Mwanaume kabla ya kuoa hakikisha uko vizuri kwenye mambo ya kimila au ya kanisani/msikitini

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Ni kama masikhara ila jomba hakikisha unakuwa uko fit sana kwenye kimojawapo. Kama umeamua kuwa mtu wa kanisa au msikitini basi hakikisha unashikilia sana huko. Kwa wale wazee wa mambo ya kimila hakikisha uko fit mno. Kazindikwe huko Ziwa Tanganyika siku kadhaa kabla ya kuoa. Usiwe vuguvugu.

Mimi nimeandika hivi baada ya kupata experience huko kwenye wataalamu wa sayansi ya asili. Wanawake wengi sana huenda huko kuwatengeneza wanaume zao. Enzi nikiwa mdhambi nilikuwa nina mahudhurio mazuri huko nikaona mabinti wadogo hadi kina mama watu wazima wakipanga foleni kwa wataalamu. Shida yao kuu ni kuwatengeneza wanaume wawatii. Hali ni mbaya sana. Hawa wanaoitwa NICE GUYS wengi wao wametengenezwa. Sio akili zao.

Sikushauri uwe mchawi ila kama mwanaume kaa chini tafakari uchague upande sahihi. Mimi nilikuwa upande wa mambo ya kimila ila niliyatupilia mbali baada ya kuona ni upuuzi kuishi kwa masharti.
 
Wanawake wanaotoka Kwenye familia za kichawi ndio wana hizo tabia za kuwaroga waume zao na kuwageuza ndondocha.

Ila ukioa binti aliyelelewa Kwenye misingi ya kidini huwezi mkuta akimfanyia mumewe huo upuzi wa kumroga.

Jamani tuweni makini Sana wanawake tunaotaka kuoa
 
Nabii Mussa aliomba dua nzuri sana akapewa mke mwema alisema
"Rabi inni lima anzalta ilayya min khayrin fakir"
Maana yake "Eeh Mungu hakika mimi ni muhitaji wa kila heri utakazonipa"

Kwa sisi watu wa imani tunashauriwa tuombe dua kama hii tunapotafuta wake au wanawake wanapotafuta waume.
 
Wanawake wanaotoka Kwenye familia za kichawi ndio wana hizo tabia za kuwaroga waume zao na kuwageuza ndondocha.

Ila ukioa binti aliyelelewa Kwenye misingi ya kidini huwezi mkuta akimfanyia mumewe huo upuzi wa kumroga.

Jamani tuweni makini Sana wanawake tunaotaka kuoa
Fact
 
Hivi wenye hela nao wanarogwa? kwa mfano tusikie Bakhresa kapewa limbwata au usikie mama Samia kampa limbwata mumewe au haya mambo yako uswahilini
Mambo ya uswahilini hayo, ushuani huwezi kuta upuzi Kama huo
 
Wanawake wanaotoka Kwenye familia za kichawi ndio wana hizo tabia za kuwaroga waume zao na kuwageuza ndondocha.

Ila ukioa binti aliyelelewa Kwenye misingi ya kidini huwezi mkuta akimfanyia mumewe huo upuzi wa kumroga.

Jamani tuweni makini Sana wanawake tunaotaka kuoa
Wanawake wengi hubadilika.. halafu ishu ya kuroga haifanyiki hadharani ni suala la kificho mno. Huko kwa waganga utakuta mwanamke aliye mstari wa mbele kanisani yupo anasubiri tiba. Au mama anayeheshimika kanisani kampeleka binti yake.
 
Wengi wanarogwa Na michepuko
 
Wanawake wengi hubadilika.. halafu ishu ya kuroga haifanyiki hadharani ni suala la kificho mno. Huko kwa waganga utakuta mwanamke aliye mstari wa mbele kanisani yupo anasubiri tiba. Au mama anayeheshimika kanisani kampeleka binti yake.
Hawezi kubadilika tu mwenyewe labda awe amepata toxic friends wanaompa ushauri wa kumroga mumewe.

Hakuna watu wanaowapotosha wanawake Kama mashoga zao.
 
Back
Top Bottom