Nilikuwa najiandaa kuhoji ukweli wa habari kwa misingi ambayo umeiletea ushahidi na hivyo naondoa shaka yangu juu ya taarifa hii.
Ndugu yangu naona tunafikiri sawa katika mambo fulani.
Suala la DNA ni nyeti sana. Habari ilivyokaa ni suspect sana.
Kwa watu wa caliber fulani, kuhoji habari ni lazima.
Ukianza kuhoji tu, nakupandiaha cheo. Kwa maana ni rahisi sana kufikiri kwamba Canada wamefikia ustaarabu wa kusema hawatagusa DNA.
Kwa maana, kama baba kampenda mke na mtoto anayejua si wake kibaiolojia, despite DNA, hapo serikali ya Canada itamkataliaje mtu aliyemtunza mtoto kwa miaka 17 na kumwambia himuyu si mtoto wako?
Hivi Eatanzania wakiambiwa leo Julius Kambarage Nyerere si mtoto wa Kibaiolojia wa Chifu Burito Nyerere, ni mtoto wa Mama na mtu mwingine tu, hiyo Chifu Burito Nyerere ubaba wake utatoweka licha ya kuwa father figure na kumlea na kumsimesha Julius Kambarage?
Hili si swali hypothetical tu.
Ni swali la kweli
Wazee Watiama wanaojua historia wanasema Julius si mtoto wa Chifu Burito.
Nilijadikiana sana na muandishi mmoja wa kitabu cha maisha ya Nyerere, mwisho nikqmwambia, kama Chifu Burito ni Baba wa kibaiolojia au si baba si kitu muhimu sana.
Kwa sababu, Waswahili walisema "Udugu ni kufaana, si kufaana".
Maana yake, anayekufaa katika dhiki ni ndugu yako kuliko anayefanana nawe, lakini hataki kukufaa.
Chief Burito alimfaa Mwalimu Nyerere sana kumlea na kumsomesha, kumkubali tu kama mwanawe. Hilo lilitosha kumfanya Julius Kambarage Nyerere kuwa mwanawe. Hata kama hakuna udugu wa damu.
Sasa mtu kama Chief Burito - hata kama si Baba wa kibaiolojia- ukienda kumpa mitihani ya DNA, itakuwa umemtendea haki kweli yeye au mtoto?"
Yesu - namtaja kama mwanafalsafa, si Mungu- katika hadithi ya Msamaria mwema, aliuliza. Jirani yako ni yupi? Mtu wa kabila yako aliyekuacha pembeni ya njia umepigwa? Au mtu asiye wa kabila yako aliyekuokota pembeni ya barabara na kukuhudumia majeraha yako?
Sent using
Jamii Forums mobile app