Jeshi la Polisi limelazimika kuwahi eneo la tukio na kuingilia kati taharuki iliyojibuka Kimara Mwisho, Wilayani Ubungo Mkoani Dar es salaam jioni hii baada ya Wananchi wa eneo hilo kumpiga Mwanaume mmoja anayedaiwa kupoteza sehemu za siri za Mkazi mmoja wa Kimara baada ya kumshika begani.
Japokuwa bado Mamlaka hazijathibitisha kupotea kwa
sehemu hizo za siri za Mkazi huyo wa Kimara Mwisho, baadhi ya Mashuhuda waliozungumza eneo la tukio wamenukuliwa wakisema wamemkamata Mtu aliyeiba “mali ya Mwanaume”.
Shuhuda aitwae Kundaeli ambaye ni Mkazi wa Kimara mwisho, amesema Mtu ambaye amedai sehemu zake za siri kuyeyuka alikuwa akiendelea na shughuli zake za Ufundi wa pikipiki na ndipo alipojitokeza Mtu huyo na kumuomba chenchi na kumshika bega kitendo kilichomfanya aanze kutetemeka na kupagawa akitokwa jasho na kuwaambia wenzake kuwa uume wake umepotea.
Soma Pia: Mtu anayedaiwa akigusa nyeti zako zinapotea azua taharuki Tunduma