Mwanaume mmoja nchini Nigeria amjeruhi vibaya mkewe baada ya vipimo vya DNA kuonesha kuwa watoto wao watatu sio wa mwanamme huyo

Mwanaume mmoja nchini Nigeria amjeruhi vibaya mkewe baada ya vipimo vya DNA kuonesha kuwa watoto wao watatu sio wa mwanamme huyo

Mkuu watoto watatu alaf umuache tu burebure iviivi dah

Sent using Jamii Forums mobile app
Vijana katika ujana wenu jitahidi uwe na mtoto 1 au 2 ili ukiingia kwenye ndoa uwe na wa nje
Hili likikufika angalau hata umfukuze au mmeachana usiumie kivile coz ziada ipo.
Hakuna kitu inauma kama mtoto mapendo yote yale leo sio wako dah sijui kifua gani hicho cha kutunza hilo!
Yote 9 kuanza 1 jambo lo lote inauma mno kupoteza muda, pengine wa mwisho labda ana miaka 10 just imagine unaanza 1 mimba kakue kaanze shule kamalize we nae umri ndo huo unasonga yaani huyo mke ashukuru kug’olewa meno na sura kuparuliwa
Mi ningemuuwa potea mbali. Shida sio Canada shida hawa sio damu yangu! Cheza rough ujanani hilo ndo nimejifunza kwa hiki kisa!
 
Itakuwa huyu Mwanaume hana uwezo wa kutungisha mimba,haiwezekani mpo kwenye ndoa mnagegedana mimba haitungi lakini akichepuka tu ndo anapata mimba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama vile ambavyo wapo wanaume wana watoto nje ya ndoa vile vile wapo wanawake. uwe me au ke kama huwezi samehe ukalea achaneni kwa amani.
Kosa sana kutaka wote me/ke wawe sawa kwa kila jambo, Mume mume tu ndo maana unaacha watoto unaolewa kwingine mme hata akioa tena watoto ni mme tu
 
Ni vyema wakapime atoe ridhaa mwenyewe.
Wapo wengine wapo tayari akuache huru na asitake tena kuoa kuliko kuchukua maamuzi mwenyewe hatari namna hiyo.
Hapo utakuta jamaa alikuwa anahela kwa hiyo akataka kuwakuzia watoto wake kwa hela za jamaa ili baadae amuue abaki na mali, watoto na baba mzazi. Hii sio poa.
Ni dhulma kwa jamaa na jamii yake pia iliyomuhangaikia kusomesha

Sent using Jamii Forums mobile app
Pia unaweza kuta hata baba zao wazazi na hao watoto hawajui km walizaa na huyo mwanamke. (Labda sio mmoja ni watatu tofauti) na mwanamke alifanya ivyo ili kudumisha ndoa yake.
 
Kuna website naipenda sana kwa kuangalia kama habari ni ya kweli au uongo Snopes.com

Humu ukileta habari za Snopes.com ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.

Nilizileta sana humu habari za snopes mwaka 2016. Kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa Marekani.

Kulikuwepo na uzushi mwingi sana dhidi ya Donald Trump kusema maneno ya kashfa dhidi ya Waafrika.

Nikajaribu hata ku-reason na watu kwamba, ni vigumu sana kwa Trump kusema maneno kama hayo halafu media ya Marekani, ambayo kwa kiasi kikubwa ni anti-Trump, kupuuza maneno kama hayo na wasiyatumie dhidi yake.

Nikajaribu ku-reason na watu pia, kwamba, ni vigumu sana Trump aseme maneno kama hayo halafu wapinzani wake kwenye primaries wakae tu kimya wasiseme kitu.

Nikaleta na habari za snopes zilizo debunk huo uzushi.

Lakini wapi. Watu waliamini tu waliyokuwa wanayasoma mtandaoni.

Nikahitimisha kuwa idadi ya wajinga na wapumbavu ni kubwa kuliko nilivyokuwa nadhania mwanzoni.
 
Ila yote kwa yote jamaa alichokifanya sio fair kabisa,Usijekuta mashine za Dna zilisoma vibaya
 
Kosa sana kutaka wote me/ke wawe sawa kwa kila jambo, Mume mume tu ndo maana unaacha watoto unaolewa kwingine mme hata akioa tena watoto ni mme tu

hamna anayetafuta ushindani ila jambo moja ni hili mwanadamu kwa asili ni mdanganyifu. hili jambo halina cha ke au me ukiweza msamehe mwenzio lea huwezi achaneni kwa amani.
 
Canada wanafanya DNA testing kwenye immigration, kwa hivyo msingi wake upo, kwa nini unasema habari ni ya uongo?

Nilikuwa najiandaa kuhoji ukweli wa habari kwa misingi ambayo umeiletea ushahidi na hivyo naondoa shaka yangu juu ya taarifa hii.
 
Nilikuwa najiandaa kuhoji ukweli wa habari kwa misingi ambayo umeiletea ushahidi na hivyo naondoa shaka yangu juu ya taarifa hii.
Ndugu yangu naona tunafikiri sawa katika mambo fulani.

Suala la DNA ni nyeti sana. Habari ilivyokaa ni suspect sana.

Kwa watu wa caliber fulani, kuhoji habari ni lazima.

Ukianza kuhoji tu, nakupandiaha cheo. Kwa maana ni rahisi sana kufikiri kwamba Canada wamefikia ustaarabu wa kusema hawatagusa DNA.

Kwa maana, kama baba kampenda mke na mtoto anayejua si wake kibaiolojia, despite DNA, hapo serikali ya Canada itamkataliaje mtu aliyemtunza mtoto kwa miaka 17 na kumwambia himuyu si mtoto wako?

Hivi Eatanzania wakiambiwa leo Julius Kambarage Nyerere si mtoto wa Kibaiolojia wa Chifu Burito Nyerere, ni mtoto wa Mama na mtu mwingine tu, hiyo Chifu Burito Nyerere ubaba wake utatoweka licha ya kuwa father figure na kumlea na kumsimesha Julius Kambarage?

Hili si swali hypothetical tu.

Ni swali la kweli

Wazee Watiama wanaojua historia wanasema Julius si mtoto wa Chifu Burito.

Nilijadikiana sana na muandishi mmoja wa kitabu cha maisha ya Nyerere, mwisho nikqmwambia, kama Chifu Burito ni Baba wa kibaiolojia au si baba si kitu muhimu sana.

Kwa sababu, Waswahili walisema "Udugu ni kufaana, si kufaana".

Maana yake, anayekufaa katika dhiki ni ndugu yako kuliko anayefanana nawe, lakini hataki kukufaa.

Chief Burito alimfaa Mwalimu Nyerere sana kumlea na kumsomesha, kumkubali tu kama mwanawe. Hilo lilitosha kumfanya Julius Kambarage Nyerere kuwa mwanawe. Hata kama hakuna udugu wa damu.

Sasa mtu kama Chief Burito - hata kama si Baba wa kibaiolojia- ukienda kumpa mitihani ya DNA, itakuwa umemtendea haki kweli yeye au mtoto?"

Yesu - namtaja kama mwanafalsafa, si Mungu- katika hadithi ya Msamaria mwema, aliuliza. Jirani yako ni yupi? Mtu wa kabila yako aliyekuacha pembeni ya njia umepigwa? Au mtu asiye wa kabila yako aliyekuokota pembeni ya barabara na kukuhudumia majeraha yako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom