Hahah inategemea na kosa na kiwango cha thamani yako kwangu kilichobakia moyoni. Maana kero huwa zinashusha thamani ya upendo hasa zikiwa mara kwa mara.
Pia kuna wasichana ambao yeye anapenda attention sana ila hana mbinu za kiintelijensia za kuipata toka kwa mpenziwe, anachoona rahisi ni kuanzisha ligi ili mbishane tu mwishowe unamchoka sasa. Hii ni kwa wenye vile vi age vya 21-25! Kuna mmoja kala Red Card kwa sababu hio, mie sipendagi kelele af nashikwaga na hasira sana ila analazimisha msuguano ili tu asikie naongea tu hata kwa ubishani usio na maana...Really turns me off na sitakaa nikubembeleze kwa vitu vya namna hio.
Kanuni niliojiwekea, tukigombana nikachukia nikilala nikaamka nakuwa fresh kama kitu kibaya hakijatokea last night. Huwa si hold ugomvi au hasira, new day i'm refreshed na nashukuru mungu bibie amesha adopt hilo.
Hayo mambo ya kununiana week nzima au miezi naona ni utoto tu.