga hoja yako katika mawanda ambayo kueleweka inahitaji kuwa na akili ya akili.
Si unafahamu mambo ya kiroho kwao wasio wa roho ni upumbavu?..
Wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…