Mwanaume kuwa makini na 'Dinner dates'

Mwanaume kuwa makini na 'Dinner dates'

Ni kweli umetushauri vyema ila nikwambie ukweli tu "yamepitia kulia yametokea kushoto!"
Kesho tu tarajia mtu anakuja analia amepuruswa mpk hela ya ada!.
😂😂😂😂 daah umenichekesha Mkuu
 
Kibongo bongo mdada anaweza kukualika na bado akataka ulipe bill zote. Last weekend kuna demu alinicheki akaniambia twende kwenye show ya cristian bella, nikamwambia ok but we will split all bills. Yule dada akapotea hewani
Wanapenda kulipiwa mpaka condom wakati ni kwa ajili ya protection yake mwenyewe
 
Hayo mapicha yamenikera sana....kila baada ya paragraph picha tena yanajirudia nimeacha kusoma
 
Vijana mnasikitisha sana,
Anayetoa idea ya out ndie anaetakiwa kulipa
Mwanaume ukiwa ndio unalipa, lazima uchague pa kwenda, siyo uchaguliwe
Mmoja tulipanga date nikamwambia eneo, yeye akataka kujua excatly jina la eneo.
Nikamuuliza kwani unataka kutanguliza watu wakaniteke au kuweka dawa za kulevya, nikamwambia hutaki acha.
Vijana acheni udhaifu
 
Yan dinner ya shilling 10k 15k nayo alipie mschana ebu Tulia kwanza mkuu Ungenambia labda nauli ya bus akiomba na hela ya kula njiani huyo ni madako
 
Wanapenda kulipiwa mpaka condom wakati ni kwa ajili ya protection yake mwenyewe
Wakati wanapigania usawa hawakuwaza kama haki sawa itakuja na wajibu sawa, matokeo yake ndio haya sasa wanaitaka nafasi ya provider lakini hawautaki wajibu unaomfanya provider kupewa iyo nafasi
 
Inatagemea na destiuri za watu wa nchi hiyo

Marekani / europe mnaweza kusplit the bill… au mmojq akalipa
Kibongo bongo hata unayemuita aje kula hata nauli ya kuja anadai hana so inabidi umtumie nauli ili aje kula pesa zako .. pathetic..! uaidate na watu wa namna hii
 
Katika enzi hizi za usawa wa kijinsia, ni muhimu kuchunguza kwa kina mabadiliko yanayohitajika katika uhusiano wa kimapenzi. Ni muhimu kuzingatia kwamba uhusiano wenye afya unajengwa juu ya msingi wa heshima, uwajibikaji, na uelewano wa pande zote.
View attachment 3178890
Mada ya nani anapaswa kulipa kwenye dinner date imekuwa eneo la utata kwa muda mrefu. Katika ulimwengu wa leo, ambapo wanawake wengi wana kazi na wanaweza kujitegemea kifedha, wazo la mwanamume kulipa kila kitu linaweza kuonekana kuwa la kizamani.
View attachment 3178896

Kubalianeni kuwa mtaenda sehemu gani na kiwango cha mwisho cha matumizi, kwa mwanaume tumia muda mwingi kumpa ushauri mtoto wa kike sehemu isiyo na gharama, iwe ni Restaurant au Take Away Center, eneo la kawaida, mwambie kuwa itakuwa ni sehemu yenye chakula cha bei ya kitanzania, wali maharage, ugali nyama na vyakula vya kawaida, endapo mwanamke atabadilika na kuchukia basi fahamu huyo sio mtu atayeweza kuishi maisha ya ugali dagaa (bomu hilo).

Katika hali ambapo mwanamke hajavutiwa na mwanaume, ni haki kabisa kwa mwanamke kushiriki katika gharama za dinner date. Hii inasaidia kuzuia hali ambapo mwanaume anaishia kulipa kwa kitu ambacho hakikuwa cha kuridhisha kwa pande zote.
View attachment 3178894

Kumbuka wewe sio mtetezi wake, na upo hapo kwa ajili ya kuangalia kama mnaweza kubond! Na kubwa zaidi, mwanaume agiza vitu vya gharama ndogo ili kumpima akili yake, agiza maji makubwa halafu mruhusu yeye aagize chochote (kaa pembeni uone masikini akiwa ameruhusiwa kujiachia). Kufahamu gharama na kuwa economical ni kitu cha msingi sana, haina maana mdada una buku tano ya nauli tu halafu umeagiza savanna tano peke yako?! Haupo serious. Mmekwenda kuzungumza sio kula pekee bi mdada.
View attachment 3178892

Suala jingine ni ustaarabu baina yenu, Ustaarabu ni sifa muhimu katika uhusiano wowote. Umempa taarifa aje yeye basi mwambie akiongezeka kiumbe mwingine hamtokuwa na dinner date, na ukiwaona kwa mbali majenerali wenye njaa kali wanakuja basi jikatae polepole.
View attachment 3178895

Mwanamke na mwanaume wanapaswa kufika kwa wakati. Ucheleweshaji usio na sababu unaweza kuonyesha ukosefu wa heshima ya muda na inaweza kuathiri mtazamo wenu kuhusu uhusiano huo. Kama mmepanga kukutana saa 12 jioni basi kitanzania kufika saa 12 na dakika 10 ni sawa ila ni ajabu kuona mpaka saa 1 na nusu bado hujafika na ukidai kuwa upo njiani (mdau mmoja alisema akitaka boda 🏍 mwambie apande bolt 😃)

Kwa upande mwingine, mwanaume hapaswi kusubiri kwa muda mrefu zaidi ya dakika 30. Hii inaonyesha heshima katika kutunza muda wako mwenyewe na inamzuia kupoteza muda ambao angeweza kutumia na mtu mwingine au jambo jingine.
View attachment 3178896

Ni ujinga wa kiwango cha lami kuona unamsubiria mtoto wa kike ambaye amekupa taarifa ametoka kwao saa 9 na mpaka saa 1 na nusu hajafika, jiongeze chap, endelea na ratba zako.

Watu wachache sana huongea kuhusu hili, ila kabla ya ndoa, kila mtu anapaswa kuwajibika kwa maisha yake mwenyewe.
View attachment 3178895

Mwanamke anapaswa kujitahidi kujitegemea kifedha pasipo kumfanya mwanaume kitega uchumi. Hii itawasaidia wote kuwajibika katika jambo lolote linalowahusu, katika andiko lililopita nilizungumzia upuuzi wa baadhi ya wanawake kudai pesa ya nauli, nywele, pamoja na mavazi kwa ajili ya kukutana kwenye date.
View attachment 3178892

Swali la msingi, je baada ya date, hivyo vitu utavirudisha? Nywele utazirudisha? Viatu na nguo utazirudisha ama? Watoto wa kike wengi wana lugha za kitapeli kwa wanaume. Mnazungumza misamiati ya kikahaba kwa wanaume kuwa ili apate muda wako kwa ajili ya mahusiano ni lazma akununue. Wewe ni mtu mzma tafuta kazi upate kununua mahitaji yako.
View attachment 3178894

Wazazi na walezi wanaweza kusaidia katika malezi ya mwanamke, kifedha na kimawazo, ila mwisho ni jukumu lake mwenyewe kuhakikisha kuwa anaweza kujitunza mwenyewe. Hii inamuwezesha kufanya maamuzi huru na kuishi maisha anayotaka, pasipo kuingiliwa na mwanaume mwingine.
View attachment 3178893

Wakati wa tukio, mawasiliano ya wazi ni muhimu sana. Mwanaume anapaswa kuuliza maswali ya kina kuhusu uhusiano, maadili, na malengo ya maisha ya mwanamke. Hii inamsaidia kuelewa utu wake na kuona kama kuna changamoto za kihisia. Mwanaume ukiona mwanamke yupo busy na simu yake kwa zaidi ya 40% mara yupo Tiktok, Instagram na Kucheza Candy Crush basi nikuombe tu, simama omba ruhusa ya kwenda toilet kisha angalia nafasi ya kuondoka, muache atumie simu yake na bill atalipa yeye.
View attachment 3178892

Mwanaume anapaswa kuwa makini na ishara za mwanamke anazozifanya akiwa mbele yako. Ikiwa anaonekana kuwa hajakubaliana na kitu fulani au ikiwa anaonyesha ishara za kutokupendezwa, mwanaume anapaswa kuheshimu hilo na kumpa nafasi yake ya maamuzi.

Ukijaribu kumshika mkono na anakwepesha jiongeze, huyo yupo na business zake! Ukimuangalia machoni anakwepesha macho, jiongeze bro, huyo sio wako! Njaa ndo imemleta hapo. Ukikutana na mdada yupo serious kama mwanasayansi wa Kirusi, hapo hakuna kitu, jiongeze brother. Dada majibu yake ni YES, NO wala hakuna ufafanuzi, yeye ni Kibu Denis kwenye mishikaki iliyopo mezani! Hapo hakuna kitu.
View attachment 3178890

Ukifika eneo la tukio, weka simu yako silent au vibration na wekeza umakini wako kwa mtoto wa kike, ukimwambia aache kutumia simu na akawa hajapendezwa na hilo basi maliza kinywa chako na fanya kuomba Bill lipia ulichokitumia wewe na mwambie mhudumu kuwa gharama za mtoto wa kike atalipa yeye, acha kuwa simp kabsa.
View attachment 3178891

Uhusiano wenye afya unajengwa juu ya msingi wa heshima, uwajibikaji, na mawasiliano ya wazi. Ni muhimu kwa wanaume na wanawake kuelewa majukumu yao na kuheshimu mipaka ya kila mmoja. Date sio kwa ajili yako peke yako, ni kwa ajili yenu, ukiona yupo busy na mambo yake ina maana yupo na biashara zake zingine, vaa uanaume na mshukuru Mungu kwa siku nyingine, kisha ondoka.

KUMBUKA NYINYI WOTE NI WATU WAZMA! NA MNATAFUTA KUANZISHA UHUSIANO! NYIE SIO WATOTO! HIVYO KAMA MNATAKA KUFANYA MICHEZO MKUBALIANE KUWA MNATAKA MICHEZO.
Binti zangu huwa nawashauri kuhakikisha akipata mwaliko ahakikishe:-
1. Mfukoni ana gharama ya usafiri wa taxi ya kutoka alipo hadi anapolala;
2. Chakula anachoagiza lazima ahakikishe mfukoni ana hela ya kukilipia;
3. Asinywe kilevi chochote; na
3. Awe na hela ya ziada ili ikiwezekana alipe gharama za mtoko husika.
 
Mambo mengine ni kifala.

Atakae anzisha mada ya date na kumuita mwenzake ndo alipie
 
Back
Top Bottom